Papa:vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu,tuelimishe kwa ajili ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana kwa Mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 14 Januari 2024 amesema: “Ninatoa salamu zangu kwenu ninyi nyote, Warumi na mahujaji wanaotoka Italia na kutoka sehemu nyingi za dunia. Hasa ninawasalimu washiriki wa Ndugu wa Sakramenti ya Mama Yetu wa Villarrasa (Hispania). Tusisahau kuwaombea wahanga wa maporomoko ya ardhi yaliyotokea nchini Colombia, ambayo yalisababisha wahanga wengi.”
Baba Mtakatifu akiendelea aidha alisema: “Na tusiwasahau wale wanaokabiliwa na ukatili wa vita katika sehemu nyingi za dunia, hasa Ukraine, Palestina na Israel. Mwanzoni mwa mwaka tulitakiana matashi mema ya amani, lakini silaha ziliendelea kuua na kuharibu. Tunaomba wale walio na mamlaka juu ya migogoro hii watafakari ukweli kwamba vita sio njia ya kutatua, kwa sababu inapanda vifo kati ya raia na kuharibu miji na miundombinu.”
“Kwa maneno mengine, leo vita yenyewe ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Tusisahau hilo kwamba: vita yenyewe ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wananchi wanahitaji amani! Dunia inahitaji amani! Dakika chache zilizopita, katika kipindi cha A Sua Immagine yaani "Katika Picha Yake", nilimsikia Padre Faltas, Padre Msimamizi wa Nchi akatifu huko Yerusalemu, alizungumza juu ya kuelimisha amani. Ni lazima tuelimishe juu ya amani.” Tunaona kuwa bado hatujawa na elimu ya kutosha-ubinadamu wote-kukomesha kila vita. Tuombe daima neema hii: kuelimisha amani.Ninawatakia Dominika njema. Tafadhali Msisahau kuniombea. Mlo Mwema mchanana kwaheri ya kuonana!" Papa Francisko amehitimisha.