Tafuta

Uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya Plastiki. Uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya Plastiki.  (AFP or licensors)

Marekani:Januari 2026,huko Califonia ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki!

Tangu Januari 2024,huko Califonia kumepigwa marufu kutumia mifuko ya Palastiki katika maduka makubwa na madogo.Mnamo 2014 matumizi ya mifuko hiyo,ilikuwa tayari imekatazwa hata hivyo wakiacha uwezekano wa kuwapatia wateja,kwa senti,mifuko ya plastiki inayostahimili uwezo wa kutumika tena.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Gavana Gavin Newsom alitia saini tarehe 24 Septemba 2024 ya sheria inayopiga marufuku kutumia mifuko ya Plastiki kuanzia Januari 2026, iwe katika maduka makubwa na maduka madogo. Saini hiyo inaneleza kwamba:"Acha kutumia mifuko ya plastiki California."

Jimbo la Marekani lilikuwa limepiga marufuku mifuko ya matumizi hayo mnamo mwaka 2014, hata hivyo ikiacha uwezekano wa kuwapatia wateja, kwa senti chache, mifuko ya plastiki inayostahimili uwezo wa kutumika tena. Walakini, kulingana na vyama vingine vya watumiaji, hii ilisababisha kuongezeka kwa tani za plastiki kwenye taka za California kwa asilimia  47% tangu 2014 hadi 2021.

Kutangazwa kwa sheria hiyo kulikuja siku ambayompango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa ulikaribisha “muunganisho"kwenye mkataba wa kwanza wa kimataifa wa kupunguza plastiki, unaotarajiwa kufikia mwisho wa 2024.

25 September 2024, 12:23