Tafuta

2023.09.23  Papa Francisko ametembelea kituo cha Watawa  wamisionari wa Upendo wa  Mama Teresa wa Kalkuta wanaotoa msaada kwa watu maskini. 2023.09.23 Papa Francisko ametembelea kituo cha Watawa wamisionari wa Upendo wa Mama Teresa wa Kalkuta wanaotoa msaada kwa watu maskini.   (Vatican Media)

Papa atembelea Utume wa Upendo wa Kimisionari:udugu ni unabii

Papa,akiwa huko Marsiglia ametembelea kwa faragha Nyumba ya Masista wa Mama Teresa wa Kalkuta huko Mtakatifu Mauront,kikundi cha watu walio katika hali ngumu ya kiuchumi wakisaidiwa na watawa hao.Katika ushuhuda wa Sr.Crosvita amebainisha kuwa kwa kila mtu wanayemwona ni kama Kristo."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kwa  tabasamu alikuwa akizungumza na kundi alilokutana nao kuwa Kupeana mikono ni ishara ya udugu na kuishi kama ndugu ni unabii. Hii ilikuwa katika siku ya pili ya Papa akiwa Marsiglia tarehe 23 Septemba 2023 iliyofunguliwa  kwa mkutano wa faragha na baadhi ya watu walio katika hali ngumu ya kiuchumi na inayofanyika kwenye Nyumba ya Wamisionari wa Upendo, watawa wa Mama Teresa wa Calcutta, huko Mtakatifu  Mauront, moja ya vitongoji kati ya watu maskini zaidi nchini Ufaransa.

Papa amekutana na wahitaji wanaohudumiwa na watawa wa Mama Teresa wa Kalkuta
Papa amekutana na wahitaji wanaohudumiwa na watawa wa Mama Teresa wa Kalkuta

Papa Francisko bila hotuba iliyotarishwa alisema: "Asante kwa makaribisho yenu, kwani sisi sote ni ndugu, hii ni muhimu: udugu. Mara nyingi ustaarabu wetu unatuongoza kuishi kama maadui au wageni. Ishara ya kinabii ni kuishi kama ndugu na huu ni unabii!, ule wa udugu unaokwenda zaidi wa mawazo ya kisiasa na kidini,” alisema Papa Francisko. Kwa hiyo salamu za Papa zilikuwa ni shukrani kubwa kwa watawa hao kwamba:  “Asante kwa ushuhuda wenu ambao mmeniambia, nami nimefurahi kuwa nanyi hapa.” Alisema hayo mara baada ya Msimamizi wa watawa na wageni kuzungumza.

Watawa wa Mama Teresa na Papa
Watawa wa Mama Teresa na Papa

Kwa upande wa Sr Crosvita alimmsimulia  Papa kwa hisia kali kwamba kwa miaka miwili akiwa Marsiglia yeye na Masista wenzake wamekuwa wakiendesha jiko la kupika supu kwa ajili ya maskini, ambalo linakaribisha watu 50 kwa wakati mmoja, mara 3-4 kwa siku, kuanzia saa 3. 30 hadi 5.30 na katika siku moja inaweza kuwafikia watu  250.

Hawa ni maskini alieleza mtawa  huyo kuwa wengine wanaishi mitaani, hivi karibuni kuna kundi la watu wamefika kutoka Sudan, hawana pa kukaa, wanalala mitaani. Halafu pia kuna watu ambao wakipata sehemu ya kulala hawana chakula kwa jiyo tunawakuta hapa kuanzia asubuhi na mapema."

23 September 2023, 17:32