COP29:UNICEF Takriban watoto bilioni 1 wako hatarini kutokana na mabadiliko ya tabianchi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP29, Jumatatu tarehe 11 Novemba 2024 huko Baku nchini Azerbaijan, takwimu za UNICEF zilizoonesha kuhusu mzozo wa hali ya tabianchi ni wa kushangaza: karibu watoto bilioni 1 - karibu nusu ya watoto bilioni 2.2 duniani - wanaishi katika nchi 1 kati ya 33 zilizoainishwa kama "hatari kubwa" kutokana na mabadiliko ya tabianchi; zaidi ya watoto 420,000 kwa sasa wameathiriwa na ukame uliorekodiwa katika eneo la Amazonia; Mtoto 1 kati ya 5 - au milioni 466 -anaishi katika maeneo ambayo yanapata angalau mara mbili ya idadi ya siku za joto kali kila mwaka ikilinganishwa na miaka sitini tu iliyopita; joto kali husababisha ongezeko la watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na wanaozaliwa wakiwa wamekufa, huku uwezekano ukiongezeka kwa 5% kwa kila ongezeko la 1°C la joto; uchafuzi wa hewa sasa ni sababu ya pili ya hatari ya kifo duniani kote kwa watoto chini ya umri wa miaka 5, baada ya utapiamlo. Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa nchini Bangladesh, katika miaka ambayo majira ya joto huchukua zaidi ya siku 30, hatari ya ndoa za utotoni huongezeka maradufu kwa wasichana wenye umri wa miaka 11-14 ikilinganishwa na miaka ambayo hakuna majira ya joto.
Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuharibu sayari
Kwa njia hiyo katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 29) uliofunguliwa na ambao utahitimisha tarehe 22 Novemba 2024 huko Baku, Azerbaijan unaudhuriwa na Wanachama wa Mkataba wa Paris huku majanga ya hali ya tabianchi yakiendelea kuharibu maisha na ustawi wa watoto ulimwenguni kote. Hivi sasa Ulimwenguni kote, majanga ya hali ya tabianchi yanaathiri afya na maendeleo ya watoto, usalama wao na upatikanaji wao wa huduma muhimu. Ulimwengu haufanyi vya kutosha kulinda watoto. Kwa njia hiyo UNICEF itafanya kazi katika mkutano huo wa COP29 ili kuhakikisha kwamba mahitaji, haki na mitazamo ya watoto inajumuishwa katika sera za hali ya tabianchi, vitendo na uwekezaji katika ngazi zote.
Watoto wamepitia mwaka wa joto kali
Bi Catherine Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF alisema:"Watoto wamepitia mwaka mwingine wa rekodi ya joto kali, mafuriko mabaya, ukame na vimbunga vya kutishia maisha. Hawana jukumu la kutosha kwa majanga haya, lakini wanabeba mzigo wao.” Kwa njia hiyo “Katika COP29 na kupitia Michango Iliyoamuliwa Kitaifa, Serikali lazima zipe kipaumbele cha haki za watoto. Watoto lazima wajumuishwe katika suluhisho, na viongozi wa kimataifa lazima wafanye huduma za afya, elimu, maji na usafi wa mazingira, mifumo ambayo watoto wanategemea - kustahimili zaidi athari za mabadiliko ya tabianchi,” alisisitiza Bi Rusell”. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua."
Maoni kutoka Kamati 26 za Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto
Wanachama katika Mkataba wa Paris walikubaliana kwamba wakati wa kuchukua hatua za hali ya tabianchi, na lazima waheshimu, wakuze na kuzingatia haki za watoto na usawa wa vizazi. Hata maoni ya Jumla ya 26 ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto pia yanasema kuwa Nchi Wanachama lazima zichukue hatua ili kuunga mkono haki ya watoto ya mazingira safi, yenye afya na endelevu. Ingawa baadhi ya maendeleo yalifanywa kwa watoto katika COP28 - ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Urais Bingwa wa Vijana wa Hali ya ya Tabianchi na makubaliano ya kufanya mazungumzo ya kitaalam kuhusu watoto na mabadiliko ya tabianchi katika Mkutano wa Hali ya tabianchi wa (SB60) huko Bonn nchini Ujerumano mnamo Juni 2024 -lakini hakuna chochote ambacho kimeleta juhudi kubwa au uwekezaji kwa sera ya hali ya tabichi inayozingatia watoto.