Papa atoa wito kwa ajili ya Myanmar,Palestina,Israel na Ukraine
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatififu Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 19 Novemba 2023 akiwageukia Waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, amewafahamisha juu ya Jumamosi tarehe 18 Novemba 2023 huko Seville, Manuel Gonzales-Serna, Padre wa jimbo na Mapadre kumi na tisa wenzake na walei, waliouawa mwaka wa 1936 katika mazingira ya mateso ya kidini ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania, walitangazwa kuwa wenyeheri. Wafia imani hawa walimshuhudia Kristo hadi mwisho. Mfano wao na uwafariji Wakristo wengi ambao katika nyakati zetu wanabaguliwa kwa ajili ya imani yao. Kwa njia hiyo ameomba kuwapongezwa hao wenyeheri wapya…..
Baba Mtakatifu amendelea kusema kuwa anawaweka kwa upya ukaribu wangu kwa watu wapendwa wa Myanmar, ambao kwa bahati mbaya wanaendelea kuteseka kutokana na vurugu na unyanyasaji. Ninaomba kwamba wasivunjike moyo na kutumaini msaada wa Bwana kila wakati. Papa pia amewageukia kaka dada wote waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwamba tuendelee kuiombea Ukraine inayoteswa - aliona bendera hapo - na kwa watu wa Palestina na Israel. Amani inawezekana. Inachukua mapenzi mema. Amani inawezekana. Tusijitoe kwenye vita! Na tusisahau kwamba vita daima, daima, daima ni kushindwa. Watengenezaji wa silaha pekee ndiyo wanaofaidika.
Siku ya Maskini duniani.
Baba Mtakatifu amesema kuwa, Leo tunaadhimisha Siku ya VII ya Maskini Duniani, ambayo mwaka huu inaongozwa na kaulimbiu, "Usiwaondolee macho maskini" (Tb, 4,7). Ninawashukuru wale wote wa majimbo na Parokia ambao wamehimiza mipango ya mshikamano na watu na familia zinazojitahidi kusonga mbele. Na siku hii pia tunawakumbuka wahanga wote wa barabara: tuwaombee, kwa ajili ya familia zao na tujitoe katika kuzuia ajali. Baba Mtakatifu amependa kutaja Siku ya Uvuvi Duniani, ambayo itaadhimisha tarehe 21 Novemba 2023. Amewasalimu wote kwa upendo, mahujaji kutoka Italia na sehemu nyingine za ulimwengu.
Amewasalimu waamini wa Madrid, Ibiza na Warsaw, na washiriki wa Baraza la Umoja wa Walimu Wakatoliki Ulimwenguni. Amewasalimu vikundi kutoka Aprilia, Mtakatifu Ferdinando di Puglia na Mtakatifu Antimo; Chama cha FIDAS cha Orta Nova, na washiriki katika "Siku za Kushiriki" za Harakari ya Kitume ya Vipofu. Salamu maalum kwa jumuiya ya Ecuador ya Roma, ambayo inaadhimisha siku kuu ya Bikira wa Quinche. Na salamu kwa watoto wa Mama wa Moyo Safi. Kwa kuhitimisha amewatakia Dominika Njema na tafadhali wasisahau kumuombea. Amewatakia mlo na mchama mwema.