Nicaragua,mapadre wapya 9 wawekwa wakfu.Wito mpya wa UN
Vatican News
Jimbo kuu la Managua nchini Nicaragua limepata mapadre wapya tisa waliowekwa wakfu mnamo tarehe 6 Januari 2024, katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Epifania, yaani Tokeo la Bwana kwa kuongozwa na Askofu mkuu, Kardinali Leopoldo José Brenes Solórzano.Waamini wengi walishiriki kwa shangwe na hisia kali katika ibada hiyo, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Managua.
Brenes: makuhani, mashahidi wa udugu
Katika mahubiri yake, Kardinali alimshukuru mwenyezi “Mungu kwa zawadi ya ajabu ya mapadre wapya, huku akisema kwamba ukuhani si nguvu, bali utume na huduma. Mapadre ni watumishi na mashahidi, wanaoitwa kuishi ushirika na udugu,” alisema.
Wimbi la kukamatwa
Mapadre wapya waliwekwa wakfu katika wakati mgumu kwa Kanisa la Nicaragua. Ni tangu tarehe 20 Desemba 2023, ambapo mapadre wasiopungua 14, waseminari wawili na askofu Isidoro del Carmen Mora Ortega wa Siuna, walikamatwa na kutekwa nyara baada ya kumuombea Aslofu Rolando José Álvarez Lagos, wa jimbo la Matagalpa na msimamizi wa kitume wa Jimbo katoliki la Estelí aliyehukumiwa kifungo cha miaka 26 jela bila kufikishwa mahakamani na bila sheria tangu mwezi Februari 2023. Katika jumuiya ya kikanisa hata hivyo kuna wasiwasi, hasa, kwa mapadre waliotekwa nyara ambao wana matatizo ya kiafya, akiwemo Padre Ismael Serrano, paroko wa Mtakatifu Mikaeli Mkuu na Padre Gerardo Rodrígues, padre wa Kanisa la Mama Safi wa Moyo , ambao wote ni kutoka Jimbo kuu la Managua na ni wagonjwa na wanahitaji matibabu.
UN yatoa wito kwa serikali ya Nicaragua
Kwa upande wake, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu kwa Amerika ya Kati (OACNUDH) amezindua wito mpya kwa serikali ya Nicaragua ili kufichua kwa haraka mahali ambapo AskofuMora, ambaye ni “mwathirika wa kutoweka kwa lazima anashikiliwa kwa siku 16, alipo.” Kwa kuficha habari hizi, kama inavyosemokea( si legge in un post su X )- “ Maisha yake yako hatarini.”
Tayari tarehe 28 Desemba Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu wa Amerika ya Kati (OACNUDH)ilikuwa imelaani “kutoweka kulazimishwa kwa Askofu Isidoro Mora na wimbi jipya la kukamatwa kwa watu wa kidini ni kinyume na haki ya uhuru wa kidini, nguzo ya kila nchi ya kidemokrasia.” Kulingana na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Nicaragua inakwenda “kuongezeka” kutoka katika utawala wa sheria na “kutoka katika uhuru wa kimsingi” kwa kuwatesa “viongozi wa kisiasa na raia, washiriki wa Kanisa Katoliki, wanaharakati na waandishi wa habari” kwa “kesi zinazorudiwa mara kwa mara za kuwekwa kizuizini kiholela.”
Papa Francisko aliombea Maaskofu na mapadre walionyimwa uhuru
Hivi karibuni, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu, alikuwa amewaombea watu wa dini hao. Katika siku hiyo alisema: “Ninafuatilia kwa wasiwasi mkubwa kile kinachotokea Nicaragua, ambako Maaskofu na mapadre wamenyimwa uhuru wao. Nimawaeleza wao, familia zao na Kanisa zima nchini ukaribu wangu katika maombi. Pia ninawaalika ninyi nyote mliopo hapa na Watu wote wa Mungu kusali kwa bidii, huku nikitumaini kwamba ni kutafuta daima njia ya mazungumzo ili kuondokana na matatizo. Hebu tuiombee Nicaragua leo.”
Ikumbukwe kufikia sasa mamlaka ya Nicaragua haijathibitisha wala kukanusha kuzuiliwa kwa mapadre hao ambao waliripotiwa kutoweka.