Tafuta

"Zanzibar Cup 2024 Kaskazi"  kufanyika 24 Agosti 2024. "Zanzibar Cup 2024 Kaskazi" kufanyika 24 Agosti 2024. 

Tanzania,Zanzibar Cup2024 Kaskazi:Conte,kila kitu kiko tayari hata upepo!

Toleo la II la ‘Zanzibar Cup 2024 Kaskazi’ la Mashindano ya kitesurfing yanafanyika Kiwengwa Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024.Kwa mujibu wa daktari Stefano Conte,kutoka Italia,mkaazi wa Zanzibar na mpenda na mhamasishaji mkuu wa mchezo wa kitesurfing,akizungumza na Vatican News:"kila kitu kipo tayari."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Nchini Tanzania katika kisiwa cha Zanzibar Toleo la II liitwalo “Zanzibar Cup 2024 Kaskazi” lifanyanyika ambalo lina lengo la kuhamasisha, kupitia mashindano ya mchezo kitesurfing, heshima na mapatano kati ya watu. Mpango mzima wa mashindano ya Kimataifa ulioandaliwa na Baraza la “Kitaifa la Michezo Zanzibar (ZNSC), tarehe 24 Agosti 2024 huko Kiwengwa, lilikuwa limetoa tarifa ya awali kuhusiana na ratiba nzima.

Mkutano wa kuwasilisha mashindano ya Kombe la Zanzibar 2024 wa Kitesurf Kimataifa
Mkutano wa kuwasilisha mashindano ya Kombe la Zanzibar 2024 wa Kitesurf Kimataifa

Haoa tunachapisha taarifa iliyokuwa imetolewa awali kama ifuatayo:“Kufuatia mashindano ya kwanza ya kitesurfing yaliyofanikiwa Zanzibar (Tanzania) yanayoitwa ZANZIBAR CUP 2024 KASKAZI, yaliyofanyika mnamo tarehe 10-02-2024, tuliamua kuandaa mashindano ya pili ya kila mwaka ya mchezo wa kitesurfing yanayoitwa ZANZIBAR CUP 2024 KUSI yatakayofanyika Kiwengwa (Zanzibar) tarehe 24-08-2024. Jiunge nasi kwa mbio hizi za kushangaza za kusherehekea mbio za kasi zaidi za Bahari ya Hindi kwa roho ya amani na udugu kati ya watu wa ulimwengu!”

Washindi wa Toleo la Kwanza Zanzibar Cup Februari 2024
Washindi wa Toleo la Kwanza Zanzibar Cup Februari 2024

Vile vile walisisitiza kuwa “ Regatta ya kitesurf itakuwa IKA darasa TTR (Twin Tip Race). Mkutano utakuwa saa 4.00 asubuhi tarehe 24-08-2024 katika ufukwe wa Kiwengwa (eneo kamili tutawasiliana baadaye), wote wenye kitambulisho (kiters TZ) au Pasipoti (Non-TZ), kwa MUHTASARI na utoaji wa mbio za lycras na medali za ushiriki. Aidha walibainisha kuwa: “Wachezaji wote walio na umri wa chini ya miaka 18 wanapaswa kuja na mzazi mmoja au mtu mzima mwingine wakiwa na ujumbe kutoka kwa mzazi walio na kitambulisho cha mzazi.

Wakati wa michuano ya Kitesurf Feb 2024
Wakati wa michuano ya Kitesurf Feb 2024

Mchezo wa kinyang'anyiro, ikijumuisha joto na fainali yoyote, itaanza saa 8.00 Mchana. Tukio hilo litakamilika kwa hafla ya utoaji wa tuzo saa 11.00 jioni kwenye Hoteli ya Melia. Kila mshiriki atakimbia na gia yake. Ubao unapaswa kuwa “aina ya twintip na kite “aina ya pampu.” Ukubwa ni bure.

Wakati muhimu wa  kupongezana kwa ushindi wa  Feb 2024
Wakati muhimu wa kupongezana kwa ushindi wa Feb 2024

Regatta itafanyika kwenye kozi inayolingana na pembetatu ya Olimpiki inayoundwa na maboya (upepo wa kwanza, abeam ya pili na ya tatu ya chini) kurudiwa mara moja au mbili kulingana na nguvu ya upepo. Kuondoka kutafanyika baharini baada ya dakika 3 za kuzunguka. Ukiukaji wowote wa kipaumbele na sheria za usalama utasababisha kutohitimu mara moja na jaji wa mbio.” Kwa njia hiyo “Tunawahimiza wachezaji wa kigeni wanaotoka nje ya Tanzania kujipanga kukaa Zanzibar kwa angalau siku chache kuanzia siku iliyopangwa kwa ajili ya mbio hizo kutokana na uwezekano wa kuahirishwa kutokana na upepo kutotosheleza.”


Kwa mujibu wa daktari Stefano Conte, kutoka Italia, mkaazi wa Zanzibar na mpenda mchezo wa kitesurfing,  muhamaishaji mkuu ambaye ni daktari wa upasuaji wa watoto ambaye amejitolea utaalamu wake kwa miaka mingi barani Afrika, akizungumza na Vatican News Asubuhi ya Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024 amebainisha kuwa kila tayari na upeno upo hivyo mchezo utafanyika.

24 August 2024, 10:30