Masalia ya Mwenyeheri Carlo Acustis yatakuwa Ireland
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Askofu Domenico Sorrentino wa jimbo la Assisi – Nocera Umbra – Gualdo Tadino na Foligno katika matazamio ya hija ya masalia ya kijana Mwenyeheri Carlo Acustis yanayotarajiwa kuanzia tarehe 11-15 Mei katika Jimbo Armagh, Down na Connor nchini Ireland amesema: “Tunafurahi kwamba masalio ya Mwenyeheri Carlo Acutis yanaweza kufika Ireland kwa sababu tunasadiki, kutokana na uzoefu wa hapo awali, ambao kwa kijana huyu, alijitolea na ambaye aliishi Injili kuwa ni mfano na msaada kwa Kanisa na vijana wengi ambao wanatafuta vidokezo vya kufahamu uzuri wa imani.
Kwa mujibuwa taarifa kutoka Jimbo hilo atakayesindikiza kipande cha pericardium yake, yaani Kiungo cha utando ambacho, kama gunia, hufunika na kulinda moyo na mishipa mikubwa ya moyo, atakuwa Monsinyo Anthony Figueiredo, mhusika wa Mahusiano ya Kimataifa.
Mwenyeheri Carlo Acutis, ambaye angesherehekea miaka 32 ya maisha yake, tarehe 3 Mei 2023, alikufa kutokana ugonjwa wa saratani ya damu akiwa na umri wa miaka 15 tu mnamo mwaka 2006, na aliweka maisha yake yote hasa kwenye Ekaristi ili kukua katika uhusiano wake na Yesu. Akifafanua katika shara lake anaandika kuwa: “Tunapopokea zaidi Ekaristi, ndivyo tutakavyokuwa kama Yesu zaidi”.
Carlo Acutis kwa hiyo alijaribu kuhudhuria Misa kila siku na kutumia muda katika Kuabudu, akiamini kwamba “tunapojikuta mbele ya Yesu katika Ekaristi, tunakuwa watakatifu. Kutokana na tukio hilo hata hivyo linaturejesha kwamba Masalio ya Mwenyeheri Carlo Acutis tayari yameheshimiwa mnamo mwaka 2022 katika Jimbo la Marekani, kisha mnamo Novemba 2022 huko Poland na hivi karibuni yalikuwa kwenye Upatriaki wa Venezia Italia. Kwa hiyo kwa kiangazi hiki hasa wakati siku ya Vijana Duniani WYD huko Lisbon Mwenyeheri Carlo atakuwa mmoja wa wasimamizi wenza na wa siku hiyo na masalio hayo yatatembelea majimbo ya Brazil.