Papa Francisko na Zahati ya Mtakatifu Marta:tusisahu watoto wa Ukraine!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Siku moja baada ya siku kuu yake ya Kuzaliwa, Dominika tarehe 18 Desemba 2022 ameweza kushiriki kusherehekea na wale wanaofanya kazi katika kituo cha zahanati ya watoto ya Mtakatifu Marta mjini Vatican kwa msaada wa vifaa, matibabu na kiroho. Pia mbele ya baadhi ya familia za Kiukreni ambazo ni mwenyeji jijini Roma, ambapo Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewakumbuka na kuomba kuwasaidia wale wote wanaoteseka kutokana na vita, pia katika sehemu nyingine nyingi za dunia , kutokana na ukosefu wa haki.
Baba Mtakatifu amewashukuru kila mmoja wao, kwa uwepo wao hapo na kwa siku hiyo ya furaha ambapo inawaanda kufikia Noeli. Papa amebainisha kwamba “Na hatupaswi kusahau watoto wa Ukraine, na hakika msiwasahau! alionesha ishara kwa wale waliokuwa wanawakilisha na kusema “Amani”; hapo, ninaona kuna bendera ya Ukraine”.
“Watoto wengi wanateseka na vita; na pia wanateseka katika sehemu nyingine kutokana na dhuluma. Bwana awapatie furaha hii ya kusherehekea Noeli namna hii, sisi sote kwa amani, tuwafikirie pia wale wanaoteseka na tuwaombee, sote kwa pamoja”. Kwa maana hiyo Papa ameongeza kuwashukuru na pia kuwaomba waendelee na tamasha lao.