Tafuta

2024.09.03 Mkutano Mkuu wa 15 wa Umoja wa Utangazaji wa Afrika(AUB) huko Goborone,3-6 Septemba 2024. 2024.09.03 Mkutano Mkuu wa 15 wa Umoja wa Utangazaji wa Afrika(AUB) huko Goborone,3-6 Septemba 2024. 

Mkutano Mkuu wa XV wa AUB kukabiliana na IA na mabadiliko ya Tabianchi

"Mustakabali wa vyombo vya habari vya Kiafrika vinavyokabili changamoto za teknolojia mpya na mabadiliko ya tabianchi,"ndiyo mada ya Mkutano Mkuu wa 15 wa Umoja wa Utangazaji Afrika(AUB),Gaborne,Botswana Septemba 3-6,2024.Mjadala wa kina kuhusu Akili Mnemba(IA)na jinsi gani watangazaji wa Afrika wanaweza kuimarisha ushirikiano katika mada zinazohusiana na Tabianchi.

Na Stanislas Kambashi, SJ –Gaborone.

Umoja wa Utangazaji barani Afrika(AUB), katika kuwasilisha Mkutano Mkuu wa XV uliofanyika huko jijini Gaborone nchini Botswana kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Mustakabali wa Vyombo vya Habari vya Afrika vinavyokabiliwa na changamoto za teknolojia mpya na mabadiliko ya tabianchi," ulisema kuwa: "Akili Mnemba inafafanua upya ni kwa jinsi gani tunavyounda, kuhariri na kusambaza maudhui yetu. Teknolojia hizi zinapowekwa kwenye maabara za utafiti, sasa ni ukweli unaoonekana na kujidhihirisha kama mshirika kamili anayejihusisha katika kazi kwenye viunga vyetu vya habari.”

Katika mkutano huo kwa hakika ulijadili kwa kina juu ya matumizi ya Akili Mnemba(AI)katika mustakabali wa tasnia ya utangazaji na jinsi gani watangazaji wa Kiafrika wanaweza kuimarisha ushirikiano juu ya mada zinazohusiana na hali ya Tabianchi.Mkutano Mkuu wa AUB kwa hiyo uliwaleta pamoja Watendaji Wakuu wa tasnia ya Vyombo vya Habari na Utangazaji, maafisa, wataalamu, wasomi, waundaji wa maudhui kutoka katika bara zima la Afrika na wawakilishi wa Mashirika ya Watawa na washirika wengineo.

Mkutano wa AUB huko Gaborone, Botswana
Mkutano wa AUB huko Gaborone, Botswana

Katika majadiliano,  washiriki hao waligusa  mada mbalimbali kama vile:  "Ustahimilivu wa vyombo vya habari vya Kiafrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Utetezi wa Vyombo vya habari kwa ushiriki wa raia katika hatua ya mabadiliko ya tabianchi, ufumbuzi wa Akili Mnemba(AI) kwa ajili ya kuboresha michakato ya uzalishaji wa maudhui, ufumbuzi wa AI katika ukusanyaji wa data kwa kipimo cha watazamaji na kuboresha kubadilishana maudhui katika habari na maendeleo ya programu."

Makamu rais wa Bostwana, mgeni rasmi wa ufunguzi

Ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa XV wa AUB ulifanyika siku ya Jumanne tarehe 3 Septemba na kuhitimishwa tarehe 6 Septemba 2024. Katika ufunguzi huo, Makamu Rais wa Botswana, Bwana Slumber Tsogwane, aliongoza hafla hiyo kama mgeni rasmi ambapo aliambatana pia na wajumbe wengine wa serikali na wabunge kadhaa. Katika hotuba yake, Makamu Rais alitoa wito wa kuwa waangalifu katika kukabiliana na fursa na changamoto zinazoletwa na ujio huo mpya wa Akili Mnemba(IA). Aliitaka AUB vile vile kujitahidi kuwa na uwakilishi halisi wa vyombo vya habari vya Kiafrika. “Teknolojia, lazima iwe katika huduma ya wanadamu kila wakati,” alisema. Makamu Rais pia alitoa wito wa matumizi mazuri ya majukwaa shirikishi ya vyombo vya habari ambayo yatawezesha AUB kueleza historia halisi ya Kiafrika, bila kuzuiwa na chuki zinazoenea katika bara hilo.

Rais wa AUB: "Afrika imekuwa ikibadilika kila wakati"

Kwa upande wake, Rais wa  Umoja wa Utangazaji wa Afrika (AUB) Cleophas Barore kutoka nchini Rwanda, alisisitiza  kuwa “teknolojia yoyote daima imekuwa ikizua hofu kwa binadamu. Afrika imekuwa ikibadilika kila wakati, na wakati huu, bara liko tayari kuzoea kama lilivyofanya siku zote.” Hata hivyo Mkutano huko ukiongozwa na Barore ulipitisha kwa kauli moja uundwaji wa Kituo cha Uchunguzi wa Kiafrika, mpango kabambe wa AUB unaolenga kusaidia vyombo vya habari vya bara hilo katika mageuzi yao ya kidijitali. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa AUB, Grégoire Ndjaka alisisitiza umuhimu wa mpango huo kama hatua madhubuti ya utekelezaji wa mapendekezo ya Mkutano wa AUB kuhusu Akili Mnemba  na Vyombo vya Habari, uliofanyika mnamo Machi 2024 kwa ushirikiano na UNESCO.

Kwa maelezo zaidi: baada ya mkutano wa AUB na UNESCO Machi 2024

Baada ya mkutano kati ya Umoja wa Utangazaji wa Afrika (AUB) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO),kuhusu: Akili Mnemba(IA) na Vyombo vya Habari, "uliofanyika huko Yaoundé nchini Cameroon, mnamo Machi 2024, Umoja huo ulilenga kwa hiyo katika Mkutano unaofuata, kuchambua jinsi ambavyo Akili Mnemba(IA) inaweza kubadilisha uundaji na usambazaji wa maudhui ya utangazaji barani Afrika na pia kujadili mchango wa utangazaji wa Kiafrika kwa mipango ya kimataifa ya kupambana na  mabadiliko ya tabianchi. Kwa njia hiyo mijadala ya Mkutano huo ilizingatia: mchango wa Akili Mnemba katika mabadiliko ya utangazaji wa Kiafrika na uundaji wa maudhui ya AI, uchunguzi wa teknolojia za AI kwa ajili ya uzalishaji wa maudhui ya awali na ya kuvutia ya utangazaji, na vile vile  kupunguza gharama, Suluhishi za AI za uboreshaji wa michakato ya uzalishaji, mchango wa mtakwimu, jukumu la Afrika katika uzalishaji na usimamizi wa metatakwimu kwa maudhui ya sauti na taswira na mabadiliko ya fani katika sekta ya utangazaji kutokana na athari za Akili mnemba (AI) juu ya ujuzi na fani katika taswira ya sauti.  kwa njia hiyo  Sekta hiyo ilitoa muktadha thabiti zaidi kwa taarifa ya jumla iliyopokelewa huko Yaoundé.

Wajumbe mwishoni mwa Mkutano Mkuu huo walipaswa kuwa na vifaa bora zaidi vya kufanya maamuzi muhimu zaidi juu ya masuala yote yanayohusiana na akili mnemba kwenye vyombo vyao vya habari. Uwasilishaji maalum juu ya mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi,  lazima uzingatia jukumu la tasnia ya sauti na kuona katika kuongeza uelewa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuchukua tathmini ya mradi wa AUB-UNDRR ambao katika miaka minne umewezesha kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya mabadiliko ya tabianchi na kupunguza hatari ya maafa yake.

Wakati wa Mkuano wa AUB huko Gaborone, Botswana
Wakati wa Mkuano wa AUB huko Gaborone, Botswana

Katika mkutano huo, aidha AUB pia walijikita katika suala la ubadilishanaji wa maudhui, ambao ni shughuli yake kuu. Majadiliano yalizingatia njia bora zaidi ya kukuza ushiriki wa nchi, na  sio tu katika kushiriki maudhui kwenye jukwaa la AUBvision,(yaa kusikiliza na kuona),lakini pia kuifanya kuwa chanzo kikuu cha usambazaji, kutokana na njia chache za wanachama. Matokeo yaliyotarajiwa katika mkutano huo ni pamoja na mapendekezo ya vitendo na mikakati ya kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo katika sekta hiyo.

MKUTANO WA AUB HUKO GABORONE 3-6 SEPTEMBA 2024
11 September 2024, 12:24