Mwanamke wa Kipalestina aliyefukuzwa makazi,anatumia maji nje ya makazi yake,huko Khan Younis. Mwanamke wa Kipalestina aliyefukuzwa makazi,anatumia maji nje ya makazi yake,huko Khan Younis. 

Idadi ya vifo huko Gaza inazidi 45,000 huku njaa ikitanda kaskazini

Mkuu wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa,UNICEF,anaripoti kuwa zaidi ya watoto 14,500 wameripotiwa kuuawa huko Gaza,huku idadi ya vifo ikipita 45,000 kulingana na mamlaka ya Gaza.Mashirika ya kibinadamu yanaendelea kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ili kuwahudumia wathiriwa na kusambaza msaada wa chakula unaohitajika sana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limeripoti kuwa usiku wa kuamkia tarehe 16 Disemba 2024, watu 13 walikufa na 48 walijeruhiwa wakati wa shambulio la anga ambalo hakuwa na onyo. Idadi ya watoto walikuwa miongoni mwa waathirika. Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamelaani mashambulio mabaya ya hivi karibuni ya anga katika Ukanda wa Gaza unaokumbwa na vita, ikiwa ni pamoja na katika shule iliyogeuzwa makazi ya Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa unaripoti kwamba baadhi ya waathrika walikuwa wamehamishwa kwa nguvu mara saba au nane, na kuishia katika shule hii ya UNRWA ambayo ilishambuliwa kwa bomu, na kuongeza kuwa hali "inahisi kutokuwa na matumaini."

Idadi ya waliofariki Gaza inaongezeka bila kupunguzwa

Ghasia za hivi karibuni zilikuja wakati mkuu wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Bi Catherine Russell, alisema zaidi ya watoto  14,500 wameripotiwa kuuawa huko Gaza huku maelfu ya wengine wakiaminika kufukiwa chini ya vifusi. Pia alitoa tahadhari juu ya njaa ambayo "inaendelea kutanda kaskazini" huku ufikiaji wa misaada ya kibinadamu ukibaki "umezuiliwa vikali." Matukio hayo ya kusikitisha yamekuja huku mamlaka huko Gaza ikiripoti kuwa zaidi ya watu 45,000 wameuawa katika eneo hilo katika kipindi cha miezi 14 iliyopita. Bi Catherine Russell alisema kwenye mtandao wa kijamii kwamba "takriban watoto milioni 1.1 huko Gaza wanahitaji ulinzi wa dharura na msaada wa afya ya akili," wakati jeshi la Israeli lilipofanya mashambulizi katika muda wa saa 24 zilizopita na kusababisha vifo vya Wapalestina 69, kutoka Beit Lahia kaskazini hadi. Rafah kusini.

Kukata tamaa ya msaada wa chakula uliozuiliwa

Mkuu wa Mawasiliano ya Dharura wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Jonathan Dumont, aliiambia Habari ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano kwamba "raia wanatamani sana msaada wa kuokoa maisha na kuna hatari ya kuongezeka kwa njaa."  Alielezea kiwango cha uharibifu katika Ukanda wa Gaza kama "kinachoshangaza kabisa", na akasema watu wengi wamelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Familia, aliongeza, zinaishi ama kwenye mahema au kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka, bila kupata umeme au maji ya bomba. Dumont alionya, "hakuna umeme au maji ya bomba au maji taka (matibabu). Karibu kila mtu amepoteza nyumba yake. Watu wengi wanaishi kwenye mahema. Tuna chakula cha moto, usambazaji ...Watu wamekata tamaa kweli. Unaweza kuiona katika nyuso zao na unaweza kuiona machoni mwao. Ili kuzuia njaa tunahitaji kutafuta njia ya kupata mtiririko thabiti wa chakula ndani. Kwa kukosekana kwa usitishaji mapigano, alihitimisha, kila juhudi lazima ifanywe "kutafuta njia ya kupata chakula chote tulicho nacho nje ya Gaza."

19 December 2024, 17:01