Tafuta

Katiba ya kitume 'Praedicate evangelium' yaani 'Hubirini Injili' imetimiza mwaka mmoja tangu kuanza kutumika mnamo tarehe (5 Juni 2022- 5 Juni 2023). Katiba ya kitume 'Praedicate evangelium' yaani 'Hubirini Injili' imetimiza mwaka mmoja tangu kuanza kutumika mnamo tarehe (5 Juni 2022- 5 Juni 2023). 

Ni mwaka tangu kutumika rasmi Katiba ya Kitume:'Predicate evangelium'

Papa Francisko alichapisha Katiba mpya ya Kitume:'Predicate evangelium' yaani 'Hubirini Injili' kuhusu Sekretarieti kuu ya'Curia Romana' na Huduma kwa Kanisa lote Ulimwenguni tarehe 19 Machi 2022.”Katiba ilianza kutumika rasmi 5 Juni 2022 ambayo ilichukua nafasi ya Katiba ya Kitume ya Pastor bonus ya tarehe 28 Juni 1988.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katiba ya kitume Praedicate Evangelium  ya Sekretarieti Kuu, 'Curia Romana' iliyochapishwa Jumamosi tarehe 19 Machi 2022 na kuanza kutumika rasmi tarehe 5 Juni 2022 imeimetimiza mwaka mmoja. Hati hii inapanga mchakato wa mageuzi yanayotokana na mjadala wa kabla ya mkutano mkuu wa 2013 na ambao tayari umetekelezwa kwa kiasi kikubwa katika miaka kumi sasa  iliyopita ya Upapa wa Papa Francisko. Ni andiko linalokita kwa kina na kufanya miongozo ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Kiekuemene wa Vatican, ambao kama madhumuni yake ya awali ulikuwa na jibu la swali kuu kuhusu jinsi gani ya kutangaza Injili katika enzi ya mabadiliko ambayo baadaye yangejidhihirisha, kama Papa Fransisko mara nyingi alivyosisitiza kuwa na mabadiliko ya zama.

Marekebisho hayo yalikuja baada ya yale yaliyoasisiwa na Mtakatifu Yohane  Paulo II  ya ‘Pastor Bonus’, 1988, ambayo kwayo ilirekebisha ile iliyotangazwa na Mtakatifu Paulo VI ya ‘Universi depositini Ecclesiae’ ya 1967). Kwa njia hiyo kipaumbele cha Uinjilishaji na nafasi ya waamini walei ni mawazo makuu yanayounganisha Katiba mpya ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican.

Mwaka mmoja tangu kutumika rasmi kwa katiba ya kitume Praedicate evangelium
05 June 2023, 17:57