Tafuta

Papa amesali mbele ya Picha ya Bikira Maria Salus Populi Romani,baada ya kutoka Mongolia katika Ziara yake ya Kitume nchini Mongolia(31 Agosti-septemba 4). Papa amesali mbele ya Picha ya Bikira Maria Salus Populi Romani,baada ya kutoka Mongolia katika Ziara yake ya Kitume nchini Mongolia(31 Agosti-septemba 4). 

Sala ya Papa mbele ya Salus Populi Romani kushukuru kwa ziara yake

Mwishoni mwa Ziara yake ya 43 ya Kitume nchini Mongolia,Papa Fransisko amepitia tena katika eneo lake muhimu la ibada kwa Mama Maria kumshukuru Bikira kwa mafanikio ya hija yake katika moyo wa Asia.

Vatican News

Mara baada ya kurejea kutoka Nchini Mongolia, kama kawaida yake ya hitimisho la Ziara yake ya kitume, tarehe 4 Septemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko alikwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, ambalo alitulia katika sala mbele ya Picha ya Bikira Salus populi romani, yaani Bikira Afya ya Watu wa Roma.

Kwa njia hiyo kama ilivyo desturi yake, hata kabla ya kuondoka katika hija yake ya 43 ya Kitume kimataifa ambayo ilimuona akienda katikati ya moyo wa Asia mnamo tarehe 31 Agosti 2023, alikuwa amekwenda kujikabidhi kwa Mama Maria. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari Vatican, vimeeleza kuwa mwishoni mwa sala yake katika Kanisa Kuu la Kiroma, Papa alirejea mjini Vatican.

Hata hivyo kwa kujitoa kwake kwa Maria ambako  kunatambulika, kumethibitishwa kwa mara nyingine tena  katika  fursa ya kipekee katika muktadha wa matukio ya kusisimua zaidi ya ziara yake huko Ulaanbataar ambapo tulimuona akimtembelea Bi Tsetsege, mama wa watoto kumi na mmoja, ambaye miaka kumi iliyopita aliokota sanamu ya Bikira kwenye shimo la takataka na sasa kwa waamini wa Mongolia anaitwa "Mama wa Mbinguni."

04 September 2023, 19:00