Ukraine,kuelekea mazungumzo mapya kati ya Trump na Putin
Na angella Rwezaula – Vatican.
Rais wa Marekani Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya ndege ya (Air Force One) alipokuwa akirejea Washington kutoka Florida kuwa: "Nitazungumza na Rais Putin Jumanne(kwa maana ya tarehe 18 Machi 2025). Tulifanya kazi kwa bidii mwishoni mwa juma." Trump aliongeza kusema kuwa “kuna uwezekano mkubwa kwamba mazungumzo na Putin yatakuwa na matokeo chanya.” Wakati wa mkutano huo, Trump alisema, watazungumza pia kuhusu maeneo na mitambo ya nishati. Naye Mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff alisema Dominika 16 Machi 2025 kwamba, Trump na Putin watakuwa na "majadiliano ya kuvutia na chanya ndani ya Juma."
Moscow,Kyiv na Washington zinataka vita imalizike
Moscow, Kyiv na Washington "zinataka hii imalizike," mwanadiplomasia huyo aliongeza kwa shirika la Ahabari la (CNN). Bado haijafahamika ni masharti gani yatapelekea Urusi kuidhinisha usitishaji huo. Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, zinaeleza kuwa Kyiv huenda ikalazimika kujinyima uanachama wake na NATO na kukubali kuachia maeneo yanayokaliwa kwa sasa na majeshi ya Moscow.
Kyiv Inabadilisha Uongozi wa Kijeshi, Kombora jipya lilijaribiwa
Wakati mazungumzo ya mapatano kati ya Urusi na Ukraine yakiendelea, Zelensky alitangaza mjini Kyiv kwamba wanajeshi wa Ukraine wamefanyia majaribio kombora jipya la masafa marefu lenye uwezo wa kuchukua umbali wa kilomita 1,000. Kwa hiyo, Long Neptune inayozalishwa nchini ingeweza kufika Moscow. Vyanzo kadhaa visivyo rasmi vinaripoti kwamba shambulio la Ijumaa kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta cha Tuapse katika eneo la Krasnodar la Urusi lilitekelezwa kwa kombora hilo jipya. Wakati huo huo, Zelensky mwenyewe alitangaza mabadiliko mapya juu ya Kikosi cha Wanajeshi, akimbadilisha Mkuu wa Wafanyakazi Anatoly Barhylevych na Meja Jenerali Andriy Gnatov. Uamuzi huo ungejibu hitaji la kuongeza "ufanisi wa usimamizi wa wima wa vikosi vya jeshi", kulingana na rais wa Ukraine.
Ukraine yaangusha ndege 90 kati ya 174
Jeshi la Ukraine lilitangaza kuwa limeangusha ndege 90 kati ya 174 zilizorushwa na Urusi usiku kucha. Vikosi vya Urusi, kwa upande wao, vilisema viliharibu ndege 72 za Ukraine zilizolenga maeneo kadhaa ya Urusi, pamoja na Kursk. Pia usiku kucha, vikosi vya Ukraine vilifanya shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani kwenye vituo kadhaa vya miundombinu, pamoja na eneo kubwa la mafuta na nishati, katika mkoa wa Astrakhan nchini Urusi. Shambulio hilo - linaripoti shirika la habari la Urusi Tass - lilisababisha moto, mtu mmoja alijeruhiwa na mitambo ambayo wafanyikazi walikuwa wamehamishwa.