Watu wakisubiri matokeo ya uchuguzi Marekani. Watu wakisubiri matokeo ya uchuguzi Marekani.  (AFP or licensors)

Mtazamo wa Ulimwengu wetu

Huko Marekani matokeo ya kwanza baada ya siku ya uchaguzi:Donald Trump yuko mbele wakati Bi Haris nafasi zinapungua japokuwa bado kuwa na uhakika.tarehe 5 Novemba huko Lebanon watu 15 walikufa.Ukraine:mji wa Zaporijgia ulipigwa tarehe 5 Novemba na watu 6 walikufa wakati watu 23 kujeruhiwa.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Kwa mtazamo wa kinachoendelea Ulimwenguni tunaweza kuona mengi tu kwa kudadavua lakini kwa ufupi tuanzie na sehemu zile ambazo vyombo vya habari vinamulika zaidi: Marekani: matokeo  ya kwanza baada ya "siku ya uchaguzi": Donald Trump yuko mbele, na ameshinda katika majimbo 2 ya (Georgia na Caroline Kaskazini), ushindi mwekundu pia huko Pennsylvania. Warepublican wanachukua viti vingi katika Seneti. Ni matokeo ambayo hayana uhakika lakini nafasi za Kamala Haris zimepunguzwa. Wakati  Israel: Netanyahu amfuta kazi Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant na kumweka Israel Katz, baada ya kutofautiana kuhusu vita huko Gaza. Giedon Saar, mpinzani wa zamani wa waziri mkuu, anachukua nafasi ya Mambo ya Nje.

mabomu  huko Lebanon
mabomu huko Lebanon

Lebanon: Watu 15 walikufa tarehe 5 Novemba 2024  katika shambulio la Israeli kwenye jengo la makazi huko Barja kusini mwa Beirut na - Urusi: Baraza la Shirikisho (Jumba la Juu) linapiga kura tarehe 6 Novemba 2024  kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kimkakati na Korea Kaskazini. Kwa upande wa  Ukraine: mji wa Zaporijgia ulipigwa tarehe 5 Novemba  na watu 6 walikufa wakati watu 23 kujeruhiwa. Kwa mtazamo wa Congo- DRC: Wanajeshi wanne walihukumiwa kifo kwa kupora parokia moja. Na - Italia: Rais Mattarella akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Antonio Tajani wanazuru nchini China hadi tarehe 12 Novemba 2024.

06 November 2024, 17:19