Rais Tebboune wa Algeria katika ushindi tena. Rais Tebboune wa Algeria katika ushindi tena. 

Algeria:Tebboune athibitishwa tena kuwa rais

Kwa maombi ya kweli,Algeria ilimtunuku tena Rais Tebboune mamlaka ya pili ya kuongoza nchi hiyo. Twakwimu hasi kutoka kwa uchaguzi wa mapema wa Jumamosi iliyopita ni kutopiga kura kwani zaidi ya 50% ya wale walio na haki ya kupiga kura walijiondoa kwenye uchaguzi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Takriban 95% ya wapiga kura walitoa maoni yao kumuunga mkono Abdelmadjid Tebboune ambaye kwa hiyo anafanikiwa kuongoza tena Algeria. Kwa hiyo ni kura ambayo kwa kiasi kikubwa inathibitisha utabiri wa matumaini zaidi. Hakuna cha ushindi wa Abdelali Hassani, mgombea wa Kiislamu, ambaye wafshabiki wake wanashutumu udukuzi wa kura na mwanasoshalisti Youssef Aouchiche, ambaye kati yao alipata zaidi ya 5% tu ya kura.

Nusu ya Algeria haikupiga kura

Dosari pekee katika uchaguzi huo wa mapema, kwa mujibu wa waangalizi, ni kutokuwepo kwa kiasi kikubwa cha kwenda kufanya uchaguzi wa zaidi ya nusu ya Waalgeria, takwimu ambayo bado ni bora kuliko uchaguzi wa 2019, ambapo karibu 40% ya wale walio na haki ya kupiga kura walipiga kura.  Kuna wanaozungumzia kususia kupiga kura baada ya vuguvugu maarufu la Hirak, lililosaidia kuuangusha utawala wa rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika, na kutengwa.

Kuboresha muundo wa kijamii na kiuchumi

Rais Tebboune, anayeshutumiwa kwa kutumia sera ngumu na upinzani, sasa ataendelea kutekeleza mpango wa kuboresha hali ya uchumi ya nchi ya Algeria, ambayo hutoa gesi na hidrokaboni kwa nusu ya Ulaya, hata hivyo atakosa umaarufu wa uungwaji mkono unaotarajiwa na chama chake, “National Liberation Front), hasa kwa sababu ya msimamo mkali wa kutoshiriki.

09 September 2024, 16:32