2020.06.16 Kardinali Zuppi atemebelea Hospitali ya Watoto ya  Charitas ya  Bethlehemu. 2020.06.16 Kardinali Zuppi atemebelea Hospitali ya Watoto ya Charitas ya Bethlehemu. 

Kard.Zuppi katika Hospitali ya Watoto Bethlehemu:mateso ya watoto hayakubaliki!

Rais wa CEI,alifika katika hospitali ya Watoto ya Charitas,ambayo ni pekee ya watoto katika Ukingo wa Magharibi huko Betlhehemu.Ni sehemu ta ratiba ya hija ya amani na mshikamano ya Jimbo Kuu lake kuanzaia tarehe 13-16 Juni.“Siku zote tunachelewa sana kulinda maisha,hapa tunahitaji kujaribu kuwafanya watu wazima wafikirie na kupata ujasiri wa kusitisha mapigano.”

Vatican News

Kardinali Matteo Maria Zuppi, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna na rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI,)  katika Hija iliyoanza tarehe 13 Juni na ambayo imehitimishwa tarehe 16 Juni 2024, aliwasili Bethlehemu tarehe 15 Juni alasiti  katika Hospitali ya Mtoto ya Charitas (Cbh), ambayo ndiyo iliyo  pekee ya watoto katika Ukingo wa Magharibi. Ilikuwa ni ratiba iliyopangwa kuwa sehemu ya hija ya kijimbo iliyoongozwa na mada: “amani na mshikamano” ambayo ilifsanyika kati ya  Yerusalemu na Bethlehemu, na kuongozwa na Kardinali mwenyewe pamoja na washiriki 160 wa Jimbo lake na  kutoka miji mingine ya Italia.

Mahujaji kutoka Italia kwenda Nchi Takatifu

Kardinali Zuppi, akiwa na ujumbe wa mahujaji hao kwa mujibu wa ripoti ya Daniele Rocchi, mwandishi wa Shirika la habari za kidini la Baraza la Maaskofu Italia ( SIR) alibanisha kuwa alikaribishwa baada ya kuwasili kwake na Shireen Khamis, kutoka ofisi ya mawasiliano ya hospitali, ambaye alimwonesha video fupi ya historia ya hospitali ambayo mwaka 2024 inaadhimisha miaka 71 ya shughuli isiyokatizwa. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watoto elfu 410 walio chini ya umri wa miaka 18 wanaishi katika eneo hilo. Historia ya sasa ya Hospitali ya Caharitas ya  Watoto ya inazungumza bila shaka juu ya vita, ile ya Gaza, ambayo inazidisha ugumu wa kuhama familia zinazohitaji kutibiwa watoto wao, lakini pia inazungumza juu ya shida ya kuzidiwa kwa wagonjwa na ukosefu wa matibabu na  vitanda.


 

“Ili kufika Bethlehemu watu wanapaswa kupita katika mamia ya vituo vya ukaguzi vya Israeli. Katika miezi mitatu ya kwanza ya vita, watoto 7,000 hawakuweza kupata matibabu kwa sababu hii,” alifafanua Khamis. “Zaidi ya hayo, vita vilizidisha matatizo makubwa ya kiuchumi ambayo tayari yalikuwa makubwa. Bila utalii na mahujaji familia nyingi zimepoteza kazi na haziwezi kumudu matibabu.” Lakini Hospitali ya Watoto ya Charitas inaendelea kufanya sehemu yake, hata inapochoka, kusaidia watoto wagonjwa: “katikati ya Machi iliyopita kikundi cha watoto 68 kutoka Ukanda wa Gaza walifika Bethlehem. Wakikaribishwa katika kituo maalumu, sasa wanafuatiwa na shirika la SOS-Children's Villages, huku msaada wa matibabu ukikabidhiwa hospitali,” alisema Khamis.

Mateso ya watoto hayakubaliki

Kardinali Zuppi akiongozwa na Sr Aleya Kattakayam mwenye dhamana, wa Shirika la Kitawa la Maria Bambina linayosimamia Hosptiali hiyo (Cbh), alitembelea idara mbalimbali, kuwasalimia na kuwakumbatia baadhi ya watoto wadogo waliolazwa hospitalini, kwa wazazi wao walioonekana kuwa na matatizo, kisha aliweza kuzungumza na madaktari na wauguzi. “Tuko mahali ambapo mateso ya watoto wengi yanapata tiba. Lakini hii sio wakati wote. Ni lazima tuanzie hapa kuelewa ni nini kinahitajika kwa wadogo na wanyonge zaidi ili waweze kupata kila kitu wanachostahili. Mateso ya watoto hayakubaliki. Na hapa tunahitaji kujaribu kuwafanya watu wazima wafikirie.” Alisema Kardinali na  Kuhusiana na hilo  Kardinali alitaka kuwakumbuka watoto wa Israel waliouawa tarehe 7 Oktoba 2023 wakati wa shambulio la Hamas dhidi ya Israel na watoto wa Kipalestina waliofariki Gaza katika miezi hii 8 ya vita. “Baadhi ya Wagaza hawa wadogo walitibiwa katika hospitali za Italia, pamoja na huko Bologna. Nilisikia mambo ya kutisha kutoka kwao, kama kukatwa viungo bila ganzi.”

Linda maisha na kupata ujasiri wa kusitisha mapigano

“Lazima tuwaandalie maisha ambayo yanawezekana kwao, kwa kuwatazama tunaelewa nini tunapaswa kufanya. Chuki, mantiki mbaya ya unyanyasaji, kutoweza kuelewa mateso ya wengine na kufikiria tu ya mtu mwenyewe ni mambo ambayo yanazalisha ukatili zaidi na wahasiriwa wasio na hatia kama vile watoto, aliongeza Askofu Mkuu wa Bologna ambaye alitaka kurejea maneno yake. Rachel Goldberg-Polin, mama wa kijana Hersh, mateka wa Hamas huko Gaza, alikutana mwanzoni mwa hija. “Mwanamke huyu alikuwa akifikiria maumivu yake na ya wengi huko Gaza. Rachel alisema kitu sahihi sana: 'Nataka maumivu yangu yasisababishe maumivu zaidi'. Maana ya ziara hii ni kuelewa maumivu na kukabiliana nayo kwa upendo mmoja, kukaa karibu, kusaidia na kuomba ili tupate nguvu na ujasiri wa usitishaji wa mapigano na njia ya haraka ya mazungumzo.” Alihitimisha

17 June 2024, 16:54