Nicaragua imwaachia wafungwa. Nicaragua imwaachia wafungwa.  (AFP or licensors)

Nicaragua yawaachilia huru wafungwa 135 wa kisiasa

Kufuatia shinikizo la kidiplomasia kutoka Marekani,Serikali ya Nicaragua imeachilia huru kundi la wafungwa wa kisiasa kwa misingi ya kibinadamu ambao wamehamishiwa Guatemala.Na Bunge la Nicaragua limeidhinisha sheria inayowaadhibu waandishi wa ujumbe kwenye mitandao ya kijamii,ambao,kulingana na mamlaka ya Managua,wanaeneza woga kati ya watu.

Osservatore Romano

Utawala wa Marekani umesimamia kuachiliwa kwa wafungwa 135 wa kisiasa waliozuiliwa Nicaragua kwa sababu za kibinadamu. Hayo yalitangazwa na Ikulu ya Marekani kufuatia upatanisho na serikali ya Rais Daniel Ortega.

Uhamisho hadi Guatemala

Kulingana na Ikulu ya Marekani kundi hilo tayari limehamishiwa nchini Guatemala, ambalo serikali yake "kwa ukarimu" ilikubali kuwakubali. Marekani iliongeza kusema kuwa "watu hawa watapewa fursa ya kutafuta njia za kisheria za kujenga upya maisha yao nchini Marekani au nchi nyingine." Walipowasili katika Jiji la Guatemala, watu hao 135 walikaribishwa na mamlaka mahalia na mashirika yanayowasaidia wahamiaji.

Shinikizo kwenye mitandao ya kijamii nchini Nicaragua

Bunge la Nicaragua limeidhinisha sheria inayowaadhibu waandishi waenye kutoa ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, ambao, kulingana na mamlaka ya Managua, wanaeneza "woga" kati ya watu. Adhabu za hadi miaka 5 jela zinatarajiwa. Upinzani ulioko uhamishoni umefafanua hatua hiyo kama "sheria ya gag", ambayo italenga kulenga maudhui ya kijamii yanayokosoa serikali ya Rais Daniel Ortega, hata wakati mtu anayeichapisha yuko nje ya nchi.

Sheria ya adhabu mtu awe ndani au nje ya nchi

Uamuzi wa Managua unakuja siku chache baada ya kuidhinishwa kwa sheria nyingine inayotoa adhabu kwa raia wa Nicaragua, nyumbani au nje ya mipaka ya kitaifa, kupatikana na hatia ya "uhalifu dhidi ya Serikali". Umoja wa Mataifa tayari ulikuwa umeelezea wasiwasi mkubwa katika suala hili. Upinzani ulioko uhamishoni umefafanua hatua hiyo kama "sheria ya gag", ambayo italenga kulenga maudhui ya kijamii yanayokosoa serikali ya Rais Daniel Ortega, hata wakati mtu anayeichapisha yuko nje ya nchi.

12 September 2024, 13:53