Tafuta

Migogoro nchini Sudan imesababisha kuwahama kwa watu wengi Migogoro nchini Sudan imesababisha kuwahama kwa watu wengi  (AFP or licensors)

Sudan Kusini:Jumuiya ya Mt.Egidio yakutana na serikali na makundi ya upinzani yenye silaha

Hivi karibuni ulifanyika mkutano jijini Roma kati ya Serikali na makundi ya upinzani yenye silaha ya Nchini Sudan kusini uliohamasishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.Katika mkutano huo wa kwanza baada ya miezi kadhaa kati ya serikali ya Sudan Kusini na viongozi wa makundi ya upinzani,vyama hivyo vilieleza nia ya kuendelea njia ya mazungumzo kama suluhisho pekee la mzozo wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mkutano wa ngazi ya juu, ili kuweka matumaini ya amani hai nchini Sudan Kusini, ulifanyika siku za hivi karibuni katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio jijini Roma. Waliokuwepo ni mjumbe maalum wa rais wa Sudan Kusini, balozi Albino Aboug, ujumbe wa makundi yenye silaha na wa vyama vya upinzani SSOMA, vikiongozwa na Jenerali Thomas Cirillo, na wawakilishi wa serikali ya Kenya, akiwemo Jenerali Lazarus Sumbeiywo, mkuu wa “Tumaini Peace Initiative,” yaani “Mpango wa Tumaini la Amani ambapo ulikuwa ni mchakato wa mazungumzo ambayo yalifanyika Nairobi tangu Mei mwaka 2023. Katika mkutano huo, wa kwanza baada ya miezi kadhaa kati ya serikali ya Sudan Kusini na viongozi wa makundi ya upinzani, vyama hivyo vilieleza nia ya kuendelea kwenye njia ya mazungumzo kama suluhisho pekee la mzozo wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo kushughulikia misimamo tofauti kwa njia ya maelewano na mashauriano.

Ishara chanya kwa ajili ya wakati ujao

Sudan Tribune anaandika kuwa “Mkutano uliofanyika mjini Roma kwa kuhamasishwa  na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ni ishara ya maendeleo muhimu katika mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. Na ni onesho la ahadi mpya ya serikali na vikundi vya upinzani kutaka kufuata njia ya mazungumzo. Changamoto nyingi za wazi zimesalia lakini utayari wa pande zote mbili kukutana na kujadili ni ishara chanya kwa mustakabali wa nchi.”

Umoja wa Mataifa:hatua muhimu kuelekea amani

Jumuiya ya kimataifa imekaribisha kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya amani nchini Sudan Kusini. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo ya Kiafrika (Unmiss) uliuita mkutano huo hatua muhimu mbele na kuzitaka pande zote mbili kurejesha ahadi zao za kutafuta mazungumzo. Watu wa Nchi hii, waliozaliwa mwaka wa 2011, wamepata mateso makubwa, ardhi yenye rasilimali nyingi iliyomwagika na migogoro na vurugu.

Papa na Sudan Kusini

Papa alitembelea nchini Sudan Kusini kuanzia tarehe 3 hadi 5 Februari 2023.  Ziara ya Kitume ya Papa Francisko ilikuwa ni hatua zaidi katika safari iliyoanza mnamo mwaka 2019 wakati wa mafungo ya kiroho kwa mamlaka ya kiraia na kikanisa ya nchi hiyo ya Kiafrika. Mwishoni mwa mkutano huo Baba Mtakatifu anakumbukwa alivyo inama na kubusu miguu ya Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, na makamu wa rais waliokuwa wameteuliwa. Ilikuwa ni ishara ya kusisimua ya kuomba amani nchini Sudan Kusini. Lakini hata leo hii matumaini hayo ya upatanisho yamerejea kwa upya katika njia ya mazungumzo. Hiyo ni njia yenye nguvu zaidi ya kushinda mantiki ya nguvu, mashindano na vita, kwa sababu hadi sasa hawajatekeleza ahadi ya amani!

Mkutano kuhusu Sudan ulioandaliwa na Jumuiya ya Mt.Egidio,Roma
17 August 2024, 13:03