Biden abadili hukumu za kifo kwa wafungwa 37 hadi kifungo cha maisha.Hivi karibuni wito wa Papa!
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Ombi la Papa lilijibiwa. Wanaume na wanawake 37 waliokuwa katika hukumu ya kifo nchini Marekani watabadilishiwa hukumu zao kutoka katika kunyongwa hadi kifungo cha maisha. Hayo yalitangazwa na rais anayemaliza muda wake huko Marekani, Bwana Joe Biden, tarehe 23 Desemba 2024 katika, mkesha wa Noeli na kufunguliwa kwa Jubilei, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosema kuwa watu hao wataona vifungo vyao vikiwekwa upya kuwa vifungo vya maisha bila uwezekano wa kuachiliwa huru.
Habari ya Ikulu
Ujumbe huo huo kutoka Ikulu ya (White House), ulisisitiza kwamba Biden "anaamini kwamba Marekani lazima iache matumizi ya adhabu ya kifo katika ngazi ya shirikisho, isipokuwa katika kesi za ugaidi na mauaji ya watu wengi yanayochochewa na chuki", kwamba "hatua hii ya kihistoria ya huruma kwa Rais inaendelea kuwa rekodi ya mageuzi ya haki ya jinai.” Mapema mwezi huu Desemba, Rais Biden alikuwa tayari ametangaza ubadilishaji wa hukumu kwa takriban Wamarekani 1,500 ambao "walionesha ukarabati uliofanikiwa na kujitolea kufanya jamii kuwa salama." Hawa ni pamoja na msamaha wa watu 39 waliopatikana na hatia ya uhalifu usio na vurugu.
Ombi la Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana
Uamuzi wa kiongozi huyo wa kidemokrasia, ambaye siku chache kabla ya kumalizika mamlaka yake, unakuja baada ya wito wa dhati wa Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika Bwana katika Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili tarehe 8 Desemba 2024 alipokuwa akiwahutubia waamini wote waliokuwepo kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro na kuunganishwa katika utiririshaji, ambapo aliomba "kuwaombea wafungwa nchini Marekani ambao wako kwenye njia ya kifo.Papa aliongeza kusema kuwa: "Tuombe ili hukumu yao ibadilishwe na kubatilishwa. Hebu tuwafikirie hawa kaka na dada zetu na tumwombe Bwana kwa neema ya kuwaokoa na kifo."
Jitihada ya maaskofu na vyama
Maneno ya Papa Fransisko ambaye daima amekuwa akisisitiza kutokubalika kwa hukumu ya kifo, hata kurekebisha Katekisimu ya Kanisa Katoliki juu ya suala hilo, mara moja yalikusanywa na kuzinduliwa tena na Baraza la Maaskofu Katoliki la Marekani(USCCB,) ambalo liliwaomba waamini wote nchini Marekani kuungana na kumwomba Rais Biden abadilishe hukumu za kifo kwa wale wanaohukumiwa kifo katika magereza ya shirikisho hadi kifungo cha maisha. Kabla ya Maaskofu, Mtandao wa Uhamasishaji wa Kikatoliki (Cmn), shirika la Kikatoliki la kitaifa linalopambania kukomeshwa kwa adhabu ya kifo nchini Marekani, lilikuwa limeanza kampeni ya kubatilisha hukumu za watu 40. Mkurugenzi mtendaji, Krisanne Vaillancourt Murphy alisisitiza kwamba kwa Rais Biden ilikuwa fursa pekee na ya mwisho kwa Biden kukumbatia mafundisho ya Kikatoliki na kuokoa maisha ya watu hao. Mwangwi wa dhamira ya chama hicho ulimfikia Papa ambaye alizindua upya katika ngazi ya kimataifa.
Papa na Biden katika simu
Hatimaye, bila kusahau simu iliyopigwa siku zilizopita kati ya Papa Francisko na Joe Biden, ambaye miongoni mwa mada mbalimbali zilizozungumzwa katika mazungumzo hayo, alimshukuru Papa kwa "kazi yake ya kukuza haki za binadamu."