Tafuta

Siku ya vijana kimataifa 2024:Kutoka Mibofyo hadi Maendeleo:Njia za Kidijitali za Vijana kwa Maendeleo Endelevu. Siku ya vijana kimataifa 2024:Kutoka Mibofyo hadi Maendeleo:Njia za Kidijitali za Vijana kwa Maendeleo Endelevu.  (@jugomedia)

Siku ya Kimataifa ya Vijana 2024 inaakisi uhusiano wa kidigitali na maendeleo endelevu!

Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Vijana 2024 inayoadhimishwa tarehe 12 Agosti ni:"Kutoka Mibofyo hadi Maendeleo:Njia za Kidijitali za Vijana kwa Maendeleo Endelevu."Mada hii inaakisi uhusiano muhimu kati ya uwekaji wa kidigitali na kuharakisha maendeleo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) huku ikisisitiza michango muhimu ya vijana katika mchakato wa mabadiliko.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ya Kimataifa ya Vijana huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 12 Agosti ili kuleta masuala ya vijana kwa jumuiya ya kimataifa na kusherehekea uwezo wa vijana kama washirika katika jamii ya kimataifa ya leo hii. Siku hiyo inatoa fursa ya kusherehekea na kujumuisha sauti, vitendo, na mipango ya vijana, pamoja na ushirikiano wao wa maana, wa ulimwengu wote na wa usawa. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) lilianzisha Siku hiyo tarehe 17 Desemba 1999, baada ya kuidhinisha pendekezo lililotolewa na Mkutano wa Dunia wa Mawaziri Wanaohusika na Vijana uliotaka tarehe 12 Agosti kutangazwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Vijana.

Ujumbe wa Video wa UN Habitat: Siku ya Kimataifa ya Vijana 2024

Kwa mwaka 2024  Siku hiyo inaongozwa na Kauli Mbiu: “Kutoka Mibofyo hadi Maendeleo: Njia za Kidijitali za Vijana kwa Maendeleo Endelevu.”  Kwa njia hiyo wanabainisha kwamba uwekaji kidigitali unabadilisha ulimwengu wetu, ukitoa fursa ambazo hazijawahi kushuhudiwa ili kuharakisha maendeleo endelevu. Teknolojia za kidijitali kama vile vifaa vya mkononi, huduma, na Akili Mnemba(AI) ni muhimu katika kuendeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Ujumbe kutoka kwa UNDESA USG Li Junhua kwa Siku ya Vijana 2024

Data inayotokana na mwingiliano wa kidijitali inasaidia kufanya maamuzi kulingana na ushahidi. Kukiwa na athari kubwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kimazingira, teknolojia za kidijitali na data huchangia angalau asilimia 70 ya malengo  'ya 169 ya SDG huku ikiwezekana kupunguza gharama ya kufikia malengo haya kwa hadi dola trilioni 55. Vijana wanaongoza katika kupitishwa na uvumbuzi kidijitali, huku robo tatu ya wale walio na umri wa miaka 15 hadi 24 wakitumia intaneti mwaka wa 2022, kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuliko vikundi vingine vya umri. Hata hivyo, tofauti zinaendelea, hasa katika nchi za kipato cha chini na miongoni mwao ni  wanawake vijana, ambao mara nyingi wana ufikiaji mdogo wa mtandao na ujuzi wa kidigital ikilinganishwa na wenzao wa kiume.

Ujumbe wa video kutoka kwa Doreen Bogdan-Martin, Katibu Mkuu, ITU

Ingawa kuna hitaji la dharura la kuimarisha ujumuishaji wa kidijitali, vijana wanatambulika kwa kiasi kikubwa kama "wazaliwa wa kidijitali," wakitumia teknolojia kuleta mabadiliko na kuunda masuluhisho. Kadiri muda wa mwisho wa 2030 wa SDGs unavyokaribia, jukumu la vijana katika uvumbuzi wa kidijitali ni muhimu kwa kushughulikia masuala ya kimataifa.

Ujumbe wa Video kutoka kwa Carol Roach, Mwenyekiti wa IGF kwa Siku ya Kimataifa ya Vijana 2024

Kwa kusherehekea michango ya kidijitali ya vijana, tunaweza kuhamasisha uvumbuzi zaidi na ushirikiano kuelekea kufikia maendeleo endelevu.

Siku ya Vijana Kimataifa 2024
12 August 2024, 15:39