Sudan Kusini hali ya kulazimisha ndoa za utotoni kukithiri. Sudan Kusini hali ya kulazimisha ndoa za utotoni kukithiri.  (AFP or licensors)

Sudan Kusini:Gavana wa Jimbo la Umoja apiga marufuku ndoa za kulazimishwa!

Nimefahamisha jamii katika kaunti zote saba kuripoti visa vyovyote vya ndoa ya watoto au kulazimishwa kwa makao makuu ya serikali kwa uchunguzi ndani ya saa 24.Hiyo ni kauli ya Gavana wa Jimbo la Umoja,huko Sudan Kusini,Riek Biem,ambaye alisisitiza tena kwamba:"Inatosha ndoa za kulazimishwa za wanawake na wasichana."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hivi karibuni Gavana wa Jimbo la Umoja, huko Sudan Kusini alisema kuwa: “Mimi ni gavana wa jimbo hili na ninatangaza leo: tuwapeleke wavulana na wasichana wetu shuleni ili kufurahia manufaa ya elimu.  Hii ndiyo njia pekee tunaweza kuendeleza usawa wa kijinsia katika jimbo letu,” Biem alisema. “Nimefahamisha jamii katika kaunti zote saba kuripoti visa vyovyote vya ndoa ya watoto au kulazimishwa kwa makao makuu ya serikali kwa uchunguzi ndani ya saa 24,” aliongeza. Uamuzi wa gavana wa Jimbo la Umoja ulichukuliwa baada ya mauaji ya kikatili ya msichana wa miaka 20, aliyepigwa hadi kufa na baba yake kwa kukataa kuzingatia ndoa ya kulazimishwa iliyokubaliwa na familia.

Ndoa za kulazimishwa kwa wanawake na wasichana

Ndoa za kulazimishwa za wanawake na wasichana, hata wachanga sana, ni janga nchini Sudan Kusini. Takwimu za hivi karibuni zaidi za mwaka wa 2010 zinaonesha kuwa 52% ya wasichana nchini Sudan Kusini wameolewa kabla ya kutimiza miaka 18 na 9% huolewa kabla ya umri wa miaka 15. Familia nyingi huwalazimisha binti zao kuolewa ili kupata mahari, hata kama wako chini ya miaka 18. Uhaba wa chakula unaoathiri nchi umeongeza tatizo hilo.

Familia zinawauza binti zao

Familia kadhaa zinalazimika kuwauza binti zao ili kulisha washiriki wao wa familia kwa namna moja ni kama kufaya mtaji na kuuza watoto wao. Asilimia 6 pekee ya wasichana humaliza shule ya msingi, wakati 1 kati ya 5 huacha shule kwa sababu ya ujauzito. Kuzidisha hali ya wanawake ni ukweli kwamba unyanyasaji wa kijinsia hutumiwa dhidi ya wanawake na wasichana kama mbinu ya vita. Unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe hauripotiwi sana kutokana na unyanyapaa, hofu ya kulipiza kisasi na ukosefu wa mfumo wa haki wa kutosha.

Mkataba juu ya Haki za Mtoto 2015

Kusini mwa Sudan  ilijiunga na Mkataba wa Haki za Mtoto mwaka 2015, ambao unaweka umri wa chini wa kuolewa kuwa miaka 18. Pia ni mtia saini Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW), ambao unalazimu mataifa kuhakikisha kuwa huru na ridhaa kamili ya ndoa. Lakini hadi sasa matokeo hasi yanajionesha kuwa haufutwi mkataba huo.

 

21 August 2024, 17:29