Papa:si tendo la kibinadamu na wala kikristo kuharakisha kifo cha wazee
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko katika kuanza tafakari ya katekesi, Jumatano tarehe 9 Februari 2022 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.Katika kuendeleza mada ya Mtakatifu Yosefu amesema:“Katika katekesi iliyopita kwa kwa kuongozwa kwa mara nyingine tena na sura ya Mtakatifu Yosefu tulitafakari maana ya umoja wa watakatifu: na ndiyo kuanzia na hilo ninapenda kutafakari umuhimu pekee wa ibada ambazo watu wakristo wamekuwa nazo daima kwa Mtakatifu Yosefu kama ndiye “Msimamizi wa Kifo Chema”. Akiendelea Baba Mtakatifu amesema hiyo ni ibada iliyozaliwa na wazo ambalo Yosefu alikufa akisaidiwa na Bikira Maria na Yesu kabla ya kuacha nyumba ya Nazareti. Hakuna takwimu za kihistoria, lakini kwa sababu ya kutokuona tena Yosefu katika maisha ya umma, inafikiriwa kuwa alikufa huko Nazareti na familia. Na watu waliomsindikiza walikuwa ni Yesu na Maria.
Vyama vya wakati vya kuombea watu walio katika kufa
Papa Benedikto XV, kwa karne moja iliyopitia aliandika barua yake binafsi kuwa:“kwa njia ya Yosefu sisi tunakwenda moja kwa moja kwa Maria na kwa njia ya Maria, tunaelekea asili ya kila utakatifu na ambaye ni Yesu”. Awe Yosefu na Maria wanatusaidia kwenda kwa Yesu. Papa ameongeza kusema “inatia moyo mazoezi ya ibada kwa heshima ya Mtakatifu Yosefu, na katika maeno hayo alikuwa anashauri moja ambayo alikuwa anasema kwamba “kwa sababu yeye anazingatiwa kuwa anastahili kuwa muafaka wa ulinzi wa wanaokufa, kwa kuwa alitoa pumzi akiwa anasaidiwa na Yosefu na Maria, atakuwa mlinzi wa Wachungaji watakatifu wa kuomba na kuhimiza[...] vyama vya wachaMungu vilivyoanzishwa ili kumwomba Yosefu kwa ajili ya wanaokufa, kama vile vya :“Kifo Chema” , cha “Usafiri wa Mtakatifu Yosefu” na kwa walio katika kufa. (Motu proprio Bonum sane, 25 Julai 1920). Hivyo vilikuwa vyama vya wakati ule, Papa amebainisha.
Katika ufafanuzi wake Papa Fancisko amesema kwamba inawezekana wengine wakafikiri kwamba lugha na mada hiyo ni ya wakati uliopita, lakini kiukweli uhusiano wetu na kifo hautazami kamwe wakati uliopita bali ni wakati uliopo daima. Baba Mtakatifu amegeukia mtangulizi wake kwamba “ Papa Benedikto hivi majuzi akizungumzia juu yake amesema kwamba: “mbele ya mlango wa giza la mauti”. Ni vizuri kumshukuru Papa Benedikto ambaye ana miaka 95 lakini akiwa angavu wa kutueleza jambo hili kwamba: “Mimi ninakabiliwa na giza la mauti, mlango wa giza wa mauti”. Huu ni ushauri mzuri ametupatia!, Papa amesisitiza na kuongeza kusema “ Utamaduni unaoitwa “uzuri” unatafuta kuondoa ukweli wa kifo, lakini kwa kiasi kikubwa janga la virusi vya uviko limeonesha wazi. Ilikuwa mbaya sana: kifo kilikuwa kila mahali, na kaka na dada wengi sana walipoteza wapendwa wao bila kuwa na uwezo wa kuwa karibu nao, na hii ilifanya kifo kuwa kigumu zaidi kukubali na kushughulikia”. Papa Francisko ameongeza kusema: “Muuguzi mmoja aliniambia kuwa bibi mmoja aliye kuwa na uviko wakati anakufa aliambia: “Ningependa kusema kwaheri kwa watu wangu, kabla sijaondoka”. Na muuguzi, kwa ujasiri, alichukua simu na kumuunganisha. Huo ndiyo upole wa kuaga namna hiyo ...”.
Ikiwa hakuna ufufuko kutoka kwa wafu, basi Kristo hakufufuka
Licha ya hilo, lakini tunajaribu kwa kila njia kuondoa mawazo ya ukomo wetu, na hivyo kujidanganya wenyewe kuchukua nguvu zake kutoka katika kifo na kufukuza hofu. Lakini imani ya Kikristo si njia ya kuondoa hofu ya kifo, badala yake inatusaidia kukabiliana nayo. Hivi mapema au baadaye, sote tutakwenda katika mlango huo. Nuru ya kweli inayoangazia fumbo la mauti inatokana na ufufuko wa Kristo. Hapa kuna mwanga. Naye Mtakatifu Paulo anaandika: Sasa, ikiwa inahubiriwa kwamba Kristo amefufuka kutoka kwa wafu, inawezekanaje baadhi yenu kusema kwamba hakuna ufufuko wa wafu? Ikiwa hakuna ufufuko kutoka kwa wafu, basi Kristo hakufufuka! Lakini ikiwa Kristo hakufufuka, basi kuhubiri kwetu ni bure, na imani yenu ni bure” (1Wakorintho 15:12-14). Kuna uhakika mmoja: Kristo amefufuka, Kristo amefufuka, Kristo yu hai kati yetu. Na hii ndiyo nuru inayotungoja nyuma ya mlango huo wa giza la mauti. Baba Mtakatifu Francisko amesema, imani tu katika ufufuko tunaweza kutazama giza la mauti bila kusumbuka na hofu. Na si tu, tunaweza kujikabidhi katika kifo kwa njia chanya. Kiukweli wazo la kifo, likiangazwa na fumbo la Kristo, linatusaidia kutazama kwa macho mapya maisha yote.
Kuna maana gani kubishana na kaka au dada, na rafiki, na jamaa
Kwa mara nyingine tena Papa umerudia kutoa mfano mmoja wa kipindi fulani kwamba: “Sijawahi kuona lori limebeba mizigo linalotembea nyuma ya gari la kubebea maiti! Na hii ina maana kwamba tutakwenda huko peke yetu, bila chochote katika mifuko ya sanda: hakuna chochote. Kwa sababu sanda haina mifuko. Upweke huu wa kifo: ni ukweli, sijawahi kuona gari la kubebea maiti au lori lenye mizigo. Hakuna maana ya kujilimbikizia, ikiwa siku moja tutakufa. Tunachopaswa kukusanya ni upendo, ni uwezo wa kushirikisha, uwezo wa kujali mahitaji ya wengine. Au, kuna maana gani kubishana na kaka au dada, na rafiki, na jamaa, au na kaka au dada katika imani kama siku moja sisi tutakufa? Kuna faida gani kukasirika, kukasirikia wengine? Katika uso wa kifo, maswali mengi yanapunguzwa. Ni vizuri kufa ukiwa umepatanishwa, bila kuacha kinyongo na bila majuto! Papa ameongeza kusema “Ningependa kusema ukweli mmoja: sote tuko njiani kuelekea kwenye mlango huo, kila mtu”. Injili inatuambia kwamba kifo huja kama mwizi, hivyo Yesu anasema: huja kama mwizi, na kwa kadiri tunavyojaribu kudhibiti ujio wake, labda kwa kupanga kifo chetu wenyewe, inabaki kuwa tukio ambalo lazima tushughulike nall na mbele yake ya kufanya uchaguzi.
Ni lazima kusindikiza kufikia kifo, lakini sio kusababisha kifo
Mambo mawili kwa ajili yetu sisi Wakristo yanabaki yamesimama. Lakwanza: hatuwezi kukwepa kifo, na kwa sababu hiyo, baada ya kufanya kila liwezekanalo kibinadamu kumponya mgonjwa, kuendelea katika matibabu kwa nguvu ni kinyume cha maadili (taz. Katekisimu ya Kanisa Katoliki, n. 2278). Maneno hayo ya watu waamini wa Mungu, ya watu rahisi: “mwache afe kwa amani, “msaidie afe kwa amani”, ni ya hekima kiasi gani! Papa ameongeza kusema. Jambo la pili la kuzingatia linahusu ubora wa kifo chenyewe, ubora wa maumivu, wa mateso. Kiukweli, tunapaswa kushukuru kwa msaada wote ambao dawa inajaribu kutoa, kwa kupitia kile kinachoitwa huduma shufaa”, kila mtu ambaye anajiandaa kuishi sehemu ya mwisho ya maisha yake, anaweza kuifanya kwa kiasi kikubwa, ni njia sahihi na iwezekanayo ya kibinadamu. Hata hivyo, ni lazima tuwe waangalifu ili tusichanganye usaidizi huu na mielekeo isiyokubalika na inayosababisha kuua. Ni lazima kusindikiza kufikia kifo, lakini sio kusababisha kifo au kusaidia aina yoyote ya kujiua. Nakumbuka kwamba haki ya kutunza na kutunza wote lazima iwe na upendeleo siku zote, ili walio dhaifu zaidi, hasa wazee na wagonjwa, wasitupwe kamwe. Maisha ni haki, si kifo, ambayo lazima kukubaliwa, na kamwe si kusimamiwa. Na kanuni hiyo ya kimaadili inahusu kila mtu, si Wakristo au waamini pekee yake.
Kuna tabaka fulani la kijamii linaloharakisha kifo cha wazee
Papa Francisko amesema “Lakini ningependa kutaja hapa tatizo la kijamii, lakini la kweli. Sijui kama hiyo “mipango” ni neno sahihi, lakini kuharakisha kifo cha wazee. Mara nyingi sana inaonekana katika tabaka fulani la kijamii kwamba wazee, kwa sababu hawana uwezo, wanapewa dawa kidogo kuliko wangehitaji, na huu ni unyama: hii sio kuwasaidia, hii inawasukuma haraka katika kifo zaidi. Na hiyo si tendo la mwandamu na wala la Mkristo. Wazee lazima wachukuliwe kama hazina ya ubinadamu: wao ni hekima yetu. Hata kama hawasemi, na ikiwa hawana maana, ni ishara ya hekima ya kibinadamu. Hao ndio waliotangulia mbele yetu na kutuachia mambo mengi mazuri, kumbukumbu nyingi, hekima nyingi. Tafadhali usiwatenge wazee, usiharakishe kifo cha wazee. Kumbembeleza mtu mzee kuna tumaini sawa na kubembeleza mtoto, kwa sababu mwanzo wa maisha na mwisho daima ni fumbo, fumbo ambalo lazima liheshimiwe, lisindikizwe, litunzwe na kupendwa.
Mama yetu Maria awe nasi katika saa ya kufa kwetu
Mtakatifu Yosefu atusaidie kuliishi fumbo la kifo kwa namna bora kabisa iwezekanavyo. Kwa Mkristo, kifo kizuri ni uzoefu wa huruma ya Mungu, ambayo hutukaribia hata katika dakika hiyo ya mwisho ya maisha yetu. Hata katika sala ya Salamu Maria, tunaomba Mama Yetu awe karibu nasi na saa ya kufa kwetu”. Kwa sababu hiyo amependa kuhitimisha katekesi hiyo kwa kusali pamoja kwa Mama Yetu kwa ajili ya wanaofariki, kwa wale wanaopitia wakati huu wa kupita kwenye mlango wa giza, na kwa ajili ya wanafamilia wanaopatwa na maombolezo.