Mwaliko wa Papa kwa maaskofu wapya:wawe wachungaji karibu na maskini
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Ulikuwa ni mkutano wa kawaida kwa wote kukaa pamoja katika mduara ambao ulijikita katika shuhuda, ushauri na kutia moyo ili kuhudumia maskini zaidi. Katika siku zilizofuata za kujifunza jinsi ya kuwa maaskofu, changamoto gani za kukabiliana nazo, ni mada gani za kupeleka mbele. Maaskofu wapya wapatao 200 walioshiriki katika kozi ya malezi iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na kwa Makanisa ya Mashariki ambao walipokelewa asubuhi ya tarehe 19 Septemba 2022 na Baba Mtakatifu Francisko katika Ukumbi wa Clementine mjini Vatican. Mkutano huo, ambao Kardinali Marc Ouellet Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu alikuwepo, ulihifadhiwa ili kuruhusu mazungumzo huru kati ya Papa na maaskofu (wengi wao kutoka Amerika ya Kusini), katika muktadha huo wale walioshiriki katika hatua ya pili ya kozi, iliyofanyika tangu 12-19 Septemba katika Taasisi ya Ateneo Regina Apostolorum huko Roma.
Hatua ya kwanza iliyofunguliwa na Misa iliyoadhimishwa na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, ilifanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Septemba 2022 iliyopita (mgawanyiko uliundwa kwa idadi kubwa ya washiriki kutokana na vikwazo vya Uviko). Papa Fransisko alikuwa amepokea washiriki katika kozi hiyo katika Chumba cha Clementine ya utamaduni ulioanza mnamo mwaka 2000 chini ya upapa wa Yohane Paulo II na kuendelea kufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu mada ilikuwa ni: "Kutangaza Injili katika mabadiliko ya zama na baada ya janga: huduma ya askofu”
Hata katika hali hiyo hapakuwa na hotuba iliyoandikwa, lakini yalikuwa ni mazungumzo ya faragha kwani askofu msaidizi,Angelo Ademir Mezzari, wa Mtakatifu Paulo aliripoti katika ofisi ya uhariri kwa lugha ya Kireno. Kwa upande wake alisema kwamba Baba Mtakatifu, aliwakaribisha wale waliohudhuria kwa ujumbe, yaani, bila kusahau ukaribu na maskini, akifahamu kwamba kila kitu kimeunganishwa na kila kitu kinahitaji huduma katika sayari hii. Kisha alitaka kuwasikiliza wageni wake moja kwa moja, hisotria zao, maoni yao na maombi yao. Mkutadha huo ulidumu kama saa moja na nusu. Mpango huo huo ulirudiwa tena katika mazingira ya "kisinodi", kama ilivyotangazwa na askofu wa Brazil Maurício da Silva Jardim ambaye tarehe 23 Oktoba atakabidhwa jimbo la Rondonópolis-Guiratinga.
Kwa mujibu wake alisema kukaa kisinodi ndiyo ilikuwa hali ya juma la kazi katika Taasisi ya Regina Apostolorum, ambapo, kwa nuru ya uadilifu wa Papa Francisko, wasemaji waliweka mada katikati na kutoa nafasi katola mkutano, kujieleza, na kuibua maswali na matatizo madhubuti ya ukweli, kama vile njaa, vurugu, ukosefu wa usawa wa kijamii, uhamiaji, migogoro ya kisiasa na kiafya, maadili na masuala ya kijamii duniani kote" Maaskofu wapya 19 wa Brazil waliweza kuwafahamisha washiriki wa kozi hiyo na Papa, hata matatizo makubwa ambayo yanaharibu uso wa Amazonia, kama vile uchimbaji madini, unyonyaji, ukataji miti ovyo.
Wakati wa kozi hiyo, maandishi ya Papa Francisko yakaririwa kwa kina hasa Wosi wa Amoris laetitia, Fratelli tutti na Laudato si ', na baadhi ya mambo muhimu ya upapa wa Jorge Mario Bergoglio kama vile familia na udugu wa ulimwengu mzima kupitia uhamasishaji wa binafamu fungamani,. Ilikuwa ni fursa ya kutembea pamoja katika nyanja tofauti, kututia moyo kuwa 'wachungaji wa watu' na kutoa vipengele vya kutenda katika majimbo yetu, kwa kanuni iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko wa kimisionari, Kanisa la Sinodi, umoja na ushiriki”. Kundi jingine la Maaskofu lilipokelewa katika Mkutano wa Jumamosi iliyopita tarehe 17 Septemba na kwamba wachungaji wa nchi za kimisionari walioshiriki katika semina nyingine ya malezi jijini Roma, iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Katika mazungumzo ya wazi, na ya faragha, aliwahimiza maaskofu kuona ukaribu wa wachungaji, kwanza kabisa na Mungu, kisha ushirika kati ya maaskofu na mapadre, bila kuwasahau waamini.
Kama ilivyoripotiwa kwa wenzao katika ofisi ya uhariri ya lugha ya Kihispania na Msimamizi wa Kitume wa Caroní huko Venezuela, Askofu Gonzalo Ontiveros, maaskofu walipata fursa ya kushiriki uzoefu wao wa kazi ya kimisionari na Papa, hivyo kumpa Baba Mtakatifu mwanzo wa kutafakari yake. Kwa upande wa Papa Francisko alisisitiza umuhimu wa maombi katika huduma ya kiaskofu kwa sababu askofu asipoomba, anamwacha Mungu na hunyauka. Pia, alisema Ontiveros, kwamba Papa alitaka umoja zaidi kati ya maaskofu kama ndugu katika uaskofu na ukaribu wa karibu na mapadre, washiriki, jumuiya za parokia kwa uwajibu kwa wote. Kuwa waangalifu kwa mahitaji yao. Miongoni mwa mapendekezo hayo, yapo pia ya kujiepusha na mbwembwe za kimbembele na kujirejea binafsi na kutoka katika kugeuza imani ambayo ni tofauti na “uinjilishaji” unaopaswa kufanywa kwa mtindo wa Yesu.