Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:uchokozi wa kitoto wa mtu fulani mwenye nguvu hautakiwi!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amefika kisiwani Malta ikiwa ni hija yake ya kitume ya Siku mbili Jumamosi na Jumapili 2 na 3 Aprili 2022 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida.” (Mdo 28: 2). Mara baada ya kufika uwanja wa ndege wa kimatafaifa na kupokelewa kwa afla kuu, alifanya hotuba yake ya kwanza kwa viongozi wa Serikali, wanadiplomasia pamoja na viongozi wa asasi zisizo za Kiserikali na wa ulimwengu wa utamaduni huko La Valletta. Hata hivyo kabla ya kuondoka katika Nyumba ya Mtakatifu Malta mjini Vatican, Papa amewasalimia baadhi ya familia za wakimbizi kutoka Ukraine na kuelekea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa "Leonardo Da Vinci" Roma Fiumicino. Akiwa kwenye ndege kabla ya kuacha eneo la Italia, Papa Francisko ametuma talegramu kama utamaduni wa kila ziara ya kwenda nje ya nchi kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella, ambapo amebainisha "furaha ya kukutana na ndugu wa imani katika Nchi angavu yenye uzuri sana katikati ya Bahari ya Mediteranea, vilevie Bandari salama kwa milenia ya wasafiri wa kufika na kuondoka". Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amemtumia “kiongozi wa nchi na watu wote wa Italia matashi mema, utulivu na amani". Vile vile Baba Mtakatifu kama kawaida yake kabla ya kuanza safari yoyote ile ya kimataifa, ameikabidhi kwa Mama Maria Afya ya warumi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma.
Akianza hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko amewasalimu na kushukuru Rais wa nchi kwa maneno yake aliyomwelekea kwa niaba ya wazalendo wote. Mababu wao waliweza kutoa ukarimu kwa Mtume Paulo wakati anaelekea Roma, kwa ukarimu huo akiwa na wenzake katika safari ambayo ni ya kibinadamu ( Mdo 28,2. Kwa maana hiyo Papa amesema akiwa anatoka Roma amefanya uzoefu wa joto la ukarimu la watu wa Malta ambayo kwa kizazi na kizazi imeweza kurithisha ukarimu huo. Katika nafasi, hiyo Malta inaweza kufafanulia kama Moyo wa Mediteranea, kakini si tu kwa ajili ya nafasi, msukano wa matukio ya kihistoria na mkutano wa watu ambao kwa milenia ya visiwa hivyo imekuwa kitovu cha maisha na utamaduni, cha kitasaufi na uzuri, mikatisho ambayo ilitambua kukarimu na kuelewa wimbi la wengi kutoka sehemu mbali mbali. Utofauti huo unafanya kufika upepo mwingi wenye tabia ya nchi hiyo. Si kwa bahati mbaya, katika uwakilishi wa ramani ya kizamani ya Mediteranea ilikuwa inaonesha rangi ya pinki na ambayo mara nyingi ilikuwa inatawala na kukaribia na kisiwa cha Malta. Kwa maana hiyo Papa ameomba aweze kutumia sura hiyo ya upepo wa pinki ambao nafasi ya upepo huo au dira hiyo ni misingi ya ncha nne kuu, zinazoelezea wimbi msingi wa maisha ya kijamii na kisiasa katika nchi hiyo.
Baba Mtakaifu amesema mara nyingi ni upepo kutoka Kaskazini magharibi ambao upuliza katika Kisiwa cha Malta. Kaskazini inakumbusha Ulaya kwa namna ya pekee nyumba ya Umoja wa Ulaya, iliyojengwa kwa sababu waweza kuishi familia kubwa iliyoungana kulinda amani. Umoja na amani ni zawadi ambazo watu wa Malta wanaomba kwa Mungu kila mara wanapoimba wimbo wao wa taifa. Sala iliyoandikwa na Dun Karm Psaila inasema hivi: “Mungu Mwenyezi umpatie hekima na huruma kwa yule anayeongoza, afya kwa anayefanya kazi na kuhakikisha watu wa Malta umoja na amani”. Amani inafuata umoja na kububujika ndani mwake. Hii inaangazia umuhimu wa kufanya kazi pamoja , wa kukataa kila aina ya migawanyiko, kuimarisha mizizi na thamani shirikishi ambazo zinatokana na umoja wa jamii ya Malta, Papa Francisko amesisitiza. Lakini ili kuhakikisha namna njema ya kuishi kijamii, haitoshi kuimarisha maana njema ya uwepo, bali inahitaji kuongeza nguvu msingi wa kuishi pamoja ambao unakita juu ya haki na juu ya sheria. Uaminifu, haki na maana ya uwajibikaji na uwezo ni nguzo msingi wa jamii ya kizalendo iliyoendelea. Jitihada za kuondoa uhalifu na ufisadi iwe na nguvu kama upepo ambao unavuma kutoka kaskazini na kusafisha fukwe za Nchi. Na iwe daima ni kukuza sheria na uwazi ambao unaruhusu kuondoa mabaya na uhalifu ambao umejikusanya pamoja kutokana na kutokubali mwanga wa jua.
Nyumba ya ulaya ambayo inajitahidi katika kuhamasisha thamani ya haki na usawa kijamii, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba iko pia mstari wa mbele kwa ajili ya ulinzi mpana zaidi wa nyumba ya muumbaji. Mazingira ambamo tunaishi ni zawadi kutoka mbinguni, kama ilivyo hata katika wimbo wa Taifa unaoomba Mungu atazame uzuri wa ardhi hiyo, mama aliyevikwa mwanga wa juu zaidi. Ni kweli Baba Mtakatifu Francisko amekiri kwamba Malta mahali ambapo ni angavu sehemu zake zinaleta faraja katika matatizo, kazi ya uumbaji inajionesha kama zawadi ambayo katikati ya majaribu ya historia ya maisha, inakumbusha uzuri wa kuishi katika Nchi. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anaomba kwamba nchi hiyo ilindwe dhidi ya uchu,na kupenda fedha, ujenzi usio halali ambao haustahili katika maeneo, bali kutazamia wakati ujao. Kwa maana hiyo wanapaswa kulinda mazingira na haki kijamii kwa ajili ya kujiandalia wakati ujao na ndiyo njiamuafaka wa kuwafanya vijana wapende siasa nzuri, kwa kuwaondoa dhidi ya vishawishi vya kutokujali na kutotia bidii. Baba Mtakatifu Francisko amesema Upepo wa Kaskazini mara nyingi unachanganyika na ule wa Magharibi. Nchi hiyo ya Ulaya kwa namna ya pekee katika ujana wake inashirikishana kiukweli na mitindo ya maisha na wazo la Magharibi. Kutokana na hiyo ndipo kuna mali kubwa, akifikiria thamani za uhuru na demokrazia, lakini pia hatari ambayo lazima kuzingatia na kuwa makini kwa sababu kuna kurudisha maendeleo ambayo hapayalekei kuondoa mzizi. Malta kwa maana hiyo ni ya kushangaza, “maabara ya maendeleo ya pamoja, mahali ambapo kusema maendeleo haina maana ya kukata mizizi ya wakati uliopita kwa matarajio ya uongofu wa kutaka faida, ya mahitaji yaliyokita juu ya kutumia hivyo, zaidi ambayo ni kutoka kasumba za kutaka kuwa haki ya kila kitu. Kwa kuwa na maendeleo safi ni muhimu kulinda kumbu kumbu na kusuka heshima katika maelewano kati ya vizazi bila kuachwa kunyweshwa na kile cha ufafanisho wa kijujuu na kutoka katika ukoloni wa kiitikadi ambazo mara nyingi kwa mfano katika uwanja wa maisha, wa msingi wa maisha. Ni ukoloni wa itikadi ambazo zikawnda kinyume na haki kwa maisha tangu kutungwa kwake au kabla ya kutungwa.
Vijana wanahitaji kulindwa uzuri wao dhidi ya madawa ya kulevya
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa chini ya msingi wa ukuaji thabiti kuna mtu binadamu, heshima ya maisha na hadhi ya kila mwanaume na kila mwanamke. Baba Mtakatifu amebainisha anavyojua vema jitihada za Wamalta katika kukumbatia na kulinda maisha. Tayari katika Matendo ya Mitume, walikuwa wanawatambua kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewatia moyo wa kuendelea kupenda maisha tangu kutungwa kwake hadi mwisho wa kawaida, lakini pia kuyalinda kwa kila wakati dhidi ya ubaguzi na kuachwa pekee. Papa amefikiria hasa hadhi ya wafanyakazi, wazee na wagonjwa. Na vijana ambao wako hatari ya kuachwa njiani na mabo ni wema mkuu ambao mara nyingi wanaachwa na kubaki na utupu ndani mwao binaasi. Na kile ambacho kinasababishwa kutumia hovyo, kujifungia ndani binafasi na wengine ni janga la madawa ya kulevya ambayo yanawasonga na kutaka uhuru wa kutumia. Papa ameomba kulindwa uzuri huo wa maisha. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kutazama upepo huo amejikia na Kusini. Papa amesema kutoka kusini wanafika kaka na dada wengi wanaotafua matumaini. Papa Francisko amependa kushukuru Mamlaka na watu kwa ukarimu wao ambao wanatenda kwa jina la Injili, la ubinadamu na kwa maana ya ukarimu asili wa watu wa Malta. Kwa mujibu wa asili ya neno, Malta maana yake ni “Bandari salama”. Lakini pamoja na hayo mbele ya ukuaji wa wimbi la miaka ya mwisho, hofu na ukosefu wa usalama umesababaisha kukata tamaa na usumbufu. Baba Mtakatifu amesisitiza juu ya kukabiliana na ugumu wa masuala ya uhamiaji, kuingia kwa ndani ya mahitaji mapana na ya muda mrefu na nafasi. Kwa muda sasa mbele ya uhamiaji si tu wa wakati huu lakini wa nyakati zote unapelekea madeni ya ukosefu wa haki zilizopita, unyonyaji mkubwa, wa mabadiliko ya tabianchi, matatizo ya migogoro ambayo wao wanalipa matokoe yake. Kutoka Kusini maskini na imekuwa na watu wengi ambao wanaondoka kuelekea Kaskazini iliyo tajiri zaidi; ukweli, ambao hauwezi kukataliwa na kufungwa kwa habari za kugushi kwa sababu hakutakuwa na ustawi na ushirikiano kwa kutengwa. Kuna haja ya kuzingatia tena nafai. Kuongezeka kwa dharura ya uhamiaji, kwa mfano kufikiria uhamiaji kutoka Ukraine, ambao unahitaji majibu makubwa na shirikishi.
Badhi ya nchi haziwezi kwenda juu ya matatizo na kubaki na sintofahamu
Papa amesema baadhi ya Nchi nyingine haziwezi kwenda juu ya matatizo yote na kubaki na sinfofahamu ya nyingine. Na nchi zilizostaarabika haziwezi kuanzisha, kwa ajili ya maslahi yao wenyewe, mikataba isiyoeleweka na wahalifu wanaowafanya watu kuwa watumwa. Mediteranea inahitaji uwajibikaji wa kila hali ili kugeuka kwa upya tamasha la mshikamano na siyo kwenda kinyume na janga la manusura wa ustaarabu. Papa Francisko kwa kutazama juu ya manusura, amemfikiria Mtakatifu Paulo ambaye katika mchakato wake wa mwisho wa kukatisha Mediteranee alifika katika fukwe hizo kwa namna isiyotarajiwa na kuokolewa. Na baadaye katika tukio la kuzongwa zongwa na nyoka, mkononi Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi. Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu(rej. Mdo,3-6). Papa amesema katika kuzidisha hayo, mambo mawili msingi yalikuwa yanawakosa. Paulo alikuwa mtu mwenye kuhitaji ukarimu. Ubinadamu unakuja awali ya yote na kushia kila kitu. Ulimfundisha Nchi hiyo ambayo Historia yake iliweza kumsaidia aliyekuwa anataabika baada ya kufika kwa mtume huyo mnusura. Kwa jina la Injili ambayo Yeye aliishi aliwahubiri kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu ameomba wapanue mioyo na wagundue uzuri wa kuhudumia wenye kuhitaji. Wakati leo hii mbele ya wale wanaokatisha Mediteranea ili kutafuta wokovu wanakumbwa na wasi wasi na kuelezwa kama wavamizi, Papa ameomba wawasaidie ili wasione wahamiaji kama hatari na wala kuamini vishawishi vya kuamsha vizingiti na kujenga kuta.
Baba Mtakatifu amefafanua juu ya virusi vya kujilinda lakini mtu wa kukarimu na wazo la Kikristo linaalika daima kushinda shuku, kutoaminiana, hofu ya kivamiwa na tabia za kujilinda ambazo ulimwengu wa sasa unatuweka(rej. Wosia wa kitume Evangelii gaudium 88). Papa Francisko amesema wasiache sintofahamu zizime ndoto ya kuishi pamoja. Ndiyo kukaribisha kunagharimu na kunahitaji kujitoa. Hata Mtakatifu Paulo alikuwa hivyo, ili kuweza kuokoka alikuwa mstari wa mbele kusalimisha mali katika Meli (Mdo 27, 38). Lakini ni kujikita kutafuta kwa ajili ya wema mkubwa, wa maisha ya mtu ambaye ni tunu ya Mungu. Hatimaye Papa amesema kuna upepo utokao Mashariki, ambao mara nyingi hupuliza asubuhi. Mwandishi Omero aliuta upepo huo ‘Eur’ (Rej Odissea V,379.423). Kwa hakika ni kutoka Mashariki mwa Ulaya, kutoka huko Mashariki mahali panachomoza mwanga wa kwanza wa jua, kumetokea giza la vita. Papa mesema wafikirie uvamizi wa Nchi nyingine, mapigano makali katika barabara na tishio la atomiki labda ni kumbukumbu za giza nene na chuki ambazo zina wenye nguvu katika maisha ya wengi na juu ya siku za wote . Na ingawa kwa mara nyingine tena baadhi ya watu wenye nguvu, waliofungiwa kwa masikitiko katika madai yasiyolingana ya maslahi ya utaifa, uchochezi na kuchochea migogoro, watu wa kawaida wanahisi hitaji la kujenga mustakabali ambao utakuwa pamoja au hautakuwa. Sasa katika usiku wa vita vilivyoshuka juu ya ubinadamu, Papa ameomba wasikate tamaa ya kuota ndoto ya amani.
Malta ni chemi chemi ya kutoa uzuri kwa upya
Baba Mtakatifu amesema kuwa Malta ambayo inang’aa kwa mwanga kutoka katika moyo wa Mediteranea, unaweza kuwaasha, kwa sababu ni chemi chemi ya kutoa kwa upya uzuri wa uso wa mtu, aliyebadilishwa na vita. Uzuri wa picha ya Meditaranea ya karne ya kwanza ya Kikristo inaonesha amani, Irene kama mwanamke ambaye alikuwa kweye mikono ya Pluto, ni utajiri. Yeye anakumbusha kuwa amani inazaa uzuri na vita ni umaskini tu. Hii inafanya kufikiria kwamba picha ya amani na utajiri ni vitu ambavyo vinaonesha kama mama ambao wanashika mtoto katika mikono yao. Upole wa mama wengi ambao wanatoa maisha ulimwenguni na uwepo wa mama wengi ambao badala yake kuna ukweli wa mantiki ya kurarua na madaraka, ambayo yanaleta vita. Tubahitaji huruma na utunzaji na sio maono ya kiitikadi na utaifa ambayo yanamwilisha maneno ya chuki badala ya kuwa na moyo wa maisha ya dhati ya watu wa kawaida. Baba Mtakaifu Francisko amekumbuka Meya wa Mji wa Firenze Nchini Italia, Giorgio La Pira aliyesema kuwa: “Hali ya kihistoria tunayopitia, mgongano wa masilahi na itikadi ambazo hutikisa ubinadamu katika lindi la utoto wa ajabu, inarudisha Mediterania jukumu kuu: kufafanua tena kanuni za Kipimo ambapo mwanadamu ameachwa kwenye mtafaruku na kutoweza kupimika inaweza kutambuliwa” (Hotubakatika Mkutano wa Utamaduni wa Mediterania, Februari 19, 1960). Maneno hayo ni ya sasa Papa amesisistiza na kwamba yanahitajika kupima ubinadamu, mbele ya fujo za kitoto na uharibifu ambazo zinatishia mbele ya hatari za vita vya baridi vilivyoenea na ambavyo vinaweza kusonga maisha yote ya watu na kizazi.
Kwa bahati mbaya utoto haujatoweka
Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kwa bahati mbaya, utoto huo haujatoweka. Unajitokeza tena kwa wingi katika shauku ya utawala wa kiimla, katika ubeberu mpya, katika uchokozi ulioenea, katika kutoweza kujenga madaraja na kuwaacha maskini zaidi. Kutoka hapa upepo wa vita wa baridi sana huanza kuvuma, ambao kwa mara nyingine tena umechochewa zaidi ya miaka. "Ndio, vita vimekuwa vikijiandaa kwa muda na uwekezaji mkubwa na mikataba ya silaha. Na inasikitisha kuona jinsi shauku ya amani, iliyoibuka baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ilivyofifia katika miongo ya hivi karibuni, kama vile njia ya jumuiya ya kimataifa, ikiwa na watu wachache wenye nguvu ambao wanasonga mbele wenyewe, kuitafuta, na kanda za ushawishi. Na hivyo sio tu amani, lakini masuala mengi makubwa, kama vile vita dhidi ya njaa na ukosefu wa usawa, yameondolewa katika ajenda kuu za kisiasa. Lakini suluhisho la mizozo ya kila mtu ni kutunzana kila mtu, kwa sababu matatizo ya kimataifa yanahitaji ufumbuzi wa kimataifa. Tusaidiane kusikiliza kiu ya wananchi ya kutaka amani, tufanye kazi ya kuweka misingi ya majadiliano mapana zaidi, turudi kukutana katika mikutano ya kimataifa ya amani, ambapo kaulimbiu ya upokonyaji silaha ni kiini, kwa jicho la vizazi vijavyo! Na fedha kubwa zinazoendelea kwenda kwa silaha zinabadilishwa kuwa maendeleo, afya na lishe”. Papa Francisko ametazama mashariki tena na kutoa wazo la mwisho karibu na nchi za Mashariki mbazo zinatafakari kwa lugha ya watu hao , ambapo ni maelewano na wengine na kukumbusha karibu uwezo wa watu wa Malta ambao wamejaliwa kuishi vema kati ya tofauti. Papa amesema kutoka hapo kuna haja ya Nchi za Mashariki: Lebanon, Siria, Yemen na nchi nyingine zenye muktadha wa kuongezeka kwa matatizo na vizingiti. Malta katika moyo wa meditaranee, inaendelea kuwa shemu ya macho ya matumaini, utunzaji wa maisha, ukarimu wa mwingine, dhima ya amani na kwa msaada wa Mungu ambaye jina ni amani. Mungu abariki Malta na Gozo, amehitimisha hotuba yake ya kwanza.