Tafuta

Hali halisi nchini Ukraine haijatengemaa na mazungumzo ya kidiplomasia bado hayajatekelezwa. Hali halisi nchini Ukraine haijatengemaa na mazungumzo ya kidiplomasia bado hayajatekelezwa. 

Papa Francisko aomba waamini kusali na kufunga Machi 2 kwa ajili ya Ukraine

Malkia wa Amani ailinde dunia kutokana na wazimu wa vita ndiyo maombi ya dhati ya Papa Francisko mara baada ya Katekesi yake ambapo amewaalika waamini wajitolee kwa pamoja ili katika siku ya kwanza ya Kwaresima kusali na kufunga kwa ajili ya amani barani Ulaya kwa namna ya pekee nchini Ukraine.Papa amesema:"Mungu ni baba wa wote,si mtu tu,anatutaka tuwe ndugu na si maadui."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 23 Februari 2022 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika ukumbi wa Paulo VI, jijini Vatican ameonesha uchungu moyoni kwa ajili ya hali halisi kuongezeka huko Ukraine.  Katika salamu zale, ametoa wito mpana kwa ajili ya amani ambapo hakuweza kuficha wasi wasi wake na kujutia matokeo mabaya ya mazungumzo ya kimataifa ambayo hadi sasa yamefanyika bila kuleta mafanikio. “Licha ya juhudi za kidiplomasia za wiki chache zilizopita hali zinazozidi kutisha zinafunguka. Kama mimi, watu wengi duniani wanakabiliwa na uchungu na wasiwasi. Kwa mara nyingine tena, amani ya kila mtu inatishiwa na maslahi ya upande”. Papa Francisko ameendelea: “Nitoe wito kwa wale wenye majukumu ya kisiasa wachunguze kwa kina dhamiri mbele za Mungu, ambaye ni Mungu wa amani na si wa vita, Baba wa wote, sio tu wa mtu anayetaka tuwe ndugu na si maadui. Ninaomba pande zote zinazohusika zijiepushe na kitendo chochote kinachosababisha mateso zaidi kwa watu, kudhoofisha kuishi pamoja kati ya mataifa na kudharau sheria za kimataifa”.


Waamini wajitoe kusali na kufunga tarehe 2 Machi 2022 , siku ya majivu

Papa Francisko anaelewa wazi kuwa siasa haitoshi kubadili miyo, ni Mungu peke yake ambaye anaweza kufanya hivyo na hivyo amewaaliwa waamini na wasio waamini kuunga katika maombi ya pamoja kwa ajili ya amani. Kwa maana hiyo amesema:  “Yesu alitufundisha kwamba upumbavu wa kishetani wa vurugu unajibiwa kwa silaha za Mungu, kwa maombi na kufunga. Ninawaalika kila mtu kuifanya hiyo tarehe 2 Machi ijayo, ambayo ni Jumatano ya Majivu, ni  siku ya kufunga kwa ajili ya amani. “Ninawatia moyo  hasa waamini kujitolea sana kwa ajili ya maombi na kufunga siku hiyo. Malkia wa Amani alinde ulimwengu dhidi ya wazimu wa vita”, amesisitiza Papa.

23 February 2022, 15:09