Xanana Gusmao, Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki. Xanana Gusmao, Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki. 

Xanana,Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki:upatanisho na Indonesia ni mfano wa kuigwa!

Gusmao,kiongozi wa zamani wa Harakati ya upinzani,ambaye ni Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki akihojiana na Shirika la habari za Kimisionari Fides,ametoa mtazamo wa Nchi kuanzia mchakato wa maridhiano na Indonesia hadi ndoto:"kuona watu wote wa Timor wana maisha mazuri kuanzia,mijini,vijijini na milimani.Zaidi ya ndoto ni misheni tunayojitolea kwa nguvu zote.”

Na Paolo Affatato na Angella Rwezaula – Vatican.

Timor ya Mashariki imechagua njia ya upatanisho na Indonesia, ili kuponya majeraha ya siku za nyuma. Na sasa mchakato huo wa upatanisho unaweza kuwa, kwa njia yake ndogo, mfano kwa heshima na mazingira ya migogoro katika eneo la sasa la kimataifa, ikiwa ni pamoja na Ulaya na Mashariki ya Kati".  Hili ndilo pendekezo linalopendekezwa na  Xanana Gusmao, kiongozi wa zamani wa Harakati ya  upinzani, ambaye sasa ni  Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki, akihojiana na Shirika la habari za Kimisionari Fides, ambapo alielezea matumaini ya pamoja na wenzake kuhusu ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko katika nchi changa zaidi duniani, lakini yenye zaidi ya 95% ya  wakazi Wakatoliki. Yafuatayo ni mahojiano hayo.

Xanana Gusmao,Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki akishiriki Misa Takatifu
Xanana Gusmao,Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki akishiriki Misa Takatifu

Waziri Mkuu Gusmao,ziara ya Papa Francisko ina maana gani kwa Timor ya Mashariki?

Uwepo wa Papa hunaleta hisia kali. Ni hatua ya kihistoria kwetu, nchi ndogo ya Kikatoliki hadi sasa na mbali na Vatican. Tunakumbuka ziara ya Papa Yohane Paulo  II, miaka 35 iliyopita, wakati suala la uhuru wetu lilipohitaji kuzingatiwa na jumuiya ya kimataifa. Kufika kwa Papa na maombi yalikuwa baraka kwetu. Kabla ya uvamizi wa Indonesia (mnamo mwaka 1975), nchini asilimia  30% ya watu waliobatizwa walikuwa Wakatoliki katika Timor ya Mashariki, sambamba na vurugu na mauaji, dini pia zilitumiwa na udhalimu na wakati mwingine walitaka kulazimisha watu wajiite wenyewe Waislamu. Kinyume chake, watu walijaa makanisani, ubatizo ulianza kuongezeka. Kulikuwa na uhusiano kati ya upande wa kidini na harakati zetu za kupigania uhuru. Kisha wakati wa kutisha wa mauaji ya Santa Cruz (mnamo mwaka wa 1991, na kuendelea) ulikuwa ishara muhimu na hata nchi za Magharibi zilianza kutilia maanani mapambano yetu ya kujitawala. Papa "alikuja kwa wakati ufaao", ziara yake ilikuwa ya majaliwa, vizazi vya zamani bado vinasema leo. Na tunaamini, basi, kwamba leo hii pia ni "wakati sahihi" wa kumkaribisha Papa Francisko.

Je, mchakato wa amani na upatanisho na Indonesia unaendeleaje?

Timor ya Mashariki ilitaka sana upatanisho baada ya majeraha ya zamani. Katika hili, Timor ya Mashariki inaweza kuwa, kwa njia yake ndogo, mfano kwa heshima na mazingira ya migogoro katika eneo la sasa la kimataifa, ikiwa ni pamoja na Ulaya na Mashariki ya Kati. Hapa tumepata njia ya kufuata mchakato wa upatanisho wa kweli. Pamoja na nchi nyingine katika hali tete, kumekuwa na ubadilishanaji mzuri wa uzoefu katika suala hili. Hata hivyo, nilipokuwa Uswiss kwa ajili ya mkutano wa amani kwa Ukraine, Urusi haikuwepo. Lakini amani inafanywa na maadui, ni muhimu kukutana kwenye meza za mazungumzo, na Jumuiya ya Kimataifa ina jukumu la kuwahamasisha.

Tulifanya hivyo na Indonesia. Hii haimaanishi kusahau mateso na ukatili wa wakati uliopita. Tunayo Makumbusho ya Upinzani ambayo hukusanya ushahidi wote wa matukio hayo maumivu na kuhifadhi kumbukumbu zao kwa vizazi vijavyo. Hatutaki na hatuwezi kufuta historia. Tume ya Ukweli na Maridhiano pia iliitaka Indonesia kutambua mauaji yaliyofanywa. Na pia tulikumbuka vipindi vya heshima, ambapo jeshi la Indonesia lilikataa kufanya vurugu kwa raia wasio na ulinzi, licha ya maagizo yaliyopokelewa. Lakini tunakumbuka siku za nyuma ili kujenga mustakabali tofauti, unaofanywa kwa heshima na amani. Hatutaki kuweka lawama kwa watu wa Indonesia wa leo hii. Nilikwenda Indonesia baada ya kuanguka kwa utawala wa Suharto, ambao uliamua juu ya uvamizi wa Timor ya Mashariki pia imebadilika. Iliwezekana kuanzisha mchakato wa upatanisho na uhusiano mzuri wa kisiasa. Watu wa Timor na watu wa Indonesia walishiriki mbinu hii. Tulitafuta amani na bado tunajaribu kujenga upya mustakabali mzuri, hasa tukifikiria vizazi vipya.

Kuna uhusiano gani kati ya Serikali na Kanisa katika Timor ya Mashariki?

Katiba yetu ni ya kiulimwengu, sisi ni nchi ya kiulimwengu na ya kidemokrasia ambayo inalipatia heshima Kanisa Katoliki na inatambua mchango wake wa thamani pia kwa uwazi katika Mkataba. Tuna uhusiano maalum na Kanisa Katoliki, tumetia saini Mkataba. Serikali inatoa mchango wa kila mwaka kwa Kanisa, ambao hubadilika kila mwaka, na hujumuishwa na serikali katika bajeti ya Serikali: msaada ambao hutumiwa na taasisi za Kikatoliki kwa huduma za kijamii zinazotolewa kwa watu.

Timor ya Mashariki ina idadi kubwa ya vijana. Je,takwimu  hii inashawishi vipi sera ya serikali?

Timor ya Mashariki ni taifa changa, lina umri wa miaka ishirini na mbili hivi  tu na tunaweza kusema kwamba linaundwa na idadi kubwa ya vijana. Serikali inaitwa kukuza mustakabali wao. Hebu tufikirie kuhusu uwekezaji ili kuboresha ubora wa elimu. Pili, ni lazima tusukume maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ni maendeleo ya kiuchumi pekee ndiyo yanayoweza kuhakikisha ajira nyingi kwa watu wetu, na kukatisha tamaa ya uhamiaji wa vijana. Sasa tuko kwenye mchakato huo. Sisi bado ni nchi ya kilimo, inayoundwa na familia nyingi za wakulima, lakini sasa wanapeleka watoto wao shuleni. Tunajaribu kubadili fikra za watu, kwa mfano kwa kuboresha kilimo kwa kutumia teknolojia mpya na kuhimiza sekta binafsi. Kuna haja ya mabadiliko ya kiutamaduni, ambayo yanakuza mawazo ya ujasiriamali. Kwa sababu hii tumekuza programu ya maendeleo iliyogawanywa katika miradi midogo midogo karibu mia tisa, iliyosambazwa nchini kote, tukijaribu kuwashirikisha watu, hasa vijana, wanaoanzisha biashara ndogo ndogo. Na tumeridhika na matokeo. Miradi midogo iliyoenea hutumika kuunda motisha na mfano. Biashara ndogo inaweza kusaidia familia nzima au familia kadhaa. Tunanuia kuunda benki ya maendeleo ili kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati, benki inayowezesha mikopo midogo midogo.

Rais na Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki kwa picha ya Pamoja na Papa
Rais na Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki kwa picha ya Pamoja na Papa

Je, Timor ya  Mashariki inafaaje katika eneo la kimataifa? Je, mahusiano na mataifa jirani kama vile Indonesia, Australia, China yanavutiwa vipi na mafuta ya Timor ya Mashariki?

Kama taifa changa na dogo, tulitaka kuungana na kujilinganisha na nchi zingine dhaifu, kwa sababu ya hali ya kijamii na kisiasa: hivi ndivyo mpango wa kikundi cha "G7+" ulivyozaliwa, shirika la kiserikali linaloleta pamoja nchi ambazo zinakabiliwa mzozo unaoendelea au ambao hivi karibuni umepata migogoro na udhaifu. Ina nchi wanachama 20 kutoka Afrika, Asia-Pasifiki, Mashariki ya Kati na Carribiean. Kubadilishana uzoefu mzuri na nchi hizi kumekuwa na ni muhimu sana. Kwa ajili ya unyonyaji wa mafuta, tuko katika mazungumzo na makampuni ya Australia na Kichina, waaminifu kwa kanuni moja: baada ya uchimbaji, bomba lazima lifikie Timor ya Mashariki. Ni lazima tufanye kila kitu ili kuunda kazi, na kazi zilizohitimu, kwa watu wetu. Tunanuia kuepuka kuhusisha na kutegemea makampuni makubwa kutoka ng'ambo pekee: lengo letu ni kutoa athari za kijamii na athari ya kiuchumi nyumbani. Tunafuata kanuni hii na haki hii katika vikao vyote vya kimataifa, yaani, haki ya kuleta bomba kwenye pwani yetu.

Papa huko Timor ya Mashariki

Je Xanana Gusmao,anaota nini kwa ajili ya  mustakabali wa Timor Mashariki?

Nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kuwa huru na uhuru. Ndoto hiyo ilitimia. Ilikuwa ndoto ya watu wote. Ilikuwa ni safari yenye matokeo ya ajabu. Sasa lengo ni kuona taifa linakua na kuwa na hali nzuri ya maisha. Watu waliteseka hata baada ya uhuru. Ilibidi tulijenge taifa upya kuanzia mwanzo, tukianza na miundombinu ya msingi. Sasa inabidi tuendelee na kujenga shule na hospitali vijijini. Ndoto ya leo hii ni kwamba si kuona watu wachache tu wana maisha ya heshima, lakini raia wote wa Timor wanayo maisha mazuri kuanzia, mijini, vijijini, hadi pembeni na milimani. Lakini, zaidi ya ndoto, ni misheni ambayo leo hii tunajitolea kwa nguvu zetu zote.

Mahojiano kati ya Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki: Xanana.
10 September 2024, 12:31