Tafuta

2023.01.09 Afrika nzima ilimwombea Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI kupitia Radio Maria katika Madhabahu ya Maria huko Kibeho Rwanda. 2023.01.09 Afrika nzima ilimwombea Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI kupitia Radio Maria katika Madhabahu ya Maria huko Kibeho Rwanda. 

Bara la Afrika lilimwombea Hayati Papa mstaafu Benedikto XVI

Wakati waamini wakatoliki na wasio wakatoliki wanaomboleza kifo cha Hayati Papa Mstaabu Benedikto XVI,mjini Vatican na kwingineko duniani,hata Bara la Afrika iliungana kusali Rosari kupitia Radio Maria Afrika katika Kikanisa cha Madhabahu ya Bikira Maria,Kibeho Rwanda.Mungu ampumzishe mahali pema Papa wetu.Amina.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Dominika tarehe 8 Januari 2023, katika uwanja wa Mtakatifu Petro majira ya saa sita kamili kulikuwa na watu zaidi ya 30 elfu wakimsikiliza Baba Mtakatifu Francisko tafakari yake na baadaye sala ya Malaika wa Bwana. Na wengi wa waamini na mahujaji hao  walikuwa tayari wamekwenda kutembelea groto za Vatican  yaani chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, zilizofunguliwa asubuhi saa 3.00 kamili katika kaburi la Hayari  Papa mstaafu Benedikto XVI ili kusali kwa ajili yake.

Kaburi la Hayati Papa Mstaafu Benedikito XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Kaburi la Hayati Papa Mstaafu Benedikito XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Hata Bara la Afrika nzima liliungana na ulimwengu wote kumuombea hayati Papa msataafu Benedikito XVI aliyeanga dunia mnamo tarehe 31 Desemba 2022, majira ya saa 3.34 asubuhi na kuzikwa tarehe 5 Januari 2023. Sala ya Rosari iliongozwa katika Madhabahu ya Bikiria Maria huko Kibeho nchini Rwanda, kwa kuungana pamoja kupitia Radio Maria. Aliyeongoza Sala ya Rosari ni Msimamizi wa Madhabahu hiyo  ya Bikira Maria, Kibeho,  Padre Francoise Harelimana. Sala ya Rosari iliongozwa kwa lugha ya Kiingereza na kifaransa katika Kikanisa kidogo cha Tokeo la Bikira Maria huko Kibeho nchini Rwanda. Ushiriki wa Radio Maria Afrika ulifanyika manmoa tarehe 31 Desemba, majira ya jioni saa 12.00 kamili.

Waamini wakisali katika Kikanisa cha tokeo cha Madhabahu ya Bikira Maria huko Kibeo
Waamini wakisali katika Kikanisa cha tokeo cha Madhabahu ya Bikira Maria huko Kibeo

Kwa hakika ushiriki wa Radio Maria Afrika kwa lugha ya kifaransa zilikuwa ni: Burundi, Camerun katika stesheni ya Yaoundé,  Guinea Conakry, nchini Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo (DRC) na stesheni zake: Pointe Noire, Ouesso, Kinshasa, Bukavu, Goma, Kisangani, Lubumbashi, Mbandundu, na Matadi; nchini Rwanda; Togo katika stesheni zake Lomé, Dapaong, Kara, Atakpamé na  Kpalimé

Kwa upande wa lugha ya kiingereza, walishiriki Radio Maria: KENYA katika steshi zake za Nairobi, Murang’a, Kisumu; Lesotho, Liberia, Malawi, Nigeria  kwenye stesheni ya Abuja, Sierra Leone, Tanzania, Uganda katika stesheni zake: Kampala, Mbarara, Kabale, Hoima, Nebbi, Mbale, Gulu, na  Moroto,  huko Zambia, katika stesheni za Lusaka, Chipata na Livingstone. Lakini pia ziliunganishwa na Radio Maria Ulaya kama vile  Radio Maria Ufaransa na Radio Maria Uswiss.

Waamini wakisali Rosari katika madhabahu ya Bikira Maria, Kibeho Rwanda
Waamini wakisali Rosari katika madhabahu ya Bikira Maria, Kibeho Rwanda

Hayati Papa mstaafu Benedikoto XVI ambayetangu mwanzo alikuwa amejifafanua kama "mfanyakazi mnyenyekevu katika shamba la Bwana", ni maneno ambayo yametufanya kwa hakika kuelewa umuhimu wa huduma yake aliyoifanya kama mfuasi wa Mtume Petro. Kwa maana hiyo ameacha urithi mkubwa wa tafakari ya kitaalimungu na kichungaji, na zaidi kwa mtazamo wa marejeo mengi. Inatosha kukumbuka nyaraka zake za kitume, lakini pia hata katekesi na mahubiri yake aliyotamka, ni maandiko yenye thamani kubwa sana za kimungu!

Waamini wakisari rosari kumuombea Papa Mstaafu Benedikto XVI aliyeaga dunia 31 Desemba 2022
Waamini wakisari rosari kumuombea Papa Mstaafu Benedikto XVI aliyeaga dunia 31 Desemba 2022

Hayati  Papa Mstaafu Benedikto XVI ametuachia maelekezo muhimu ya kuendelea kuishi kwa roho na upendo mkubwa wa Mtaguso wa II wa Vatican ili Kanisa liwe daima lenye uwezo wa "kuzungumza kwa watu wa kila kizazi na daima lenye uwezo wa kuunganisha imani na sababu, upendo na ukweli." Hatutamsahau kamwe kwani Hayati Benedikto XVI alikuwa mfano mzuri wa upendo wa Injili na Kanisa. Maandiko yake, yamejaa upendo mkubwa na shauku kama ile ile aliyokuwa nayo Mtakatifu Agostino, Baba wa Kanisa  ambaye alimuiga hata  katika kazi yake ya mwisho kwenye masomo ya kitaalimungu (Thesisi) ilihusu yeye na  akaweza kundika Waraka wake wa Kitume  wa kwanza  kuhusu upendo uitwao " 'Deus caritas est'  mnamo tarehe 25 Desemba 2005.

Waamini wameanza kwenda kusali katika kaburi la Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI tangu 08.01.2023
Waamini wameanza kwenda kusali katika kaburi la Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI tangu 08.01.2023

Katika utangulizi wake aliandika kuwa: "Mungu ni upendo; yeye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake” (1 Yoh 4:16). Maneno haya kutoka katika Waraka wa Kwanza wa Yohane yanaeleza kwa uwazi wa pekee kiini cha imani ya Kikristo: sura ya Kikristo ya Mungu na pia taswira ya mwanadamu na safari yake. Zaidi ya hayo, katika mstari huohuo, Yohane anataka kama kusema kusema, mfumo wa kuwako wa Kikristo: “Tumetambua upendo alio nao Mungu kwetu na tumeuamini."

Afrika nzima imesali rosari kupitia Radio Maria Afrika kwa ajili ya Hayati Papa Mstaafu XVI
09 January 2023, 11:51