Tafuta

Mwenyekiti mwenza wa Shirikisho la A- na H-Mashirika ya Waathirika wa Bomu la Japan (Nihon Hidankyo) Toshiyuki Mimaki. Mwenyekiti mwenza wa Shirikisho la A- na H-Mashirika ya Waathirika wa Bomu la Japan (Nihon Hidankyo) Toshiyuki Mimaki. 

Toshiyuki Mimaki:Tuokoe ubinadamu kutoka katika silaha za nyuklia

Mahojiano na mtu aliyenusurika katika bomu la atomiki huko Hiroshima,rais mwenza wa Mfuko wa Nihano Hidankyo wa Japan,mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2024.Mimaki anakumbuka mkutano na Papa Francisko nchini Japan mwaka 2019 na anawaomba viongozi wote wa dunia kujitolea kutokomeza tatizo hilo la silaha za nyuklia.

Na Alessandro Gisotti

Majengo yaliharibiwa. Ni tabula rasa. Kiasi kwamba ungeweza kuona bahari ambapo hapo awali kulikuwa na jiji nyuma yake. Ni kumbukumbu isiyofutika ambayo inabaki moyoni mwa mtoto wa miaka mitatu, shahuda wa tukio baya, lisilofikirika ambalo kwa bahati mbaya lilitokea. Ni kumbukumbu ambayo Toshiyuki Mimaki alishirikisha katiaka Gazeti la Osservatore Romano. Leo hii ana umri wa miaka 82 na tangu tarehe 6 Agosti 1945 wakati bomu la atomiki lilipoharibu mji wa Hiroshima, hakuacha kufikiria siku hiyo ambayo ilibadilisha historia ya wanadamu, lakini hata kabla ya hapo ilifuta maisha ya makumi ya maelfu ya watu.  Siku chache zilizopita, mnamo tarehe 10 Desemba 2024, Mimaki alipokea Tuzo ya Amani ya Nobel huko Oslo. Alifanya hivyo akiwa rais mwenza wa Mfuko wa Nihon Hidankyo ambao tangu mwaka 1956, ndipi ulianzishwa ambao umepambana kwa ujasiri na bila kuacha vikosi vya upokonyaji silaha za nyuklia.

Mfuko wa Kijapani unawaleta pamoja Hibakusha, walionusurika katika shambulio la atomiki la Amerika mara mbili huko Hiroshima na Nagasaki mwishoni mwa Vita vya II vya Kidunia. Kujitolea kwa Mfuko wa  Nihon Hidankyo kunatokana hasa juu ya nguvu ya ushuhuda, juu ya nguvu ya upole wa Historia. Thamani inayotambuliwa na Kamati ya Nobel ya Norway, ambayo katika kutoa tuzo hiyo, ilitangaza kwamba “sote tuna jukumu la kutekeleza dhamira ya hibakusha. Dira yao ya maadili ni urithi wetu. Sasa ni zamu yetu. Juhudi za upokonyaji silaha zinahitaji wito wa umma inayosisitizwa." Katika kukaribia kwa Siku ya Amani Ulimwenguni, Toshiyuki Mimaki alijibu maswali yetu na kwanza kabisa alijitambua kama mrithi wa "juhudi za watangulizi wake" ambao walitaka kuunda Mfuko wa Nihon Hidankyo: walionusurika kama yeye wa tukio lisiloelezeka lililotokea asubuhi hiyo ya  tarehe 6 Agosti miaka 79 iliyopita.

"Katika umri wa miaka 3 - alisema - mama yangu, kaka yangu mdogo na mimi tulipigwa na mionzi ya bomu tukimtafuta baba yetu, ambaye alifanya kazi katika shirika la reli huko Hiroshima. Watu wengi walikufa na majengo yakatoweka kwa moto, kiasi kwamba ungeweza kuona njia yote ya bahari. Kaka yangu kwa sasa anatibiwa saratani ya ubongo." Ingawa ni vigumu kurudisha picha kwenye kumbukumbu, kushiriki uzoefu ndio kiini cha dhamira ya hibakusha: kukumbuka janga ili lisitokee tena. Kazi ya haraka sana. Kwa bahati mbaya, katika miaka michache, kiukweli, hata manusura wa mwisho wa mabomu ya atomiki hawatakuwapo tena.  Kwa hivyo ni nini kitafanywa kuweka kumbukumbu hai kwa vizazi vijavyo? "Mji wa Hiroshima-alielezea-umechukua jukumu la kupitisha shuhuda za walionusurika, kuunda mfumo wa kuelimisha vijana kama wajumbe." Kwa upande wa Mimaki, jukumu ambalo Papa Francisko anatekeleza katika kupendelea upunguzaji wa silaha za nyuklia ni muhimu sana. Yeye mwenyewe alikutana na Papa wakati wa ziara yake huko Hiroshima na Nagasaki mnamo Novemba 2019. "Nilikutana na Papa alipokuja kututembelea-alinipa medali katika kesi nyekundu,” alikumbuka. “Nilimwomba ahakikishe kuwa silaha za nyuklia zinakomeshwa. Ninahifadhi picha ya siku hiyo."

Kwa kuzingatia dhamira hii dhidi ya silaha za nyuklia, kamwe katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu uwezekano wa matumizi ya mabomu ya atomiki na hata uwezekano wa mzozo wa nyuklia. Wazimu kwa wale ambao, kama Toshiyuki Mimaki, bado wanapata uzoefu wa kwanza na katika kina cha roho zao hofu ya siku hiyo wakati "Bomu" ilitumiwa dhidi ya raia kwa mara ya kwanza. "Kama silaha za nyuklia zingetumiwa-alibainisha kwa uchungu-ungekuwa mwisho wa ubinadamu. Kwa sababu hiyo, ninaomba serikali za nchi zinazomiliki silaha za nyuklia zijitolee kuziondoa." Kiongozi wa Nihon Hidankyo ana wasiwasi hasa kuhusu hali ya Gaza na Ukraine. "Rais wa Urusi Putin-liakumbuka kwa uchungu-amepunguza kiwango cha matumizi ya silaha za nyuklia, ili aweze kuzitumia wakati wowote. Ni hali ya kutisha. Kila mtu aje Hiroshima na Nagasaki na kutembelea Makumbusho ya Bomu la Atomiki! Ataona ni kiasi gani silaha za nyuklia zinaweza kufanya kwa wanadamu."

31 December 2024, 11:16