Mkutano kuhusu Tabianchi COP29 huko Baku Mkutano kuhusu Tabianchi COP29 huko Baku 

COP29,UNESCO:Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri mzunguko muhimu wa maji ya sayari

Kabla ya kuanza COP29,Vatican News ilizungumza na mtaalam wa maji wa UNESCO,Profesa Mariele Evers wa Chuo Kikuu cha Bonn,kuhusu jinsi gani mabadiliko ya tabianchi yanavyobadilisha mifumo ya maji katika sayari na kusababisha mafuriko ya mara kwa mara na makubwa au ukame unaoathiri maisha ya mamilioni ya watu.

Vatican News

Mkutano wa 29 wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi (COP29) ulianza mjini Baku, nchini  Azerbaijan, Jumatatu tarehe 11 na utahitimishwa tarehe 22 Novemba 2024 kwa kuwaleta wajumbe kutoka karibu nchi 200 duniani kote ambao watajadili njia za kupunguza ongezeko la joto duniani kwa muda mrefu hadi 1.5C iliyowekwa na Mkataba wa Paris mnamo  mwaka 2015 na kujiandaa kwa mabadiliko ya tabianchi ya  siku zijazo. Lengo kuu la mazungumzo hayo yatakuwa juu ya fedha za hali yatabianchi, pia msingi wa hatua za hali ya tabianchi duniani kote. Mojawapo ya athari zinazoonekana zaidi za ongezeko la joto duniani ni mabadiliko makubwa katika mifumo ya maji duniani kote. Kadiri halijoto ya kimataifa inavyoongezeka, kupungua kwa theruji nmaeneo ya milimani huzidi u kuwa tete. Ugavi wa maji unabadilika zaidi na kuna tishio lililoongezeka kutokana na mafuriko na majanga ya asili, kama inavyooneshwa na matukio ya hali ya tabianchi ya  mwaka huu 2024  ambayo yamekumba  sehemu kadhaa duniani, ikiwa ni pamoja na Valencia majuma mawili yaliyopita, Indonesia na nchi nyingine nyingine.

Hakuna maisha bila maji

Suala hili muhimu lilikuwa lengo la mazungumzo ya kimataifa yenye kichwa "Hakuna Maisha bila Maji" yaliyoandaliwa jijini Roma na Ubalozi wa Ujerumani anayewakilisha Nchi yake mjini Vatican kabla ya Mkutano huo wa COP29. Katika fursa hiyo Vatican News ilizungumza na mmoja wa washiriki, mwanajiografia Profesa Mariele Evers, Mwenyekiti wa UNESCO katika mifumo ya maji ya binadamu ambaye ni mtaalamu wa ‘eco-hydrology’ na usimamizi wa rasilimali  maji.

Mabadiliko ya tabianchi  yanazidisha ukame na mafuriko

Katika mahojiano hayo alisisitiza  udharura wa kuchukua hatua za kijasiri kukabiliana na mzozo wa hali ya tabianchi ambao, alieleza, unazidisha ukame na mafuriko katika maeneo makubwa na yenye watu wengi duniani, ikiwa ni pamoja na India na China, na kuathiri maisha ya mamilioni ya watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na  kilimo. Profesa Evers pia alitaja tatizo la unyonyaji, usimamizi mbaya na uchafuzi wa rasilimali muhimu za maji, kutokana na uchimbaji madini na shughuli nyingine za kibinadamu. Ikiwa matatizo haya yatashughulikiwa, alisema "hakutakuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kizazi kijacho," hivyo kuongeza njaa, uhamiaji na matatizo mengine.

Maji ni kipitishio cha mabadiliko ya tabianchi lakini pia kipunguzaji muhimu

Profesa Evers alisisitiza zaidi umuhimu wa maji katika kukabiliana na tabianchi: "Maji ni kisambazaji cha mabadiliko ya tabianchi, lakini pia ni muhimu kwa mazingira yenye afya kama vile misitu na ardhi oevu ambayo inaweza kuhifadhi kaboni  nyingi. "Tunahitaji mifumo ikolojia yenye afya ili kudumisha utendaji kazi huu ili iweze kufanya kazi kama shimo la kaboni na isiwe chanzo cha kutolewa kwa kaboni," alisema.

Unesco na Unicef katika mkutano wa Tabia nchi huko Baku
12 November 2024, 12:03