Tafuta

Papa Francisko:Mwanzo wa mzunguko wa Katekesi kuhusu thamani ya uzee

Kuna wazee wengi zaidi ya wakati uliopita.Wakati wa janga,wazee wamelipa gharama ya juu zaidi.Papa ametoa onyo dhidi ya udanganyifu wa ujana wa milele na dharau ya zamani ilikuwa picha ya udhalimu.Mwaliko ni kuwa na mazungumzo ya wazee na vijana ambayo ni njia ya kupitisha hekima kwa ubinadamu.Amesisitiza wakati wa Katekesi yake Februari 22,kwa kuanza mzunguko mpya juu ya uzee.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 23 Februari wakati wa katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika ukumbi wa Paulo VI ameanza kusema kuwa “Tumemaliza Katrekesi kuhusu Mtakatifu Yosefu. Leo hii tunaanza na mchakato wa Katekeso ambao unatafuta kuongozwa na Neno la Mungu kuhusu maana na thamani ya uzee. Kwa maana hiyo tufanye tafakari kuhusu uzee”.  Na kumbe Uzee ndiyo kimekuwa kiini cha Katekesi ya siku mara baada ya kusomwa kwa somo kutoka kwa Yoeli 3, 1-2.5 mahali ambapo somo linajikita kuona neema ya wakati na mapatano ya umri wa maisha. Baadhi ya makumi ya miaka hivi, umri wa maisha unatazama ukweli na watu wapya kabisa ambao ni wazee. Haijawahi kutokea namna hii idadi kubwa katika historia ya maisha. Hatari ya kubaguliwa bado inaendelea zadi, ambayo haijawahi kutokea kama sasa. Wazee wanaonekana mara nyingi kama mzigo. Katika hatua ya kwanza ya janga, wao walilipa gharama ya juu zaidi. Walikuwa tayari sehemu ya udhifu zaidi na kuachwa, walikuwa hawatazamwi wakiwa hai, na wala hawakutazamwa wakiwa wanakufa.

Katekesi ya Papa kuhusu Wazee
Katekesi ya Papa kuhusu Wazee

Papa Francisko ameongeza kusema: “Pia, nimepata Hati hii ya haki za wazee na wajibu wa jumuiya: hii imehaririwa na serikali, haijahaririwa na Kanisa, ni jambo la kidunia: ni nzuri, inavutia, ili kujua kwamba wazee wana haki. Itakuwa vyema kuisoma” ameshauri. Pamoja na uhamiaji, uzee ni miongoni mwa masuala ya dharura ambayo familia ya binadamu inaitwa kukabiliana nayo wakati huu. Sio tu mabadiliko ya kiasi; umoja wa zama za maisha uko hatarini: yaani, nukta halisi ya marejeeo ya kuelewa na kuthamini maisha ya mwanadamu kwa ukamilifu wake. Tunajiuliza: je, kuna urafiki, kuna muungano kati ya zama tofauti za maisha au utengano na kukataliwa kunatawala? Sisi sote tunaisha katika wakati uliopo mahali ambapo wanaishi watoto, vijana, watu wazima na wazee. Walakini, uwiano umebadilika: maisha marefu yamekuwa mengi na, katika maeneo makubwa ya ulimwengu, utoto husambazwa kwa dozi ndogo. Tulizungumza juu ya msimu wa (baridi) upungufu wa idadi ya watu, pia.

Ukosefu wa usawa ambao una matokeo mengi. Tamaduni inayotawala ina vijana kama kielelezo cha kipekee, ambayo ni, mtu aliyejitengenezea mwenyewe ambaye hubaki kijana kila wakati. Lakini je, ni kweli kwamba ujana una maana kamili ya maisha, wakati huo uzee unawakilisha tu kubatilishwa na hasara yake?  Papa ameuliza swali hili. Kuinuliwa kwa ujana kama umri pekee unaostahili kujumuisha ukamilifu wa kibinadamu, pamoja na dharau ya uzee inayoonekana kuwa dhaifu, kama uharibifu au ulemavu, ilikuwa ishara kuu ya uimla wa karne ya ishirini. Tumesahau hili? Kurefushwa kwa maisha kuna athari ya kimuundo katika historia ya watu binafsi, familia na jamii. Lakini lazima tujiulize: je, ubora wake wa kiroho na hisia zake za jumuiya ni kitu cha mawazo na upendo vinaendana na ukweli huu? Labda ni lazima wazee waombe msamaha kwa ukaidi wao wa kuishi kwa gharama ya wengine? Au je, wanaweza kuheshimiwa kwa ajili ya zawadi zinazopelekea kwenye maana ya maisha ya kila mtu? Kiukweli, katika uwakilishi wa maana ya maisha na kwa usahihi katika kile kinachoitwa tamaduni zinazoendelea, uzee una athari kidogo.

Katekesi ya Papa kuhusu Wazee
Katekesi ya Papa kuhusu Wazee

Kwa sababu gani? Kwa sababu inachukuliwa kuwa enzi ambayo haina kitu maalum cha kutoa, wala maana yake mwenyewe ya kupata uzoefu. Aidha, kuna ukosefu wa kuhamasishwa na kutiwa moyo na watu kuwatafuta, na kuna ukosefu wa elimu kutokakatika jumuiya ya kuwatambua. Kwa kifupi, Baba Mtakatifu amebainisha kwamba katika  enzi ambayo sasa ni sehemu muhimu ya nafasi ya jumuiya  na inaenea hadi theluthi moja ya maisha yote ya mtu, kuna wakati mwingine mipango ya usaidizi, lakini sio mipango  ya kuwepo. Mipango ya utunzaji, ndiyo; lakini sio mpango wa kuwafanya waishi kikamilifu. Na hii ni utupu wa mawazo, ya kufikirika, ya ubunifu. Chini ya wazo hili, kinachounda utupu ni kwamba wazee ni takataka: katika utamaduni huu wa kutupa, wazee wanaonekana kama takataka.

Ujana ni mzuri, lakini ujana wa milele ni ndoto hatari sana. Kuwa mzee ni muhimu na uzuri  ni muhimu tu kama kuwa kijana. Tukumbuke hilo. Agano kati ya vizazi, ambalo hurejesha enzi zote za maisha kwa wanadamu, ni zawadi yetu iliyopotea na lazima tuirudishe. Ni lazima ipatikane, katika utamaduni huu wa kutupa na katika utamaduni huu wa uzalishaji. Neno la Mungu lina maana kubwa ya kusema hayo kulingana na mapatano hayo. Kama ilivyosemwa unabii wa Yoeli, mwanzoni mwa Katekesi. Wazee wataota ndoto, vijana watakuwa na maono (Yl 2,1). Inawezekana kuutafsi namna hii” ikiwa wazee wataishi kwa Roho kwa kufukia katika kwakati uliopita ndoto zao, vijana hawataweza tena kuona mambo ambayo wanapaswa kufanya ili kufungua wakati ujao.

Katekesi ya Papa kuhusu Wazee
Katekesi ya Papa kuhusu Wazee

Kwa upande mwingine, wazee wanapowasilisha ndoto zao, watoto huona wanachopaswa kufanya. Wavulana ambao hawahoji tena ndoto za wazee, wakilenga vichwa vyao chini kwenye maono ambayo hayaendi zaidi ya pua zao, watajitahidi kubeba sasa yao na kubeba maisha yao ya baadaye. Ikiwa babu na bibi watarudi nyuma kujutia enzi zao, vijana watajikunja zaidi kwenye simu zao za kisasa (smartphone).  Skrini inaweza kubaki inawaka, lakini maisha huisha kabla ya wakati. Je, athari mbaya zaidi ya janga hili sio katika upotezaji mdogo wa vijana? Wazee wana rasilimali za maisha tayari ambazo wanaweza kugeukia wakati wowote. Je, watawatazama vijana ambao wanapoteza maono yao au watawasindikiza kwa kuzipasha joto ndoto zao? Mbele ya ndoto za wazee, vijana watafanya nini? Hekima ya safari ndefu inayosindikiza uzee hadi kuondoka kwao lazima ionekane kama toleo la maana ya maisha, sio kutumiwa kama hali ya kuishi kwake. Uzee, usiporejeshwa kwenye hadhi ya maisha yanayostahili kibinadamu, unakusudiwa kujifunga katika hali ya unyonge inayoondoa upendo kutoka kwa wote. Changamoto hii ya ubinadamu na ustaarabu inahitaji kujitolea kwetu na msaada wa Mungu.

Tumwombe Roho Mtakatifu. Pamoja na katekesi hizi za uzee, Papa ameongeza kusema “ningependa kutia moyo kila mtu kuwekeza mawazo na mapendo juu ya karama ambazo zinaletwa pamoja na zama nyinginezo za maisha. Baba Mtakatifu Francisko akizungumza bila kusoma katkesi yake amependa kufafanua zaidi na kusema tena “Uzee ni zawadi kwa miaka yote ya maisha. Ni zawadi ya ukomavu, ya hekima. Neno la Mungu litatusaidia kutambua maana na thamani ya uzee; Roho Mtakatifu pia atujalie ndoto na maono tunayohitaji. Na ningependa kusisitiza, kama tulivyosikia katika unabii wa Yoeli, hapo mwanzo, kwamba jambo muhimu sio tu kwamba wazee wanachukua nafasi ya hekima aliyonayo, ya historia iliyoishi katika jamii, lakini pia kwamba kuna mahojiano, ambayo yanazungumza na vijana. Vijana wanapaswa kuzungumza na wazee, na wazee kwa vijana. Na daraja hili litakuwa upitishaji wa hekima kwa wanadamu. Ni matu matumaini yake kuwa tafakari hizi zitatufaa sisi sote, ili kuendeleza ukweli huu aliousema nabii Yoeli, kwamba katika mazungumzo kati ya vijana na wazee, wazee wanaweza kutoa ndoto na vijana waweze kuzipokea na kuzipeleka mbele.

Katekesi ya Papa kuhusu Wazee
Katekesi ya Papa kuhusu Wazee

Papa Francisko amebainisha kwamba "Tusisahau kuwa katika tamaduni zote za familia na kijamii, wazee ni kama mizizi ya mti: wana historia yote na vijana ni kama maua na matunda. Ikiwa hakuna juisi na ikiwa matone haya hayatokei kwa namna ya kesema kutoka katika mizizi, hawataweza kuchanua. “Tusisahau kwamba mshairi ambaye nimesema mara nyingi: “Kila kitu ambacho mti unatoa maua hutokana na kile ambacho umezikwa ( ...kile ambacho  mti unatoa maua huishi juu ya kile kilichozikwa, (Francisco Luis Bernárdez). Kila kitu ambacho ni kizuri katika jamii kinahusiana na mizizi ya wazee. Kwa sababu hiyo, katika katekesi hizi, ningependa sura ya wazee iweze kujulikana ili ieleweke vizuri kwamba wazee si kitu cha kupoteza: ni baraka kwa jamii”.

KATEKESI YA PAPA 23 MACHI 2022
23 February 2022, 14:26