Mantiki ya zamani na ndoto mpya ya amani
Na Andre Tornielli.
“Katika usiku wa vita vilivyowaangukia wanadamu, tafadhali, tusiruhusu ndoto ya amani ipotee”. Papa Francisko pia huko Malta amezungumza juu ya kile kinachotokea katikati ya Ulaya. Ameomba kwamba: “tafadhali isiruhusiwe kuzima ndoto ya amani, tumaini la amani". Amezungumza, akirejea Giorgio La Pira, kuhusu “uchokozi wa kitoto na uharibifu ambao unatutishia”, na juu ya hatari ya “vita baridi vilivyopanuliwa” ambavyo vinaweza kudhoofisha maisha ya “watu wote na vizazi”. Sio tu kati ya wale wanaoishi katika ardhi yetu leo hii, lakini pia wale ambao watakuja baada yetu.
Kwa mara nyingine tena, ingawa wengi wangetumani Papa “abariki” vita au angalau kupunguza maneno yake kwa wale wasiopenda kusikai dhidi ya mbio za kununua silaha tena ambazo zinaonekana kuwa za dharura na haziwezi kuahirishwa, Papa Francisko ametoa maneno ya kusikitisha. Maneno ambayo hayatumiki, au yanayoweza kupunguzwa kwa kurahisisha utumaji. Papa amesema kwa uwazi kwamba hali kama ya watoto inajitokeza tena katika “ushawishi wa utawala wa kiimla, katika ubeberu mpya, katika uchokozi ulioenea, katika kutokuwa na uwezo wa kujenga madaraja na kuanza kutoka kwa maskini zaidi”. Anatambua jinsi leo hii ni vigumu kufikiria kwa mantiki ya amani kwa sababu “tumezoea kufikiri mantiki ya vita”.
Baadaye Papa amezungumza juu ya “upepo wa baridi sana wa vita, ambavyo“wakati huu pia umechochewa kwa miaka mingi”. Tena wakati huu, hiyo ni kama ilivyokuwa katika siku za nyuma ambazo tumesahau lakini ambazo wazazi wetu au babu na bibi zetu wamejua, vita vya kidugu huko Ulaya ambavyo vimeibuka na kuwa mizozo ya ulimwengu. Kwa mara nyingine tena, kama ilivyokuwa nyakati za hivi karibuni zaidi, wakati vita ilionekana kuwa mbali na sisi imeendelea na kuua mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia na kusababisha mamilioni ya wakimbizi.
Ndiyo, Papa Francisko amerudia kwa uhakika kusema kwamba: vita havikuzuka ghafla lakini vimekuwa vikiandaliwa kwa muda. Kwa namna gani? “Pamoja na uwekezaji mkubwa na biashara ya silaha”. Kwa sababu hiyo Mfuasi wa Mtume Petro amefafanua mbio za silaha kuwa ni wazimu, kwa sababu hiyo anatualika tuingie katika mantiki tofauti, mpya, mantiki ya amani na amani isiyojengwa juu ya woga na kuzuia, bali juu ya haki, mazungumzo, juu ya mfumo mpya wa mahusiano ya kimataifa. Inasikitisha kuona jinsi gani shauku ya amani, iliyoibuka baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ilivyofifia katika miongo ya hivi karibuni.
Kwa hiyo, pamoja na amani, masuala mengine mengi makuu, kama vile vita dhidi ya njaa, umaskini na ukosefu wa usawa, kwa hakika“yameainishwa” kutoka katika ajenda kuu za kisiasa. Kutokana na hiyo, ndipo kuna wito ambao Papa Fransisko amezindua huko Malta kwamba: “Tusaidiane kusikiliza kiu ya watu ya amani, tufanye kazi ya kuweka misingi ya mazungumzo mapana zaidi, turudi kukusanyika katika mikutano ya kimataifa kwa ajili ya amani, mahali ambapo mada ya upokonyaji silaha, inakuwa kiini kwa mtazamo wa vizazi vijavyo! Na fedha kubwa zinazoendelea kutengwa kwa ajili ya silaha zinapaswa kubadilishwa kuwa maendeleo, afya na lishe”.