Papa Francisko:Kazi ya dini ni kuwa mfano mzuri kwa ajili amani na tabianchi

Papa katika ujumbe wake kwa njia ya video uliooneshwa Dubai kwa ajili ya uzinduzi wa Banda la Imani ambalo ni nafasi ya harambee karibu ya Mashirika mia moja,viongozi wa kidini na kisiasa na wanasayansi ili kukuza hatua ya hali ya tabianchi amewaeleza kuwa "Watoto na masikini hasa wanatuomba.Ni jambo la dharura kuwa na imani bila kuangukia katika mtego wa ulinganifu kwa kuunda miunganisho na si kwa maslahi binafsi au ya chama kimoja,bali kwa ajili ya maslahi ya ulimwengu wetu."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kuunda miunganisho kwa  ajili ya manufaa ya wote. Ni moyo wa ujumbe kwa  njia ya video ambao  Baba Mtakatifu Francisko  ameutuma huko Dubai akielezea juu ya masikitiko yake ya kutokuwepo kwenye hiyo  COP28 na kumkabidhi tena Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, kile alichokiandaa kwa ajili ya uzinduzi wa "Faith Pavillon" yaani “Banda la Imani.” Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza  umuhimu wake  kwani hiyo ni kwa mara ya kwanza kwa banda la kidini kuundwa ndani ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.


Ulimwengu unahitaji miunganisho kwa  ajili ya maslahi ya kila mtu. Katika ukweli ambao COP28 inayoendelea katika Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu inakaribisha Banda la Imani ambapo ni ishara ya kutaka kuonesha kwamba inawezekana kuunda miungano yenye faida kwa  ajili ya maslahi ya pamoja. Miongoni mwa haya Papa anasema “ya muhimu zaidi leo ni amani na hali ya tabianchi." “Leo dunia inahitaji miungano ambayo si dhidi ya mtu yeyote, bali kwa kila mtu. Ni jambo la dharura kwamba dini, bila kutumbukia katika mtego wa ulinganifu, ziweke mfano mzuri kwa kufanya kazi pamoja: si kwa maslahi yao wenyewe au ya chama kimoja, bali kwa ajili ya maslahi ya ulimwengu wetu.

Kwa siku zijazo hasa za watu walio hatarini zaidi na mustakabali wa wote, himizo la Papa Francisko ni kulinda  kazi ya uumbaji na kulinda nyumba yetu ya pamoja. Kwa hiyo Papa ametoa mwaliko kuwa, “Tuishi kwa amani na kuendeleza amani!" Aidha Papa amesema kuwa "Tunaongoza kwa mfano, kama wawakilishi wa kidini, kuonesha kwamba mabadiliko yanawezekana, kutoa ushuhuda wa maisha ya heshima na endelevu, na tunaomba kwa sauti kubwa viongozi wa mataifa kwamba nyumba ya pamoja ihifadhiwe. Hili linaombwa kwetu, hasa, na watoto na maskini, ambao maombi yao yanafikia kiti cha enzi cha Aliye Juu."

Papa akiweka saini katika Tamko kwa ajili ya COP28

Banda la kwanza la Imani litakuwa kipaumbele  ili kuwa kitovu cha kukuza ushirikiano na umoja  wa imani kati ya dini mbalimbali, kwa lengo la kuchochea hatua madhubuti na kabambe ya hali yatabianchi. Litaunda fursa ya mazungumzo na wawakilishi wa kidini na wazalendo, wanasayansi, vijana na viongozi wa kisiasa ili kuharakisha hatua za hali ya tabianchi. litakuwa mwenyeji zaidi ya vikao 60, vinavyowakilisha zaidi ya mashirika 100.

Ujumbe kwa njia ya video wa Papa kwa COP28
03 December 2023, 11:08