Tafuta

Papa Francsiko amekutana na Meya wa Mji wa Roma pamoja na viongozi wa Mji wa Roma Papa Francsiko amekutana na Meya wa Mji wa Roma pamoja na viongozi wa Mji wa Roma  (ANSA)

Meya wa Roma,Mkuu wa Mkoa wa Lazio na ujumbe wao wakiwa na Papa

Roberto Gualtieri, Meya wa Mji wa Roma na Mkuu wa Mkoa wa Lazio,Francesco Rocca tarehe 4 Januari 2024 walikuwa katika Jumba la Kitume kwa ajili ya mkutano wa utamaduni,mwanzoni mwa mwaka na Papa Francisko.Meya baadaye katika mtandao wa kijamii aliandika:“Ni furaha kumwonesha maendeleo ya mipango ya Jubilei.Roma inampenda Askofu wake."

Vatican News

Kama ilivyo desturi ya kila mwanzoni wa mwaka mpya, wa kutakiana heri,Baba Mtakatifu Francisko aliwapokea Meya wa Roma, Bwana Roberto Gualtieri, na Mkuu  wa Mkoa wa Lazio, Bwana Francesco Rocca, katika mkutano uliofanyika tarehe 4 Januari 2024, katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Mikutano hiyo ilifanyika tofauti, mwishoni mwa asubuhi  hiyo iliyokuwa imejaa vikao ving vya Papa Francisko.

Papa na Meya wa Mji wa Roma
Papa na Meya wa Mji wa Roma

Gualtieri: mkutano wa kutia moyo sana

Katika akaunti yake ya Facebook, Bwana Gualtieri alielezea juu mkutano huo na Papa  Francisko kama mkutano wenye msukumo wa kina: “Ilikuwa jambo la kufurahisha kumwonesha maendeleo ya kazi ya mipango mingi ambayo tumeweka kwa ajili ya Jubilei, kwa kukaribisha na kutunza watu walio dhaifu”, aliandika Meya wa Mji wa Roma

Meya wa Mji wa Roma na Papa Francisko 4 Januari 2024
Meya wa Mji wa Roma na Papa Francisko 4 Januari 2024

“Ninamshukuru Baba Mtakatifu kwa mafundisho yake, kwa kujitolea kwake bila kuchoka kwa walio hatarini zaidi na kwa maneno yake ya ukarimu ya kuunga mkono na kutia moyo.” Bwana Gualtieri tena kupitia jukwaa la kijamii:  "Roma inampenda Askofu wake, ambaye anawakilisha vyema wito wake wa mshikamano, udugu na amani.”

Papa tarehe 4 Januari 2024 alikutana na Meya wa Mji wa Roma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lazio
05 January 2024, 11:49