Papa atuma Salamu za rambi rambi nchini Brazil
Vatican News
Mshikamano na sala zilioneshwa na Baba Mtakatifu Francisko katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican iliyotumwa kwa Askofu Mkuu Leomar Brustolin, wa Jimbo Kuu Katoliki la Mtakatifu Maria na rais wa Kanda ya Kusini ya 3 ya Baraza la Maaskofu wa Brazil kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la Rio Grande katika siku za hivi karibuni na kuacha nyuma yake uharibifu na vifo. Kwa hiyo, Baba Mtakatifu kwa kujali kwake amewabariki watu wote walioathiriwa na mafuriko makubwa, na anawahakikishia sala na maombi ya haki kwa pumziko la milele kwa wale wote waliopoteza maisha yao na vile vile majeruhi waliopoteza nyumba, huku akitumaini kwamba ujenzi upya wa maeneo hayo utafanyika haraka na kwa ufanisi.”
Idadi ya waathrika inaongezeka
Wakati huo huo, idadi ya vifo kutokana na kimbunga kilichopiga kusini mwa Brazil Jumatatu tarehe 4 Septemba 2023 bado kinaendelea kuongezeka. Mamlaka za nchi hiyo zinazungumza kuhusu watu 41 waliofariki, 46 hawajulikani walipo na 223 kujeruhiwa. Misako inaendelea na zaidi kuona juu ya usalama wa raia wa Jimbo la Rio Grande do Sul ambapo jumla ya watu elfu 11 wamelazimika kuacha makazi yao. Majengo mengi yaliharibiwa na miji ikafurika, huku manispaa 87 zikiathirika kwa jumla.