Papa Francisko:Sala kwa ajili ya waathirika huko Kazakhstan
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 9 Januari 2022 wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Ubatizo wa Bwana, akiwageukia mahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko ameelezea uchungu kwa ajili ya waathirika wakati wa maandamano yaliyoibuka hivi karibuni huko Kazakhstan. Kwa maana hiyo anasali kwa ajili yao na kwa ajili ya familia zao akiwa na matumaini kwamba wanaweza kupata maelewano ya haraka ya kijamii kwa njia ya kutafuta mazungumzo, ya haki na wema wa pamoja. Amewakabidhi watu wa kazakhstan kwa Ulinzi wa Mama Malkia wa amani wa Oziornoje.
Maombi kwa watoto wachanga wamepokea au watapokea ubatizo
Papa Francisko kawa kawaida hakusahau kuwasalimu watu wote, waamini kutoka Roma na mahujaji kutoka Italia na kutoka nchi mbalimbali. Hasa, salamu kwa kikundi kutoka Frattamaggiore, karibu na Napoli, Italia. Akiendelea Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha tukio la Ubatizo katika Kikanisa cha Sisitine mjini Vatican asubuhi kabla ya sala ya Malaika wa Bwana na kusema kwamba: “Asubuhi ya leo, kama kawaida katika Jumapili ya Ubatizo wa Bwana, nilibatiza baadhi ya watoto ambao ni watoto wa wafanyakazi wa Vatican. Ninatumia fursa hii kupanua sala zangu na baraka zangu kwa watoto wote wachanga ambao wamepokea au watapokea Ubatizo wakati huu. Bwana awabariki na Mama yetu awalinde".
Akikumbusha juu ya siku ya ubatizo
Papa Francisko amerudia tena kwa wote kuwahimiza wajifunze na kukumbuka tarehe ya ubatizo wao .” Je Nilibatizwa lini? Hii lazima msisahau na kukumbuka siku hiyo kama siku ya sherehe. Na kwenu nyote ninawatakia Jumapili njema. Tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema na kwaheri ya kuonana”. Amehitimisha Papa Francisko.