Watu 558 wamekufa nchini Lebanon na kamanda wa Hezbollahk kusini mwa Beirut
Vatican News
Kuna wahanga 558 nchini Lebanon baada ya wimbi la tatu la uvamizi wa Israel dhidi ya Hezbollah nchini humo. Kulingana na Wizara ya Afya ya Beirut inabainisha kuwa watoto 50 waliuawa. Wafanyakazi wawili wa UNHCR pia walifariki, kama ilivyoripotiwa na Kamishna Mkuu wa Shirika hilo Bwana Filippo Grandi. Mabomu elfu mbili yalirushwa dhidi ya shabaha takriban 1,500 zilizohusishwa na wanamgambo wa Kishia. Shambulio lililolengwa dhidi ya Abu Jawad Harikhi, Kamanda wa mfumo wa makombora ya Hezbollah, lililozinduliwa katika kitongoji cha kusini mwa mji mkuu. Harikhi aliuawa wakati wa uvamizi huo pamoja na watu wengine watano na kumi na watano kujeruhiwa.
Mashambulizi ya roketi dhidi ya Israeli
Wakati huo huo, kutoka Lebanon, karibu watu 500 wamevuka mpaka kutafuta hifadhi nchini Siria. Mashambulizi ya roketi pia yanaendelea kuelekea Israel. Na zaidi ya 65 ilizinduliwa kutoka kusini mwa Nchi ya Mwerezi. Takriban roketi kumi zililenga maeneo ya mashariki mwa Haifa na zilinaswa na ulinzi wa anga, huku nyingine zikirushwa kwenye maeneo ya wazi huko Galilaya na mwanamke mwenye umri wa miaka 58 alijeruhiwa.
Guterres: Lebanon haipaswi kuwa Gaza nyingine
"Watu wa Lebanon, watu wa Israel na watu wa dunia hawawezi kuruhusu Lebanon kuwa Gaza nyingine", alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres, katika hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. "Jumuiya ya kimataifa, lazima ihamasishe kwa usitishaji mapigano mara moja, kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote na kuanza kwa mchakato usioweza kutenguliwa kuelekea suluhisho la serikali mbili," alisisitiza Bwana Guterres.