Waasi wa Myanmar watangaza kukamata kambi ya jeshi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuna ushindi kamili wa ngome kuu ya kimkakati ya jeshi la kaskazini-mashariki mwa Myanmar, kando ya njia muhimu ya kibiashara kuelekea nchini China. Haya yalitangazwa na kundi la Chama cha National Democratic Alliance Army (MNDAA), baada ya siku kadhaa za mapigano na jeshi la Naypyidaw. Hiki ndicho kituo cha Lashio, kaskazini mwa Jimbo la Shan, ambako mapigano makali yamekuwa yakiendelea kwa muda. Kulingana na kundi hilo lenye silaha, makamanda watatu wakuu wa jeshi, akiwemo jenerali meja, pia walikamatwa.
Kundi la Mndaa
Kwa sasa hakuna uthibitisho huru wa tangazo la waasi hao, ambalo lilikuja baada ya Juma lililopita kundi hilo hilo la Mndaa kudai kuhusika na kuuteka mji wa Lashio na katika miezi ya hivi karibuni ule wa Laukkai, karibu na mpaka na China, baada ya kujisalimisha na wakati huo huo ilitangazwa kuwa walikuwa karibu askari 2,000, waliokuwa madarakani tangu mapinduzi ya 2021. Hasa katika eneo la mwisho, takriban raia 14 waliuawa siku ya Jumamosi 3 Agosti 2024 katika mashambulizi ya anga yaliyolaumiwa kwa na Birmania, ambayo pia yalipiga hospitali. Kwa sasa hakuna tangazo lolote juu ya suala hilo kwa askari wa Naypyidaw, ambao wanaendelea na operesheni za kijeshi dhidi ya makabila yenye silaha ya nchi hiyo na harakati zinazoitwa ulinzi wa watu zilizoundwa baada ya mapinduzi.