Tafuta

2023.04.18 Tanzania: Askofu Kilaini na Rweyongeza katika kituo cha KWAUSO katika kesha la Siku Kuu ya Huruma 2023. 2023.04.18 Tanzania: Askofu Kilaini na Rweyongeza katika kituo cha KWAUSO katika kesha la Siku Kuu ya Huruma 2023. 

Tanzania:Askofu Kilaini ameomba waamini wakimbilie huruma ya Mungu

Waamini wanapotafuta Huruma ya Mungu,mwanadamu anakua na Yesu mwenyewe pamoja na Mama yake Bikira Maria na kuwakumbusha waamini kila wakati Kujisadikisha kwa Kristo mfufuka.Alisema hayo Askofu Kilaini katika mkesha wa Huruma ya Mungu huko KWAUSO Bukoba.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Dominika ya huruma ya Mungu ilianzishwa rasmi na Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo mwaka 1992 ambayo aliiwekwa kwa ajili ya Kanisa zima la Ulimwengu kila Dominika ya kwanza baada ya Pasaka, na ambayo kiiutamaduni uitwa ile “Domenica in albis”. Uchaguzi wa Dominika  ya kwanza baada ya Pasaka una maana kubwa ya kitaalimungu kwa sababu inaoneesha uhusiano wa karibu kati ya fumbo la Pasaka la Ukombozi na sikukuu ya Huruma, jambo ambalo Sr. Faustina mhusika mkuu wa tukio hili na Bwana pia alibainisha kwamba: “Sasa ninaona kuwa kazi ya Ukombozi imeunganishwa kwa kazi ya huruma iliyoombwa na Bwana.” Kiungo hiki kinasisitizwa zaidi na novena inayotangulia sikukuu na ambayo huanza Ijumaa Kuu.  Katika muktadha huu, Yesu alieleza kwa Faustina  sababu iliyomfanya aombe sikukuu hiyo ianzishwe kwamba: “Nafsi zinaangamia, licha ya Mateso Yangu yenye uchungu (...).

Maadhimisho ya kubariki Kikanisa cha Huruma ya Mungu huko Kwauso
Maadhimisho ya kubariki Kikanisa cha Huruma ya Mungu huko Kwauso

Wasipoabudu huruma yangu, wataangamia milele”. Kwa hiyo katika maandalizi ya karamu lazima yawe na  novena, ambayo inajumuisha Kusali Rosari ya Huruma  ya Mungu kuanzia Ijumaa Kuu. Novena hii ilitamaniwa na Yesu na akasema juu yake kwamba “atatoa neema za kila aina”. Katika mkesha wa Siku Kuu ya Huruma ya Mungu kwa mwaka 2023 waamini Wakristu wakatoliki wamliombwa kutafuta na kuikimbilia huruma ya Mungu na kujiaminisha kwa Kristu mfufuka. Wito huo ulitolewa na Askofu Method Kilaini Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Bukoba,  wakati wa homilia yake Jumamosi  tarehe 15 Aprili 2023, katika madhimisho la Misa Takatifu ya kubariki ujenzi wa Kanisa la Huruma ya Mungu,  katika Shule ya Sekondari ya “Kwaheshima ya Uso Mtakatifu wa Yesu (KWAUSO) Jimbo Katoliki la Bukoba, Tanzania.

Wanafunzi wa SEKONDARI YA KWAUSO
Wanafunzi wa SEKONDARI YA KWAUSO
MAPADRE NA MAASKOFU HUKO KWAUSO, BUKOBA
MAPADRE NA MAASKOFU HUKO KWAUSO, BUKOBA


Padre Stanislaus Mutajwaha, ambaye ni Padre wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Tanzania ni mwanzilishi wa Shule ya Sekondari ya ‘KWAUSO’, ambayo ni Shule ya bweni mchanganyiko wa wasichana kwa wavulana chini ya umiliki wa Jimbo Katoliki la Bukoba. “Hiyo ni Shule iliyojengwa kama tunda au mrejesho wa tafakari ya dhati juu ya Sanda ya Torino hiyo hiyo ili kumuenzi Yeye Yule tunayemkumbuka kila tunapoutazama Uso unaoonekana juu yake”, alisema  na vyombo vya habari Vatican, Padre  mwanzilishi na kwamba alifikiwa na wazo la Sanda kwa mara ya kwanza bila kutegemea mwezi Aprili mnmo mwaka 1985, ikiwa ni  mwaka wake  wa 8 wa upadrisho, alipokutana na taarifa juu yake katika gazeti moja linaloitwa National Geographic Magazine, Toleo la mwezi Juni mwaka 1980. Kwa sasa imekuwa ni kituo kikuu cha kuheshimu nakala ya Sanda hiyo kilichokubaliwa na Baraza la maaskofu hivi karibuni 2022, ambapo kilizunduliwa rasmi na kufikiwa na baadhi ya Maasofu wengi wa Tanzania.

Je Sr. Faustina Kowalska alikuwa ni nani?

Alizaliwa katika kijiji cha Kipoland na kubatizwa  kwa jina la Elena, yeye alikuwa ni  mtoto wa tatu kati ya watoto 10 wa Marianna na Stanislaus Kowalski. Wazazi wake walikuwa ni wakulima maskini, katika nchi ya Poland iliyokuwa inagawanywa na imaya kati ya Urussi, Ujerumani na Austria. Alienda shule kwa miaka mitatu, kisha akaingia kwenye huduma. Alifikiria kuwa mtawa akiwa mtoto, lakini aligundua mpango huo mnamo Agosti 1925 akiwa huko Warsaw  ambao ni mji mkuu wa Poland huru  na kujiunga na shirika la watawa wa  Bikira wa Huruma, na kuchukua majina ya Maria Faustina. Naye ni mpishi, mtunza bustani, mhudumu, kisha anapitia nyumba mbalimbali za Kutaniko (pamoja na zile za Warsaw, Vilnius na Krakow).

Picha ya Mtakatifu Faustina Kowalska
Picha ya Mtakatifu Faustina Kowalska

Akiwa shirikani alikuwa mpokeaji wa maono na mafunuo ambayo waungamishaji wake walipendekeza aandike katika shajara (iliyotafsiriwa baadaye na kuchapishwa katika lugha nyingi). Na bado haamini kwamba matukio haya ya ajabu ni alama ya utakatifu. Unaandika kwamba ukamilifu unafikiwa kupitia muunganiko wa ndani wa roho na Mungu, sio kupitia neema, mafunuo, furaha. Badala yake, hizi ni njia za mwaliko wa kimungu kwake, ili kuelekeza uangalifu kwa yale ambayo tayari yamesemwa, katika maandishi ya Maandiko ambayo yanazungumza juu ya huruma ya kimungu na baadaye kuchochewa imani kwa Bwana kati ya waamini isemayo: “Yesu, ninakutumaini” na nia ya kuwa na huruma binafsi. Sr. Faustina alikufa akiwa na umri wa miaka 33 huko Krakow nchini Poland. Alitangazwa kuwa mwenye heri mnamo mwaka 1993, wakati huo huo akatangaza kuwa mtakatifu mnamo mwaka 2000 na Mtakatifu Yohane Paulo II. Mabaki hayo yapo huko Krakow-Lagiewniki, katika kanisaMadhabahu ya Huruma ya Mungu. Sikukuu yake inaadhimisha na Mama Kanisa tarehe 5 Oktoba yak ila mwaka.

Mahubiri ya Askofu Kilaini kuhusu huruma ya Mungu huko KWAUSO Bukoba Tanzania
18 April 2023, 16:48