Papa,Ukraine:Pande zote mbili ziheshimu maeneo ya kidini
Na Angella Rwezauala- Vatican.
Mwishoni mwa Katekesi ya Papa Jumatano 15 machi 2023 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko amewakabidhi kwa Mama Maria mfariji kwa walioteswa na Malkia wa Amani watu waliouawa waathirika wa uchokozi wa Urussi. “Leo, ninaomba pande zinazopigana ziheshimu maeneo ya kidini” Mawazo yake Papa hasa yamewaendea pia kwa watawa wa Kiorthodox wa Kyiv Lavra lakini pia wengine wa madhehebu yote kwamba wote wanahitaji msaada watu waliowekwa wakfu na kila msaada wa Watu wa Mungu.”
Kimbunga nchini Malawi
Mtazamo wa Papa umehamia Malawi, nchi iliyokumbwa na kimbunga cha kitropiki kiitwacho Freddy ambacho katika muda majuma matatu kilisababisha vifo vya watu 130, hasa kuathiri jiji la Blantyre na kusababisha njia ya uharibifu na machafuko. “Ninawaombea marehemu, waliojeruhiwa na waliohamishwa. Mungu awasaidie familia na jamii zilizojaribiwa zaidi na msiba huu”.
Shukrani kwa viongozi wa Argentina
Hatimaye, wakati wa salamu za lugha mbalimbali, Papa akiwahutubia waamini na mahujaji wa Uhispania, anaongeza shukrani zake kwa wanasiasa na viongozi wa kijamii wa Argentina waliomtumia barua ya kumtakia heri kwa miaka kumi ya Upapa wake, iliyoadhimishwa tarehe 13 Machi 2023. Umoja uleule uliooneshwa katika kuandika barua, ndio matakwa ya Baba Mtakatifu, kwamba ingekuwa vyema kuudumisha katika maisha na kazi za kila siku, ili kufanya mazungumzo na kuendeleza taifa kwa pamoja. “Asante kwa ishara hii. Inatokea kwangu kuwaambia kama vile mlivyokusanyika kusaini barua hii, ni vyema kukusanyika kuzungumza, kujadili na kuipeleka nchi mbele”.