Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Finale (Allegro giusto)
Ratiba Podcast
Maadhimisho ya Wiki ya Afya 2025 Nchini Tanzania yanafanyika kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 3 hadi 8 Aprili, 2025 . Maadhimisho ya Wiki ya Afya 2025 Nchini Tanzania yanafanyika kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 3 hadi 8 Aprili, 2025 . 

Maadhimisho ya Wiki ya Afya Tanzania 3-8 Aprili 2025: afya Ya Akili

Maadhimisho ya Wiki ya Afya 2025 Nchini Tanzania yanafanyika kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 3 hadi 8 Aprili, 2025 kwa kunogeshwa na kauli mbiu: “Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea Tunajenga Taifa Imara lenye Afya” huku Huduma na Elimu ya Afya vikiendelea kutolewa na kwamba, kilelele cha maadhimisho haya kitafanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais Samia Suluhu Hassan. Umuhimu wa Afya ya Akili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ugonjwa wa afya ya akili unajumuisha aina mbalimbali za matatizo ya fikira, hisia, au tabia. Kila mtu wakati mwingine huwa na mawazo yanayosumbua au yasiyo ya kawaida au hisia kali. Na watu wengi huonesha tabia ambazo wakati mwigine watu wengine huwa wanadhani ni za ajabu. Hata hivyo, kwa watu wenye changamoto ya afya ya akili, mawazo, hisia na tabia hizi hutokea mara kwa mara au ni kali kiasi kwamba watu hupata matatizo makubwa katika maisha yao ya kila siku au kufadhaishwa sana. Kuna aina nyingi za magonjwa ya akili. Ugonjwa wa akili unaweza kuwa wa muda mfupi au mrefu. Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kutofautisha ugonjwa wa akili na wasiwasi wa kawaida au huzuni, lakini ugonjwa wa akili ni mbaya zaidi, hudumu kwa muda mrefu, na huathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa mtu wa kukabiliana na changamoto za maisha. Karibu nusu ya watu wazima hupata dalili za ugonjwa wa akili na wakati fulani sonona ndio huwapata zaidi. Matibabu ya msingi ni dawa na ushauri nasaha, hii ni tiba ya kuzungumza. Familia, marafiki, na vikundi vya usaidizi vinaweza kusaidia watu kukabiliana kikamilifu na magonjwa pamoja na changamoto ya afya ya akili. Maadhimisho ya Wiki ya Afya 2025 Nchini Tanzania yanafanyika kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 3 hadi 8 Aprili, 2025 katika maeneo mbalimbali kwa kunogeshwa na kauli mbiu: “Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea Tunajenga Taifa Imara lenye Afya” huku Huduma na Elimu ya Afya vikiendelea kutolewa na kwamba, kilele cha maadhimisho haya kitafanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Juma hili ni muhimu sana katika kuongeza uelewa wa afya ya akili na hivyo kuleta mabadiliko chanya kwa afya ya akili katika ujumla wake. Ni nini kifanyike ili kukabiliana na changamoto za afya ya akili, maboresho ya afya ili kuwawezesha watanzania kuboresha afya zao katika ujumla wake. Afya ya akili ni muhimu sana kwa ustawi, maendeleo na mafao ya wengi kwani humwezesha mtu kuishi kwa furaha, matumaini, tija na hivyo kujisikia vyema! Takwimu zinaonesha kwamba, mtu mmoja kati ya nane duniani anasumbuliwa na tatizo au na changamoto ya afya ya akili.

Mfumo wa Teknolojia ya akili unde utasaidia maboresho ya afya
Mfumo wa Teknolojia ya akili unde utasaidia maboresho ya afya

Kwa upande wa Tanzania kuna watu zaidi ya milioni saba wenye matatizo ya afya ya akili, kuna watu milioni moja nukta tano wanasumbuliwa na ugonjwa wa Sonona, kihoro, “Schizophrea” na dawa za kulevya. Kumbe, kuna umuhimu kwa watanzania kuzungumza kuhusu matatizo na changamoto za afya ya akili mintarafu maendeleo makubwa ya teknolojia na utandawazi. Ikumbukwe kwamba, Afya ya akili ya mwanadamu inaweza kudhoofishwa na mambo mbalimbali kama inavyoelezwa katika tafiti nyingi za kitaalamu. Kwanza, msongo wa mawazo (stress) wa mara kwa mara huathiri utendaji wa ubongo na huweza kusababisha magonjwa kama sonona na wasiwasi. Pili ni unyanyapaa na ubaguzi wa kijamii na kijinsi au kidini ambako huwafanya watu kuhisi kutengwa, hali inayoweza kuchangia matatizo ya kisaikolojia. Tatu, matatizo katika mahusiano ya kifamilia au kijamii huweza kuathiri hali ya kihisia na kuongeza hisia za huzuni au hasira. Nne, matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya hubadilisha mfumo wa fahamu na kuharibu amani na utulivu wa akili. Afya ya akili huleta madhara mtu anapoamua kuzingatia “tatizo ni nini” badala ya “kile kilicho kizuri na kinachoendelea vizuri.” Watu wengi wanaweza kujua dalili za magonjwa ya kimwili, kama vile mshtuko wa moyo au kiharusi lakini hawajui afya mbaya ya akili. Baadhi ya ishara na dalili ni pamoja na: Kuhisi huzuni au huzuni kila wakati; Kupunguza uwezo wa kuzingatia; Kujiondoa kutoka kwenye mahusiano na mafungamano ya kijamii na shughuli za kila siku za maisha. Mabadiliko makubwa katika tabia ya kula na kulala. Mawazo ya kujiua na hisia za upweke hasi. Kufikiri kupita kiasi na hisia za hatia. Mabadiliko ya hali ya juu. Kujitenga na ukweli, “paranoia” au ndoto au hata udanganyifu kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto pamoja na shida za kila siku za maisha. Shida kuhusiana au kuelewa hali na watu. Matumizi mabaya ya dawa. Mabadiliko ya ngono. Hasira nyingi, uadui au vurugu. Mabadiliko makubwa katika kula na kulala kwani ukosefu wa usingizi wa kutosha hupunguza uwezo wa ubongo kufanya kazi vizuri na huongeza hatari ya matatizo ya afya ya kiakili.

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania mgeni rasmi wiki ya afya Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania mgeni rasmi wiki ya afya Tanzania

Kwa ujumla, mambo haya yanahitaji kushughulikiwa kwa makini ili kuimarisha afya ya akili kwani wahenga wanasema ni muhimu sana kuwekeza katika kinga kuliko tiba. Wataalam wa sayansi na teknolojia wanaendelea kuchakarika usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba, wanaivalia njuga changamoto ya afya ya akili, kwa kutumia simu janja na app, ili aweze kujipima mwenyewe afya yake ya akili. Baada ya mtumiaji kufahamu hali yake ya afya ya akili ataweza kuchukua hatua ya kuonana na daktari wa masuala ya afya na hivyo kuokoa rasilimali muda ambao ingetumika kufahamu kama mtu anakabiliwa na changamoto ya afya ya akili au la! Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM, mwezi Juni kinatarajiwa kuzindua mfumo wa matumizi ya teknolojia ya Akili Unde, “Akili Mnemba” “Akili Bandia” “Artificial Intelligency” utakaomwezesha mtu kujipima na hivyo kubaini changamoto za afya ya akili kwa kutumia simu janja au kompyuta.Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa hivi karibuni amesema Serikali ya Tanzania inatarajia kuanzisha Baraza la Afya ya Akili litakalosimamia muundo utakaoratibu Sekta mbalimbali za kitaaluma na kiutendaji ili kushugulikia ufanisi wa suala la afya ya akili. Majaliwa amesema hilo Bungeni Jijini Dodoma hivi karibuni wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu aliyetaka kujua tamko la Serikali kuhusu kuanzisha Baraza hilo baada ya kukithiri matukio yasiyo ya kawaida yanayochangiwa na tatizo la afya ya akili ikiwemo wizi, mauaji na mapenzi ya jinsia moja. “Mpango wa Serikali ni kukamilisha taratibu zote za uundwaji wa Baraza ili lianze kufanya kazi na kwa kuwa Mbunge ni kinara tutamshirikisha katika afya ya akili pamoja na kuhakikisha kwamba tunaweka mpango kazi wa kutekeleza ajenda hii ya afya ya akili.” Alisema Waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Wiki ya Afya Akili
07 Aprili 2025, 14:09
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031