2024.08.16 Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kombe la Zanzibar "Kusi 2024" Kimataifa Kitesurf Regatta. 2024.08.16 Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kombe la Zanzibar "Kusi 2024" Kimataifa Kitesurf Regatta.  (Organizzatore della Conferenza Stampa)

Tanzania:Toleo la II la mashindano ya Kombe la Zanzibar la kitesurfing Agosti,24!

Waandaaji wamewasilisha shindano la “Zanzibar CUP KUSI 2024” la kitesurfing linalotarajiwa kufanyika tarehe 24 Agosti 2024 likiwa ni tukio la II la kimichezo kuandaliwa nchini Tanzania ambalo kwa hakika linalenga“kukuza michezo ya kimataifa,lakini pia udugu na heshima miongoni mwa watu,”kama alivyofafanuliwa na mwandaaji Mkuu Dk.Stesano Conte.

Vatican News

Waandaaji wa mashindano yanayotarajiwa ya Zanzibar Cup waliliwasilisha tukio la mchezo wa kitesurfing katika mkutano na waandishi wa habari mjini Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 16 Agosti 2024. Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Baraza la Michezo la Taifa la Zanzibar alilitangaza tukio la pili la aina hiyo lililoitwa rasmi “Zanzibar CUP KUSI 2024” huku ‘Kusi’ likimaanisha jina la upepo wa msimu katika ukanda huo wa Tanzania na kufanya mchezo wa kitesurfing kufanikiwa.

Mkutano wa uwasilishaji wa Zanzibar Cup Kusi 2024
Mkutano wa uwasilishaji wa Zanzibar Cup Kusi 2024

Mashindano ya kitesurfing yamepangwa kufanyika Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024, hali ya hewa ikiruhusu, huko Kiwengwa katika mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar. Hii ni ishara ya Pili ya Kimataifa ya Kitesurfing Regatta, mchezo maarufu sana wa Zanzibar unaojulikana kwa asili yake wa kushangaza,  katika fukwe, na mandhari nzuri ya pwani hiyo. Kufikia sasa washiriki 33 wamesajiliwa, wakiwemo wachezaji wanne wa kitaalamu kutoka Austria, Italia, Afrika Kusini na Uingereza. Washiriki wengine waliowakilishwa wanatoka Poland, Jamhuri ya Czech, Hispania, na baadhi ni Watanzania.

Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kombe la >Zanziner la Kitesurf 2024
Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kombe la >Zanziner la Kitesurf 2024

Anayeratibu shindano hili la Pili la kimataifa ni daktari Stefano Conte, kutoka Italia, mkaazi wa Zanzibar na mpenda mchezo wa kitesurfing. Dk. Conte ni daktari wa upasuaji wa watoto ambaye amejitolea utaalamu wake kwa miaka mingi barani Afrika.

Mshindi wa Toleo la I la Kombe la Zanzibar la Kitesurf 2023 alikuwa mtanzania
Mshindi wa Toleo la I la Kombe la Zanzibar la Kitesurf 2023 alikuwa mtanzania

Pia alisaidia kuandaa michuano ya kwanza ya Kombe la Zanzibar iliyofanyika  mwezi Februari 2024, wakati katika mahojiano na Vatican News, alieleza kuwa “lengo ni kuunda mkutano wa watu katika ardhi ya Afrika, watu mbalimbali kutoka pande zote za  ulimwengu, wakiwa wameungana katika shauku yao ya mchezo mmoja. Tukio hili kwa njia mbalimbali linawakilisha ujumbe wa amani.”

Hii ni Picha ya mashindano yaliyopita Februari 2024
Hii ni Picha ya mashindano yaliyopita Februari 2024

Kwa njia hiyo Wadhamini wa shindano la mwezi Agosti ni pamoja na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar na baadhi ya hoteli na wafanyabiashara wa ndani ambao watasaidia kwa malazi na huduma kwa washiriki na wajumbe. Zanzibar, visiwani karibu na pwani ya Tanzania, pia inalenga kuongeza utalii wa michezo katika eneo hilo ili liwe aina ya kitovu cha michezo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Toloe la II la mashindano ya Kombe la Zanzibar la Kitesurf litafanyika 24 Agosti
20 August 2024, 16:58