Tafuta

2024.01.20 Papa akutana na Wajumbe wa Baraza la Kitaifa la  Harakati ya Upyaisho wa Roho. 2024.01.20 Papa akutana na Wajumbe wa Baraza la Kitaifa la Harakati ya Upyaisho wa Roho.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Wakarismatiki amesisitiza juu huduma ya sala na Uinjilishaji

Papa alikutana na rais na wajumbe wa Baraza la Kitaifa la Upyaisho wa Roho Mtakatifu.Tangazo la kwanza linatolewa na ushuhuda wa maisha kwani.“Nimechukizwa na wanaume na wanawake ambao wana wazazi wao katika makazi ya kutunza wazee lakini hawaendi kuwatembelea.Si nyimbo nzuri na sala ndefu tu bali ishara thabiti za upendo.”

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Baraza la Kitaifa la Harakati ya Uhuisho wa Roho Mtakatifu tarehe 20 Januari 2024. Katika hotuba yake amemsalimia Rai na wajumbe wote pamoja na washiriki wa Harakati hiyo.  Kama wanavyojua, katika miaka ya hivi karibuni Papa alitangaza CHARIS kama shirika la huduma ya kimataifa la Upyaishaji wa Karismatiki Katoliki. Na hata hivi  karibuni mwezi  Novemba 2023,  Papa alipata fursa ya kuzungumza na washiriki wa mkutano ulioandaliwa na CHARIS.  Kwa njia hiyo amewahimiza kuendelea kutembea kwenye njia hiyo  ya ushirika na kufanya kuwa tunu ya maelekezo aliyowapatia. Papa Francisko akiwa nao wanaosimamia harakati katika ngazi ya kitaifa amewaomba awashirikishe mtazamo wa kichungaji kuhusu uwepo wao na huduma yao. Awali ya yote Papa amemshukuru Bwana na kushukuru kwa mema ambayo jumuiya za Harakati hiyo hupanda kati ya Watu watakatifu, waaminifu wa Mungu, kwa kusaidia hata hali ya kiroho rahisi na yenye furaha. Papa amesisitiza mantiki mbili muhimu: Huduma katika sala hasa ya kuabudu, na huduma ya Uinjilishaji.

Papa na wajumbe wa Baraza la Kitaifa la uhuisho wa Ro Mtakatifu
Papa na wajumbe wa Baraza la Kitaifa la uhuisho wa Ro Mtakatifu

Harakati ya Karismatiki kwa asili yake hutoa nafasi na umuhimu kwa maombi, kwa namna ya pekee kwa sala ya kutoa sifa, na hii ni muhimu sana. Katika ulimwengu unaotawaliwa na utamaduni wa kuwa na ufanisi, na pia katika Kanisa wakati mwingine unaohusika sana katika shirika, Papa ametoa angalisho la  kuwa makini na hilo! “Sisi sote tunahitaji kutoa nafasi kwa kutoa  shukrani, sifa na mshangao mbele ya neema ya Mungu.”  Papa Francisko amewaomba hao ndugu kuendelea na kulitumikia Kanisa katika hilo, hasa kwa kuendeleza maombi ya kuabudu. Ibada ambayo ndani yake ukimya utawale na , ambapo Neno la Mungu lishinde maneno yetu, kwa kifupi Papa amesisitiza kuwa  iwe ibada ambayo Yeye, Bwana, awe  katikati, na sio sisi.”Hiyo ndiyo mantiki ya kwanza ambayo Papa amewashukuru na kuwatia moyo kwa sala. Baba Mtakatifu akiendelea amesema: “Mantiki ya pili ni ile ya uinjilishaji, ambayo pia ni, kwa kusema, kuwa ni kinasaba ( DNA) cha  Harakati ya Karismatiki. Roho Mtakatifu, akikaribishwa ndani ya moyo na maisha, hawezi kujizuia kufunguka, kusonga, kufanya kutoka nje; Roho daima hutusukuma kuwasilisha Injili, kwenda nje, na anafanya hivyo kwa mawazo yake yasiyoisha.” Kwa upande wetu tunatakiwa kuwa wanyenyekevu na kushirikiana Naye, kama  tunavyosimuliwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume tunavyoambiwa na Stefano, Filipo, Barnaba, Petro, Paulo na wengine. Hawa hawakuwa na mwongozo wa jinsi gani ya kuendelea,  bali walikuwa ni Roho Mtakatifu  aliyewasukuma na wakafanya mambo mengi makuu.” Papa amesisitiza na kuongeza:  Na daima kumbukeni  kwamba tangazo la kwanza linatolewa kwa ushuhuda wa maisha!”

Je kuna maana gani kufanya maombi marefu na nyimbo nyingi nzuri, ikiwa sijui kuwa na subira na jirani yangu, ikiwa sijui kukaa karibu na mama yangu aliye peke yake  ambayo pia ni amri ya nne,” Papa amesisitza na kuongeza: “Ninachukizwa na wanaume na wanawake ambao wana wazazi katika makazi  ya kutunza na hawaendi kuwatembelea,  au kwa mtu huyo aliye shida ... Msaada wa dhati, huduma iliyofichwa kila wakati ni uthibitishaji wa tangazo letu. Kwa njia hiyo ni maneno, ishara na nyimbo, bila uthabiti wa upendo, ni bure,” Papa amesisitiza. Ni sala na uinjilishaji. Papa ameongeza “Lakini ikiwa mmekuja kwa Papa sio tu kuthibitishwa katika njia hizi mbili ambazo ni karama yenu na historia yenu. Mrithi wa Petro pia ana karama, ambayo ni ile ya umoja, na zaidi ya yote anaweza na lazima kuthibitisha. Ushirika awali na yote na maaskofu wenu. Mnajua vyema, katika kila Kanisa mahalia Harakari  za kikanisa lazima daima zitafute ushirika wenye ufanisi. Na hii ina maana gani? Ina maana kwamba jumuiya ya Upyaisho lazima iwe katika huduma ya jumuiya nzima, jimbo, jumuiya nzima ya parokia, kulingana na maelekezo ya  kichungaji ya Askofu.

Ushirika pia na ukweli mwingine wa kikanisa, vyama, Harakati, vikundi na  kutoa ushuhuda wa udugu, kuheshimiana katika utofauti, ushirikiano katika kujitolea kwa mipango ya pamoja, katika huduma ya watu wa Mungu na pia juu ya masuala ya kijamii ambayo kuna hatari ya hadhi ya watu. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa ahadi ambayo tayari wanajiwekea katika hilo  na amewasihi wawe wajenzi wa ushirika, kwanza kabisa kati yao wenyewe na wawe makini na  mazungumzo. “Umoja kati yenu, hii ni muhimu sana; na pia, umoja wa  ndani ya harakati zenu, na kisha katika parokia na majimbo.” Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru tena kufika kwao. Amewaomba wandelee mbele kwa Furaa. Mama Maria awalinda, na daima awe katikati yao kama alivyokuwa katikati ya Mitume wa Kwanza katika karamu kuu (Mdo 1,14).

Wajumbe wa Baraza la Wakarismatiki kitaifa
Wajumbe wa Baraza la Wakarismatiki kitaifa

Papa Francisko kwa kuongezea ametoa ushuhuda wake binafsi kwamba : “Nilikuwa na historia maalum na ninyi, kwa sababu mwanzoni nilikuwa sipendi harakati, nilisema ni shule ya samba na sio harakati za kikanisa. Kisha kama Askofu Mkuu niliona jinsi walivyofanya kazi, na  jinsi walivyojaza Kanisa kuu wakati wa mikutano na nilianza kuwa na shukrani kubwa kwenu. Endeleeni  mbele, lakini si kama shule ya samba, bali kama harakati ya kikanisa.” Na kwa kuhitimisha Papa Francisko amewabariki kwa moyo na  huduma yao. Amewaomba tafadhali wasali kwa ajili yake.

20 January 2024, 13:58