Matarajio ya Papa kuwa makubaliano ya muda na China yapyaishwe
VATICAN NEWS
Papa Francisko amethibitisha kuwa Mkataba wa muda wa makubaliano kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China unendelea vizuri na matumaini yake kwamba unaweza kupyaishwa mwezi Oktoba ujayo. Hayo ndiyo amethibitisha wakati wa mahojiano na Shirika la Habari la Reuters, na mwandishi wake Phil Pullella. Kama inavyokumbukwa, shukrani kwa Mkataba wa Muda wa Makubalinao uliotiwa saini mnamo 2018, ambapo maandishi kwa sasa yamehifadhiwa, umewezesha kuleta unafuu wa hali mbali mbali za Kanisa Katoliki nchini China kwa kupelekea muungano kamili na Roma na maaskofu walioteuliwa bila agizo la kipapa.
Makubaliano hayo yanatazamia mchakato wa kushirikisha ili kufikia uteuzi wa maaskofu wapya, ambao kwa sasa mwenye neno la mwisho ni Papa. Kama matokeo yaliyoandakwa na mwandishi wa mahojihano na Papa Francisko ametetea Kardinali Parolin ambaye ni mwanadiplomasia muhimu wa Vatican, na kwamba ni mwanaume wa ngazi ya juu ya kidiplomasia.
Papa alisema anajua jinsi ya kufanya michakato, “yeye ni mtu wa mazungumzo, na amezungumza na mamlaka ya China. Ninaamini kuwa tume anayoiongoza imefanya kila kitu kuendelea na kutafuta njia ya kutokea na wameipata”. Kwa hiyo Papa Fransisko alitetea sera ya hatua ndogo, kwamba uvumilivu ambao alikuwa akizungumzuia Kardinali Agostino Casaroli, kuelekea nchi za Ulaya ya Mashariki, wakati huo katika kambi ya Kisovietiki, kwamba: “Wengi wamesema mambo mengi dhidi ya Papa Yohane wa XXIII, dhidi ya Paulo VI, dhidi ya Casaroli”, Papa alieleza na kuongeza kuwa, “lakini hivyo ndivyo diplomasia ilivyo. Mbele ya hali iliyofungwa, lazima tutafute njia inayowezekana, sio wazo, diplomasia ni sanaa ya iwezekanavyo na kufanya iwezekanavyo kuwa kweli. Vatican daima imekuwa na watu hawa wakuu. Lakini suala la Nchi ya China analipekea mbele Kardinali Parolin ambaye kwa namna hiyo anafanya vizuri sana”.
Akilinganisha hali ya sasa na ile ya kabla ya 1989, Papa Francisko alisema uteuzi wa maaskofu nchini China tangu 2018 umeendelea polepole, lakini kuna matokeo mema. “Unakwenda polepole, lakini maaskofu wameteuliwa”. Mchakato unakwenda polepole, kama ninavyosema, 'mtindo wa Kichina', kwa sababu Wachina wana hisia ya wakati kwamba hakuna mtu anayewaharakisha. Wao pia wana matatizo, aliongeza akimaanisha mitazamo tofauti ya mamlaka mahalia ya nchini China, kwa sababu hali si sawa katika kila eneo la nchi. “Kwa sababu ya njia ya kudumisha mahusiano na Kanisa Katoliki, pia inategemea watawala, wapo baadhi. Japokuwa makubaliano ni sawa na ninatumaini yanaweza kufanywa kwa upya mnamo Oktoba”.