Jeneza la Papa Benedikto XVI limewekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu asubuhi 2 Januari 2023, watu wengi wameanza kwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Msaafu baada ya mwili wale kuondolewa katika Monasteri ya Mater Ecclesiae na kumweka katia Altare ya Maungamo. Wa kwanza kuingia, saa 8.50, Katika Kanisa kuu la Vatican ambalo lilikuwa bado limefungwa kwa umma na lenye taa za chini, alikuwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, pamoja naye binti yake Laura ambali walisimama kwa muda kidogo upande wa kulia, wakiwa wameshikana mikono, ili kusali na kutoa heshima kwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ambaye mwili wake unaoneshwa kuanzia Jumatatu tarehe 2 hadi tarehe 4 Januari kwa ajili ya ibada ya waamini kwenye Altare ya Maungamo, sawasawa na kilichotokea wakati wa mazishi ya Papa Yohane Paulo II.
Mara baada ya Rais Mattarella, Waziri Mkuu, Giorgia Meloni, Alfredo Mantovano, katibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo Francesco Lollobrigida waliwasili pia. Ishara ya msalaba, kupiga magoti kwa muda mfupi, na pia katulia kwenye moja ya benchi nne za upande. Upande ule mwingine kulikuwa na Kadinali Michael Harvey, kuhani mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta Roma, na watawa fulani waliokuwa na nia ya kusali Rozari kwa sauti ya chini. Kardinali Mauro Gambetti, Mismamizi wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro aliwasalimia waliohudhuria.
Hata hivyo Kardinali Gambeti asubuli mapema Jumatatu 2 aliongoza ibada hiyo iliyoanza saa 7.15 hadi 7.40, baada ya kuhamishwa kwa mwili wa Papa mstaafu kutoka Nyumba ya Mater Ecclesiae, monasteri iliyozungukwa na kijani katika bustani ya Vatican ambapo Papa Mstaa Joseph Ratzinger aliichagua kuwa makazi yake baada ya kung’atuka upapa mnamo 2013. Kutoka katika kikanisa ambalo mwili wa Papa Benedikto ulipumzika siku nzima ya tarehe Mosi ukioneeshwa karibu na msalaba mkubwa, eneo la pango na mti wa mapambo ya Noeli, Askofu Gänswein, Memores Domini ambaye alikuwa ni msaidizi wa Ratzinger kila siku kwa miaka mingi, wasaidizi wa zamani wa Mater Ecclesiae walisali asala fupi, kabla ya mwili wa Papa mstaafu kuhamishiwa katika Kanisa Kuu la Kipapa, pamoja na msafara. Katika safari fupi kando ya njia ya mikondo na miti ambayo siku nzima ya jtarehe mosi, kuanzia ziara za kwanza za kibinafsi za maaskofu na makadinali, ilichukuliwa na mamia ya watu ambao hawakutaka kusubiri ufunguzi wa Kanisa Kuu Jmatatu 2 Januari, walikwenda kufanya ibada, salamu fupi na kutoa heshima za mwisho hivi mtiririko uliodumu hadi alasiri.
Wengi walirudi tena kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro Jumamatu 2 Januari 2022 wakisubiri kwenye foleni, wakiwa wamejifunika kwa mitandio na makoti kwa sababu ya baridi. Makadirio ya kwanza yanazungumza juu ya watu 15,000. Kati ya watu elfu 30 hadi 35 wanatarajiwa kwa siku katika siku tatu za onesho la jeneza kuanzia saa 2 asubuhi hadi tarehe 4 Januari jioni (kwa hiyo kuanzia saa 3 hadi saa 1 Jioni kila siku). Gavana wa Roma, Bruno Frattasi, alikuwa tayari ametarajia kwamba tarehe 5 Januari 5, siku ya mazishi inayoongozwa na Papa Francisko, mmiminiko wa takriban watu elfu 50-60 unatarajiwa!
Wakati huohuo, kikundi cha kwanza, kilipofungua mlango, kilitembea haraka haraka hadi kufikia hatua ya katikati ya Kanisa Kuu ambapo mwili umevalishwa mavazi mekundu ya kiliturujia, mitra nyeupe, viatu vyeusi, bila pallium au msalaba wa kichungaji. Kati ya vidole vilivyounganishwa, kuna Rozari. Kuna wale ambao wanafanya ishara ya msalaba kwa kupiga magoti yao, wale wanaojaribu kupiga hata picha kwa smartphone zao au kuacha tu na kuangalia. Watu wengi wanasimama kwenye vikanisa vya kandoni ili kusali Rozari au kusubiri misa kwenye vikanisa vodogo.