Tafuta

Askofu  Peter Okpaleke wa Jimbo Katoliki la Ekwulobia,Nigeria Askofu Peter Okpaleke wa Jimbo Katoliki la Ekwulobia,Nigeria 

Nigeria:Maaskofu watoa wito wa amani na upatanisho

Katika fursa ya kuanza kipindi cha Kwaresima,maaskofu nchini Nigeria wamezidisha miito yao kwa ajili ya Amani na upatanishao katika nchi hiyo.Hata hivyo vurugu (za kimwili, za matusi na kisaikolojia) pia zinaongezeka kusini-mashariki mwa nchi kama alivyosema Askofu Peter Ebere Okpaleke,wa jimbo katoliki la Ekwulobia,Nigeria.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kujenga amani kwa kusameheana na kuelimishana, huo ndiyo wito uliozinduliwa katika jumbe  nyingi  za Kwaresima kutoka kwa Maaskofu mbalimbali nchini Nigeria. “Viongozi wetu hapa kaskazini wanapaswa kufanya elimu kuwa kipaumbele badala ya kupigania madaraka”, alisema hayo  Askofu Mkuu Matthew Man-Oso Ndagoso, wa jimbo kuu la  Kaduna, kaskazini mwa Nigeria, ambako vuguvugu kubwa lilizaliwa la Boko Haram  ( ikiwa na maana Elimu ya Magharibi ni marufuku), na zaidi ni vurugu  zinazoendelea kudhoofisha eneo hilo la nchi. Maasi hao wa Boko Haram Kaskazini-mashariki yanatokana na ukosefu wa elimu, eneo la kaskazini la nchi limeshikilia mamlaka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya nchi hii na kwama  kuna sehemu ya Nigeria ambayo inapaswa kufurahia 'elimu,badala yake, amesema kwamba maaskofu ndiyo wanaonekaka kuwa wabaya zaidi katika karibu kila kitu,  alishutumu Askofu Mkuu wa Kaduna.

Hata hivyo vurugu (za kimwili, za matusi na kisaikolojia) pia zinaongezeka kusini-mashariki mwa nchi kama alivyosema Askofu  Peter Ebere Okpaleke, wa jimbo la  Ekwulobia, Nigeria.  Askofu wa jimbo hilo amebainisha  kwamba “uchokozi na vitisho vimepanda zaidi na  kuwa moja ya mtindo wa maisha na mbinu ya kuendelea kuishi. “Bado kiini cha wito wetu wa Kikristo ni kuingizwa kwa ustaarabu wa upendo” ameongeza na kwamba, kama Papa Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosema. Askofu Ebere alithibitisha kuwa   ni muhimu kupitia upya mtazamo wao kuhusu vurugu kwa upande mmoja, upatanisho, kuheshimiana, ukarimu na mshikamano kwa upande mwingine kuwa na uongofu unaanzia kujidhihirisha katika lugha inayotumika kwa sababu maneno ni madirisha ya mioyo ya kila mtu.

Askofu Mkuu Alfred Martin wa Jimbo Kuu Katoliki la Lagos nchini Nigeria
Askofu Mkuu Alfred Martin wa Jimbo Kuu Katoliki la Lagos nchini Nigeria

Naye Askofu Mkuu wa Lagos Alfred Adewale Martins, wakati wa kutoa tafakari yake ya kwanza ya Kwaresima iliyopewa mada: “Safari ya kurudi”, katika tukio la Jumatano ya Majivu, aliwaalika wanasiasa na wahubiri wa uwongo kutubu. Askofu mkuu Martins pia aliwataka viongozi wa serikali wafisadi, na wale wanaofanya uhalifu wa kikatili na utekaji nyara, watubu kwa kuwa ni wakati wao. Na hatimaye, Askofu Mkuu aliwaalika waamini kuombea amani nchini Ukraine.

04 March 2022, 16:05