Timket,Kanisa la Ethiopia linaadhimisha Tokeo la Bwana ambalo kwao ni Ubatizo wa Kristo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Timkat ni Epifania ya Kanisa la Kiorthodox la Ethiopia tofauti na Epifania ya Kanisa la Magharibi kama Italia haiadhimisha ujio wa Wafalme Watatu, yaani Mamajusi, badala yake, wao wanaadhimisha Siku Kuu ya Ubatizo wa Kristo. Ambao unaangukia kati ya Januari 19(Januari 20 wakati wa mwaka wa kurukaruka), Timket ni siku za mapumziko makubwa zaidi ya Wakristo wa Kiorthodox nchini Ethiopia ambayo hudumu kwa siku tatu, za safari na sala na mikesha.
Ketera, Mkesha wa Timket
Usiku wa kuamkia Timket unaitwa Ketera. Wakati wa siku huo Tabot, ambayo ni mfano wa Sanduku la Agano na mbao za Sheria ambazo Musa alipokea kwenye Mlima Sinai, kutoka kwa kila kanisa hubebwa kwa maandamano kuelekea mto au bwawa la maji ambapo sherehe ya siku inayofuata inaadhimishwa mahali. Hapa kuna hema maalum ambalo kila tabot hupumzika huku washiriki wa kwaya ya kanisa wakiimba nyimbo. Hii inaambatana na ngoma maalum ya mapadre.
Usiku wa kabla ya Timket
Mapadre, wakiwa wamevaa mavazi ya kiutamaduni na miavuli iliyofumwa kwa uzi wa dhahabu, husali usiku kucha, huimba na kucheza kwa ngoma na ala za kienyeji, wakipeperusha chetezo ambacho hutoa harufu ya uvumba na kuingia hewani, wakibariki maji kuzunguka mwamba wa bwawa au mto au ziwa ambapo sherehe hufanyika siku inayofuata.
Usiku kucha, maelfu ya mahujaji, wakiwemo wanawake wengi waliovalia nguo nyeupe, wanawasili kutoka nchini kote, wakitembea kwa siku baada ya nyingine ili kushiriki katika wakati huu wa kukumbukwa, karibu kana kwamba ni msafara wa kibiblia. Saa 2:00 asubuhi siku inayofuata, misa takatifu huadhimishwa, sherehe hizo hufikia kilele alfajiri, wakati watu wanajizamisha ndani ya maji na kusali.
Siku ya Timket
Baada ya sala, Padre mzee hutumia msalaba wa maandamano ya dhahabu kubariki maji na kuzima mshumaa uliowekwa wakfu unaowaka ndani ya maji. Kisha wanawanyunyiza maji juu ya washiriki lililokusanyika katika ukumbusho wa ubatizo wa Kristo.
Sherehe ya Timket ni ukumbusho, si ubatizo wa kila mwaka. Baada ya ubatizo, Tabot za kila Kanisa, isipokuwa Kanisa la Mtakatifu Mikaeli, huanza kurudi kwenye makanisa yao. Wazee huandamana kwa heshima, wakisindikizwa na uimbaji, makuhani na vijana wanaoruka, kupigwa kwa fimbo na vijiti vya maombi kukumbusha taratibu za kale za Agano la Kale.
Siku iliyofuata ya tarehe 20 Januari ni sikukuu ya Malaika Mkuu Mikaeli, Mtakatifu maarufu zaidi wa Ethiopia, uhaadhimishwa. Na ni asubuhi hiyo tu ambapo Tabot ya Mtakatifu Mikaeli hurudi kanisani kwake. Ndivyo inavyohitimisha sherehe ya siku tatu, muhimu sherehe ya kipekee ya Kanisa la Kiorthodox nchini Ethiopia.