Nicaragua:mapadre na waseminari waliachiliwa na kufukuzwa,wako Marekani
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kutoka Managua hadi Washington, haki ya Nicaragua ya serikali ya Rais Daniel Ortega imewaachilia na kuwafukuza wafungwa wa kisiasa 222, wakiwemo mapadre watano, shemasi mmoja na waseminari wawili walioshutumiwa kwa njama. Wote tayari wamewasili nchini Marekani, ambapo wanapaswa kuwapatiwa vibali vya makazi kwa kipindi cha awali cha miaka miwili.
Kunyimwa haki
Mahakama ya Rufaa ya Managua huko Nicaragua ilikubali hatua hiyo, ikisisitiza “kufukuzwa mara moja na madai ya "kupatikana na hatia ya kufanya vitendo vinavyodhoofisha uhuru, na kujitawala kwa watu, kwa kuchochea vurugu, ugaidi na kudhoofisha uchumi”. Waliofukuzwa walitangazwa kuwa ni “wasaliti wa nchi ya asili”, “haki zao za raia zilisimamishwa kwa maisha yao yote” na kunyimwa uraia wa Nikaragua. Kulingana na orodha iliyotolewa na mamlaka, miongoni mwa waliopokea kama adhabu kuna makuhani ambao ni: Óscar Benavides, Ramiro Tijerino, Sadiel Eugarrios, José Díaz na Benito Martínez; shemasi Raúl Vega; waseminari Melkin Centeno na Darvin Leyva na pia waendeshaji wawili wa vyombo vya habari kutoka Jimbo la Matagalpa, Manuel Obando na Wilberto Astola.
Askofu Alvarez bado yuko gerezani
Naye Askofu wa Jimbo la Matagalpa na msimamizi wa kitume wa Jimbo la Estelí, Rolando José Álvarez, ambaye baadaye alithibitishwa na mamlaka, alikataa kufukuzwa na bado amezuiliwa katika gereza la Nicaragua la Modelo huko Tipitapa. Kwake yeye, hukumu inaweza kusikika tarehe 15 Februari 2023. Hata makuhani wengine wawili, Manuel García na José Urbina, wa jimbo la Granada, pia bado wako kizuizini.