Tafuta

2023.02.24 Wakati wa maonesho ya Filamu ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine, Papa alizawadiwa bendera ya Ukraine. 2023.02.24 Wakati wa maonesho ya Filamu ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine, Papa alizawadiwa bendera ya Ukraine.  (Vatican Media)

Papa:Vita vinaharibu wote na tupande mbegu ndani mwetu ya amani

Katika hafla ya mwaka mmoja tangu kuibuka mzozo wa vita kati ya Ukraine na Urussi,Papa alihudhuria maonesho mjini Vatican ya filamu yenye kichwa“Uhuru motoni:Mapambano ya Uhuru wa Ukraine”,iliyohamasishwa na mkurugenzi Afineevsky.Papa,alisalimiana na baadhi ya wahusika wakuu wa filamu.Hatimaye maombi ili Mungu aponye mioyo,akili na mitazamo yetu.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

“Kwa nini hatuwezi kuishi kwa amani? Ni rahisi hivyo…. Ni swali la kuhuzunisha katika hali hii, kwa sauti ya msisimko, ambapo msichana wa Kiukrene aliuliza Papa, Kanisa, ulimwengu katika filamu yenye kichwa “Uhuru motoni:Mapambano ya Uhuru wa Ukraine”. Kazi hiyo, iliyohamasishwa  na mkurugenzi Evgeny Afineevsky, ilioneshwa alasiri tarehe 24 Februari 2023  katika Ukumbi wa Sinodi Mpya, jinini Vatican katika  siku ya kumbukumbu  ya kile ambacho Papa Francisko amekuwa akikifafanua kuwa vita vya “upuuzi”, yaani baada yam waka mzima wa vita nchini Ukraine ambavyo vinaendelea.

Papa alitazama filamu kuhusu Vita nchini Ukraine
Papa alitazama filamu kuhusu Vita nchini Ukraine

Papa mwenyewe, aliyeketi katika safu ya mwisho, alishiriki katika afla hiyo na alikutana na baadhi ya wahusika wakuu wa filamu hiyo mwishoni mwa maonesho hayo. Miongoni mwao  alikuwa ni Bi Anya Zaitseva, mke wa askari aliyetekwa, huko Ukraine kwa upande wa kulia wa Papa akiwa na Sviatoslav mtoto mdogo, mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne mikononi mwake, ambaye alicheza na kunyonya fimbo ya Papa wakati akitazama filamu au kumpa mabembelezo.

Papa aliwabariki hata watoto na wazazi wao waliokuwa kwenye ukumbi wakati wa kutazama filamu
Papa aliwabariki hata watoto na wazazi wao waliokuwa kwenye ukumbi wakati wa kutazama filamu

Baba Mtakatifu Francisko pia alitaka kuwasalimu baadhi ya wageni takriban 240 ambao walikuwa ni  watu wenye kuhitaji, wakimbizi na wanachama wa jumuiya ya Kiukrene  ya  Roma, walioalikwa na mkurugenzi huyo. Hao walikuwa pamoja na wawakilishi wa vyama mbali mbali vinavyotoa usaidizi na Kadinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Huduma ya Kipapa ya Upendo, kwa mujibu wa taarifa kutoka  Ofisi ya vyombo vya habari vya Vatican.

Papa akipokea zawadi kutoka kwa watu wa Ukraine
Papa akipokea zawadi kutoka kwa watu wa Ukraine

Kwa maana hyo Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya filamu hiyo kuhusu Ukraine alikuwa na ya kusema kwamba:  “Mungu alipoumba mwanadamu, alisema tuichukue dunia, tuifanye kukua na kuwa nzuri. Roho ya vita ni kinyume chake, cha  kuharibu,na hivyo tusiruhusu, kuharibu kila mtu, wanaume, wanawake, watoto, wazee, kila mtu. Leo ni mwaka wa vita hivi. Tutazame Ukraine, tuiombee Ukraine na tufungue mioyo yetu kwa uchungu. Tusione aibu kuteseka na kulia, kwa sababu vita ni uharibifu, vita inatupunguza siku zote. Mungu atujalie kuelewa hili”.

Papa akisalimiana na wajumbe kutoka Ukraine wakati wa kutazama Filamu
Papa akisalimiana na wajumbe kutoka Ukraine wakati wa kutazama Filamu

Na kabla ya kuwabariki Papa aliongeza sala kwamba: “Baba Mtakatifu uliye mbinguni, tazama taabu zetu, tazama majeraha yetu, tazama maumivu yetu, pia tazama ubinafsi wetu, masilahi yetu duni na uwezo tulionao wa kujiangamiza wenyewe. Uponye mioyo yetu, ponya akili zetu, ponya macho ili waone uzuri ulioufanya na usiuharibu kwa ubinafsi. Panda mbegu ya amani ndani yetu”.

Papa akipokea Ua kutoka Ukraine lenya maana kubwa katika nchi ya Ukraine
Papa akipokea Ua kutoka Ukraine lenya maana kubwa katika nchi ya Ukraine

Kabla ya kurudi Nyumbani huko  Mtakatifu  Marta, Papa  Francisko alikutana na mwanamke, mama wa mmoja wa askari waliozuiliwa katika kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, alitekwa na askari wa Urussi na kwa sasa bado ni mfungwa. Kwa msaada wa kuhani mkalimani, mwanamke huyo alimwambia Papa kuhusu kilo 40 ambazo mtoto wake amepoteza katika miezi ya hivi karibuni na alishirikisha  maombi yao kwamba yeye na askari wengine ambao wanapambania kutetea uhuru wanaweza kuwa huru mapema iwezekanavyo. Hu mama limpatia Papa zawadi tatu: ua, ishara ​​ya upinzani mpaka uhuru unapatikana; bendera ya njano na bluu ya Ukraine, ambayo Papa Francisko alibusu na kubariki; mfuko wa chumvi, ambayo ni zawadi ya kawaida kwa utamaduni wa Ukraine.

Wakati wa kutazama filamu inayohusu vita vinavyoendelea huko Ukraine
Wakati wa maonesho ya filamu kuhusu Ukraine
Wakati wa maonesho ya filamu kuhusu Ukraine

Wakati wa kumkabidhi alisema: “Ni chumvi ya dunia, na ni ishara ya nguvu: kile kinachohitajika katika vita kali sana, mbaya sana”. Papa pia alimsalimia mmiliki wa Azovstal, ambapo alipokea zawadi ya mfano kutoka kwake bangili iliyotengenezwa kwa chuma kutoka katika kinu cha chuma. Papa Fransisko alivaa kwenye mkono wake, kisha kama kawaida aliomba kwa ajili yake mwenyewe, akimwakikishia mamombi hayo  kwa ajili ya watu waliouawa.

25 February 2023, 16:01