Rai Biden wa Marekani akizungumza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Rai Biden wa Marekani akizungumza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.  (ANSA)

Marekani inadai viongozi wa Venezuela kuheshimu matakwa ya watu

Katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,Rais wa Marekani Bwana Biden alizungumza kuhusu hali ya Taifa la Amerika Kusini la Venezuela kwamba " wapiga kura wanataka mabadiliko ambayo hayawezi kukataliwa."

Osservatore Romano

Wapiga kura wa Venezuela walionesha hamu katika uchaguzi ya kuwa na mabadiliko ambayo hayawezi kukataliwa. Hayo yalisemwa na Rais wa Marekani, Bwana Joe Biden, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN 79), mjini New York Marekani unaondelea. “Ulimwengu unajua ukweli," Bwana Biden alisema, akirejea uchaguzi wa mwezi Julai 28 nchini Venezuela, ambapo Baraza la Taifa la Uchaguzi liliidhinisha uthibitisho wa Nicolás Maduro madarakani bila hata hivyo kuchapisha matokeo kamili.

Hata Waziri Mkuu wa Italia, Bi Giorgia Meloni, akizungumza kutoka huko  New York, alialika Jumuiya ya Kimataifa kutosimama na kutazama tu: “Tuna wajibu wa kupaza sauti zetu.” Mgogoro wa Venezuela, ambapo upinzani unaendelea kupinga kuteuliwa tena kwa Maduro, ni kati ya vipaumbele vya makansela kadhaa wa kimataifa. Marais wa Colombia na Brazil, Gustavo Petro na Luiz Inacio Lula da Silva, wamepanga mkutano kufanyika  mjini New York ili "utafutie suluhisho la kisiasa" la mzozo wa kitaasisi nchini Venezuela.

"Tumeanzisha muungano kwa lengo la kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mgogoro unaozidi kuwa mgumu," alielezea rais wa Colombia, Petro. Hispania wakati huo huo iliomba kwamba hali ya Venezuela na mwitikio unaowezekana wa Umoja wa Ulaya ujumuishwe katika ajenda ya mkutano ujao wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika mjini Bruxelles tarehe 17 na 18 Oktoba 2024

26 September 2024, 11:11